CHADEMA Asilia v/s CHADEMA Pesa

CHADEMA Asilia v/s CHADEMA Pesa

iArmaniAdamson

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
944
Reaction score
289
Ni kweli na dhahiri kwamba ujio wa Lowassa umeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama cha mabadiliko. Chama kimebadilika kweli kweli..

Inasikitisha kuona chama kilichofanya kampeni ndefu zaidi ya vyama vyote, yaani miaka 7 na miezi minne leo hii kimegeuka kuwa kituko..

Leo tuangalie tabia za wanachadema ASILIA (watoto wa Mungu) na Chadema PESA (Mkapa aliwaita malofa), chini ni listi ya tabia zinazoashiria makundi haya:-

CHADEMA ASILIA:
* Hawa ni WAZALENDO na hawanunuliki hata kwa milioni 300
* Hawa ni wasomi na watu makini sana na huwezi kuwaona kwenye mikutano ya Lowassa
* Hawa wanajua CCM sio tatizo bali tatizo ni kiongozi, wakati wa Nyerere na Mwinyi hakukuwa na udokozi wa hali hii
* Hawa wanajua HAWAWEZI KUMCHAGUA MTU aliyekuwa kwenye LISTI OF SHEM.
* Hawa wanajua ndani ya CCM, Warioba, Msuya, Mwandosya, na wengine wengi sana sio mafisadi bali ni watu wachache wasiozidi kumi
* Hawa HAWAJAPOTEZA kumbukumbu, wanajua MWIZI NI MWIZI TU na hawababaishwi na MACHOZI ya MAMBA.
* Hawa wanajua maendeleo hayaletwi leo wala kesho na kwao cha muhimu ni Maendeleo bora na sio bora maendeleo
* Hawa watazienzi harakati za Zitto na Dr Slaa na kamwe hawatateteleka
* Hawa wanajua umaskini anaochukia Lowassa ni umaskini wake mwenyewe

CHADEMA PESA:
* Hawa kwa kiasi kidogo cha shilingi 1,000 mpaka 2,000 wako tayari kuvaa shati na kofia ya CCM na kushangilia sana!
* Hawa huwa hawataki kuongelea sera maana hazipandi
* wengi wao huwa wanaonekana wajanja mpaka pale wanaposema serikali imeuza twiga wote!
* Wanamchukia sana Dr Slaa na kila anachosimamia kwa sasa
* Hawa wengi HAWANA KUMBUKUMBU ya kampeni ya kuuwa ufisadi nchini au wamejitoa akili hivi majuzi
* Hawa wanamwita Lowassa MPAKWA MAFUTA!
* Hawa wanadhani CCM ni pepo badala ya chama
* Hawa wanadhani CCM ni mkapa, ridhiwani, Raisi kikwete, tibaijuka na chenge
* Hawa wanadhani watumishi wote serikalini wanatibiwa India.
* Hawa NI WATU WA MATUSI TU, hawawezi kuandika bila kuteleza na tusi

SWALI:
JE WEWE NI CHADEMA GANI??? (Kura yako ni Siri yako)
 
Ngoja uchaguzi upite kwanza, tutarudi kuyajadili hayo, saivi ni Lowasa tu.
 
Hivi mfumo wa chama uliyotutesa miaka yote na mtu mmoja aliye amua kujitenga na huyo mfumo hata kama inaaminika ni mbaya wapi bora/afadhali? Dr amewahi kukaririwa akisema binadamu kiasili hapendi uovu ila akikabiliwa na mabadaya mawili atachagua baya dogo...Tafakati.
 
mimi ni chadema asilia ndo maana nimeamua kumfuata dr slaa.

Slaa hayupo Chadema tengenezeni chama lenu,,,,mmeikuta Chadema mtaiacha,,,muende tu kelele za nn?nyie asilia mtei asemeje sasa?
 
Jameni tarehe 25 tiki kwa mzee mwenye nywele kama za Nyerere na Mandela
tiki kwa wabunge na madiwani wa ukawa
peopleeeeessss (in mbowe's voice)
 
DK SLAA VS WANAUKAWA KUNA TOFAUTI?
Dk
Slaa
1) Ninajua kuwa Lowasa ni fisadi
2) Ninajua
kuwa Magufuli ni fisadi alimpa kimada nyumba
za serikali.
3)Najua kuwa kuna vyama safi na
vinawagombea wasafi kuliko ccm na chadema.
4) Lakini naomba mumchague Magufuli pamoja
na ufisadi wake na chama chake cha ccm!
WANAUKAWA
1) Tunajua kuwa Lowasa ni fisadi.
2) Tunajua kuwa Magufuli naye ni fisadi alimpa
kimada na ndugu zake nyumba za serikali.
3)
Tunajua kuwa kuna vyama visafi na
vimesimamisha wagombea wasafi.
4) Lakini
tunaomba mumchague Lowasa pamoja na ufisadi
wake na umoja wa UKAWA.
Si Dk Slaa wala
UKAWA wa kumuona mwingine amepotoka!
 
Mi nampenda slaa ila kwa sasa anisamehe tu,lowasa kwanza hayo mengine baadae
 
Chadema asilia tunasuburi chama chetu October 25,mabadiliko fake yatavyoshindwa kwa aibu.
 
M4c kura yangu sitapeleka ccm hata ningewekkewa bomu
 
chadema pesa kwa upumbavu kila jina kubwa ni mtu mashuhuri. ndio maana wanawapapatikia makapi waliotemwa ccm. kingunge mchovu wa akili wanamuona jembe. mzee huyu alishatemwa kwa ufisadi wa kampuni yake ubungo terminal. bado anaimba lugha ya kijamaa wakati anaungana na mafisadi wenye kupiga santuri tofauti. huyu mzee naye amekua msanii. sijui leo arusha ataimba wimbo gani kwa dakika 40 wakati mgombea wake urais anatumia sio zaidi ya dakika 10.
 
Back
Top Bottom