Chadema Arusha yazindua Join the Chain Ambassadors kwa mafanikio makubwa

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Leo tarehe 07/05/2022 timu ya mabalozi wa Join the Chain ( Join the Chain Ambassadors ) Arusha iliingia ndani ya Soko Kuu Arusha na soko la Kilombero kukusanya michango ya wadau mbalimbali wa chama kupitia program ya kuchangia chama ya Join the Chain.
Wadau wengi walifurahi sana na walijitoa kuchangia chama kwa furaha kubwa.

Zoezi hili la kuchangia chama kupitia program ya Join the Chain litakuwa ni zoezi endelevu. Hivyo mabalozi wa Join the Chain wanawaalika makamanda wengi zaidi kutoka Kanda ya Kaskazini kuendelea kuchangia chama kupitia ununuzi wa tshirt za Join the Chain Ambassadors pamoja na kwenda kwa wadau.

Zoezi hili limeendeshwa na Uongozi wa Mkoa,Mwenyekiti Elisa Mungure
Wilaya,Nanyaro EJ Mwenyekiti,Viola Katibu,baba boni na wengine wengi
Ema Saro Mwenyekiti wa Wilaya ya Siha
Mh Pamela Masay Mbunge wa EALA
Kamanda Dorisi Cornel kutoka jimbo la Hai
na wanachama ambalo limekuwa na mafanikio makubwa sana,

Wananchi wamechangia mia tano,elfu etc na kuonyesha maana halisi ya nguvu ya umma.

Kwa pamoja tuunge mnyororo

IMG-20220507-WA0044.jpg

IMG-20220507-WA0076.jpg

IMG-20220507-WA0037.jpg

IMG-20220507-WA0059.jpg
 
Dondosha picha za Mapokeo ya wananchi tuone uhalisia badala ya kutuonyesha picha za wapiga promo wenyewe!
 
Wizi tu, unapokeaje Hela bila risiti? Kuna wengine hapa dar es salaam baada ya kuingia katika kampeni hiyo, wakaanza kunenepa kama paka wa baa, wanakula tu michango
 
Wizi tu, unapokeaje Hela bila risiti? Kuna wengine hapa dar es salaam baada ya kuingia katika kampeni hiyo, wakaanza kunenepa kama paka wa baa, wanakula tu michango
Wewe ni kilaza tu,nenepa na wewe kwani umenyimwa?
Risiti kila mtu anapewa hata akichanga mia moja
 
Wizi tu, unapokeaje Hela bila risiti? Kuna wengine hapa dar es salaam baada ya kuingia katika kampeni hiyo, wakaanza kunenepa kama paka wa baa, wanakula tu michango
Wewe kidole tumbo, ulishawahi kupewa risiti ukitoa mchango au sadaka unatumia solar kufikiri wewe
 
Wewe kidole tumbo, ulishawahi kupewa risiti ukitoa mchango au sadaka unatumia solar kufikiri wewe
Hapo ndio mnaiba, mnarudi majumbani na viroba vya samaki, nyama na nyanya, huku matumbo yametuna bia na nyama haramu
 
Kazi nzuri Sana Mwenyekiti Nanyaro na Team yako yote.

Chadema Arusha inazidi kujikita na Wananchi tunawaunga mkono sana
 
CHADEMA ni chama Kikubwa na wananchi wanalitambua hilo hivyo itoshe niseme ya kwamba tunakoelekea ni pazuri mno kuliko tulikotoka✌🏻🙏🏻🙏🏻

CHADEMA DAIMA MBELE💪🏻💪🏻🙏🏻🙏🏻
 
Back
Top Bottom