CHADEMA Arusha wapongezwa na wananchi kwa kutekeleza ahadi za maendeleo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Habari zilizonifikia kutoka jiji la Arusha ni kuwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema ambacho ndio chama kilichoshika jiji la Arusha limeanza kufanya kazi na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.

leo wameanza na ujenzi wa kiwango cha lami kwenye barabara iliyokua imesalia eneo la kaloleni kuweka Lami, vilevile barabara ya Ilboru mita 200 wameanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe.

kweli wananchi na wakazi wa jiji la Arusha, wameonyesha furaha zao walipokua wanaojiwa na mwandishi pale waliposema haya mambo walikua wameshayasahau katika jiji hilo mambo ya maendeleo walikua wanayaona kwenye vitegauchumi binafsi vya wanaccm peke.

wakazi wa Arusha wamemshukuru Meya na Diwani Kessy wa Kata hiyo ya Kaloleni kwa kuwaletea maendeleo hayo pia wamewapongeza madiwani wote wa chadema katika jiji la Arusha kwa kusema wanaona maendeleo na usafi wa jiji la Arusha.

IMG-20160714-WA0068.jpg

IMG-20160714-WA0060.jpg
 

Attachments

  • IMG-20160714-WA0063.jpg
    IMG-20160714-WA0063.jpg
    152.7 KB · Views: 35
  • IMG-20160714-WA0058.jpg
    IMG-20160714-WA0058.jpg
    88.2 KB · Views: 34
  • IMG-20160714-WA0061.jpg
    IMG-20160714-WA0061.jpg
    118.5 KB · Views: 37
Hakika hatuja kosea kuchgua chadema, tena tunajilaumu tulichelewa wapi kuelimishwa kuwa hiki ndio chama cha maendeleo?! Hata rais ameliona hili ndio maana jana alimpongeza meya wa jiji la Dar kwa kazi nzuri ya maendeleo. Arusha sasa ni maendeleo tu majungu yamekwisha baada ya kuwafuta kabisa kijani kwenye halmashauri.
 
Haya ndio mabadiliko ambayo tulikuwa tunaimba wakati wa kampeni mwaka 2015. Inabibdi tufike wakati tujitambue sisi wananchi kwa kuchagua viongozi wenye kuleta mabadiliko na siyo kuchagua mtu kwa kuwa ametupatia kitu fulani au tu ni wa chama chako hata kama hafai.

Hongereni sana kwa mabadiliko.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
wakazi wa Arusha wamemshukuru Meya na Diwani Kessy wa Kata hiyo ya Kaloleni kwa kuwaletea maendeleo hayo pia wamewapongeza madiwani wote wa chadema katika jiji la Arusha kwa kusema wanaona maendeleo na usafi wa jiji la Arusha.

Zile tuhuma za wafanyabiashara kutoa milioni tatu rushwa ili wasiondolewe kwenye maduka ya manispaa vipi zimepatiwa ufumbuzi kwa wahusika kuachia ngazi ?
 
Mkuu mwasu hujalisoma jina la huyo jamaa vizuri nini hata akienda akoona hata elewa nini kinafanyika
Nimelisoma mkuu lakini si unajua hata hawa watu wa aina hii wana elimu yao maalum? Pale shule ya msingi uhuru kipo kitengo chao ni wenzetu tusiwatenge, inaweza wabadilisha siku moja. Teh!
 
Zile tuhuma za wafanyabiashara kutoa milioni tatu rushwa ili wasiondolewe kwenye maduka ya manispaa vipi zimepatiwa ufumbuzi kwa wahusika kuachia ngazi ?
Nafikiri hii habari nilipata kuna yule diwani wa ccm alihodhi maduka yote ya stand ndogo hapo Arusha na alikua analipa pesa kidogo sana kwenye Halmashauri ya jiji hilo kisa alikua ccm na kuna viongozi wa ccm jiji la Arusha walikua wanamlindia ulaji wake juzi ameshindwa vibaya kwenyd kesi mahakamani
 
Pongezi sana kwa viongozi wa Chadema Arusha mtakuwa mfano wa kuiga wananchi tunataka maendeleo siyo maagizo kama walivyo kwa wale wengine
 
Mpigie yule diwani wenu wa CCM atakuambia kilichomkuta. Arusha haipo tena kwenye wapiga dili tena hao wafanyabiashara wameshaondolewa wote
Zile tuhuma za wafanyabiashara kutoa milioni tatu rushwa ili wasiondolewe kwenye maduka ya manispaa vipi zimepatiwa ufumbuzi kwa wahusika kuachia ngazi ?
 
Wewe hujitambui anzisha mada yako kuhusu usafi utajibiwa huko hii inahusu miradi ya maendeleo inayofanywa viongozi wa Chadema Arusha
Arusha mmeniangusha sana yaani mmepitwa na Mbeya kwa Usafi
 
Back
Top Bottom