Chadema arusha:hatuna haja na umeya wa jiji la arusha

Chadema arusha:hatuna haja na umeya wa jiji la arusha

bato

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
3,959
Reaction score
3,476

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]SUALA la nafasi ya meya wa jiji la Arusha limechukua sura mpya, baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kudai kuwa sio ajenda yao ya sasa.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Kanda ya Kaskazini wa CHADEMA, Amani Golugwa, alipozungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa kwamba kwa sasa madiwani wa chama hicho wamejipanga kuweka mikakati madhubuti ya kupanga na kusimamia miradi ya maendeleo iliyo kwenye halmashauri hiyo kwa ushirikiano wa karibu na wananchi kwa manufaa ya taifa.
Alisema pamoja na ukweli kuwa taratibu zilizotumika kumweka Meya Gaudence Lyimo madakani hazikuwa sahihi, lakini kwa sasa kipaumbele chao ni kushughulika na maendeleo ya wananchi.
Suala la nafasi ya meya wa jiji hili, lilisababisha maafa makubwa wakati chama hicho kilipopinga kanuni zilizomweka madarakani.
Source: Tanzania daima

[TD="bgcolor: #ffffff"]

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TD]
 
ni sawa hahbri ya umea wa jiji iwekwe pembeni na badala yake madiwani walipo wambane tu meya ili mambo yaende katika jiji la Arusha na wananchi wakishaona maendeleo mwaka 2015 hatutatumia nguvu nyingi katika kutafuta ridhaa yao.
 
pamoja na yote hiyo meya wa kichina abaki kwenye makablasha kama hawawezi kumtoa..leo alikuwa amekaribishwa shule gorigotha Primary school iliyoko huko sokoni 1 kazomewa baada ya kuwaambia wazazi kuwa yeye ndiyo meya na hakuna wa kumtoa...
 
kabla ya kupata hawa madiwani sita, meya wa kichina alikuwa anakaimisha nafasi yake kuepuka vurugu kutoka chadema sasa leo tumepata madiwani sita itakuwaje nabado nguvu nyingine tunaisubiri kutoka kata ya sombetini...
 
Huyo Matata wa Arusha atapukutika mwenyewe wala hakuna haja ya kuhangaika naye , bali ni lazima atengwe na kupuuzwa , maana hana uhalali wowote .
 
Sina wasiwasi na hili kwa kuwa maamuzi yoyote hayawezi kupita bila ridhaa ya chadema kwa kuwa hupitishwa kwa kula. Pia chadema kwa wingi wao wanaweza wakajenga hoja na kuipitisha kwa kulo. Ule wimbo wa ndiooooooo sasa ndo kwanza unaanza kunoga kwa kuwa hauchezeki a town.
 
Zomea kabisa chezea wananchi weye!!

pamoja na yote hiyo meya wa kichina abaki kwenye makablasha kama hawawezi kumtoa..leo alikuwa amekaribishwa shule gorigotha Primary school iliyoko huko sokoni 1 kazomewa baada ya kuwaambia wazazi kuwa yeye ndiyo meya na hakuna wa kumtoa...
 
sasa nyie cdm wananchi wawaelewaje maana wakati wa campain mlisema mkiingia mnamng'oa meya wa kichina au mmegundua kanuni haziruhusu ndo mnakuja na maneno halafu golugwa angalia kama hujawasiliana na mbunge ndo utafukuzwa tena
 
sasa mbona madiwani mliowafukuza walisema kama golugwa kamba walichaguliwa na wananchi ili wawatumikie na siyo migomo wakafukuzwa iweje leo wanaongea yaleyale
 
sasa mbona madiwani mliowafukuza walisema kama golugwa kamba walichaguliwa na wananchi ili wawatumikie na siyo migomo wakafukuzwa iweje leo wanaongea yaleyale

Mkuu pumzika..lumumba si pamefungwa mida hii...?
 
Hayo ndio maneno, kama kweli mtasimama katika mpango huo, 2015 CCM wasijisumbue Arusha
 
Back
Top Bottom