scramble
JF-Expert Member
- Nov 29, 2012
- 1,593
- 256
Huyo itakuwa mujahidna, anawaza kijahidina na wala haelewi kama kuna tofauti ya chama cha siasa na taasisi/jumuiya na/au vyama vya kidini. Anatkiwa aelimishwe tu.
kwa hiyo chdm hakihitaji kura za waislamu? siyo vibaya chama cha siasa kusikiliza matatizo ya makundi mbalimbali ktk jamii yakiwemo makundi ya kidini. ubaya uko wapi kwa mbowe, slaa na viongozi waandamizi kumtembelea mufti na kubadilishana nae mawazo. kuwatembelea viongozi wa kanisa katoliki, anglikana, kkkt, makanisa ya kilokole, wasabato...... mimi sioni tatizo na hili. kote ulimwenguni kura na kuungwa mkono hutafutwa kwa kuonana na makundi maalumu. kuihusisha cuf na waislamu sidhani kama ni suluhisho. jambo hilo linaendelea kuwafanya waislamu wakione cuf kama chama chao. idadi ya waislamu wanayoiunga cuf itazidi kuongezeka. siasa hufanywa kwa kumvuta mtu upande wako siyo kumkimbia na kumbeza. IJULIKANE KUWA BILA KUUNGWA MKONO NA WAISLAMU, CHDM KAMWE HAKIWEZI KUINGIA IKULU. kwa wanao juwa idadi ya waislamu hapa nchini watakubaliana na mimi. huo ni ushauri wangu wa bure.