Chacha Wangwe (Rasta) yupo hai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chacha Wangwe (Rasta) yupo hai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, May 18, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Chini ya utawala wa Nguvu yaUmma,
  Nilikwishawaambia "mawe ni mepesi mkononi, ila ni mazito usoni" sasa leo hii imeanza tarime, mfano ni huu kuanzia sasa, na utaendelea kuwatokea viongozi (watawala)wote.
  Mimi ni miongoni mwa vijana tunaoitakia mema jamii yetu ya kitanzania, na kwa sababu hii sina budi kuwapongeza wananchi wa nyamongo kwa yale waliyoyafanya kwa kuwaadhibu hao wawakilishi fake.
  Huu msemo wangu "mawe mepesi mikononi ila mazito usoni", unamaana kuwa, kwa wananchi wenye uchungu, ni rahisi kuyachukua hayo mawe bila kusikia uzito wake, na yatagundulika kuwa ni mazito, pindi yatakapotua usoni mwa mlengwa.
  Natoa onyo kali kwa viongozi( watawala), wanaojitokeza kwenye mikutano ya hadhara na kutamka senteso nyepesi zenye kebehi na zinazoudhi, adhabu yao, itakuwa zaidi ya hii ya nyangw'ine.
  Pia watambue kuwa amani haipo tena tanzania, bali kuna utulivu tu, utulivu huu, ukitibuliwa hata na sisimizi, ni lazima haya ya tarime yatokee, hii ni mara ya pili katika mwezi huu wa tano, kwa tukio la aina hii kutokea, tumeona jinsi lamwai alivyoabishwa kule jimboni kwake kwa kupigwa mawe, je, hii ndio aina ya uwajibishajia wanayoitaka ccm ili wabadilike? basi na sisi wananchi tumegundua kuwa, njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwao ni hii, ya kuwachapa mawe mepesi mikononi, na yakitua usoni mwao, yanadhihirisha uzito wake.

  Na sio tu kwa nyambari, ila tukio hili litawafuata wote waliomsaidia kuingia bungeni, akina wasira, mama kabaka wale wote tunaowajua n.k, pia kwa viongozi wengine wenye kejeli, mizaha na dhihaka nao wamo kwenye orodha.

  Nashukuru Bwana mwita waitara aliyekuwa mgombea ubunge Tarime(chadema), hakuwepo kule Tarime, vinginevyo wangemsingizia kuwa yeye kawachochea na kuwatuma watu wakampe kichapo nyang'wine.
  "Chacha Wangwe (Rasta) bado anaishi mioyoni mwa wanatarime, aliowafundisha kuukataa unyanyasaji, uonevu na dhuluma. R.I.P Wangwe"- Nyakarungu-2011.
  KILA MWENYE PUMZI NA APUMUE KWA NGUVU BILA MALIPO.
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  aisee ile ya nyamongo ni noma hawa ccm watajifunza kwenda tarime kichwa kichwa
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Haya ni matunda ya kuwa na mzaha kwa mambo ya msingi kwa taifa...Ishu ya madini imepigiwa kelele sana kuwa tunanyonywa watu hawasikii...Huo ni ujumbe tosha kwa JK wenzake....
   
 4. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutaona mengi sana mpaka ifike 2015.
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kaka Nykarungu, yananyotokea tarime kwa sasa ni matunda ambayo serikali dhalimu ya chama cha ccm iliamua kutufanyia , nina mengi ya kuongea ila hasira imenipanda waliokufa pale ni ndugu zetu wakichukua chao ambao mungu aliwapa , kwanini ile dhahabu haikuwekwa hata bukoba? au kigoma hata pemba , Mungu aliwapa hiyo dhahabu pale kwa makusudi maalum, Baririck wakishirikiana na masawe wameuwa wenzetu , pia wapiga kura wetu ambao daiam hawataona jinsi tunavyochukua nchi 2015, ndugu azangu tuwaombee marehemu wa rest in peace
  walichokuwa wanapigania ni haki yao tujikumbushe single ya gadbless lema kuhusu mauaji ya arusha
   
 6. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  chacha alimalizwa na cccccc dm acha kuota
   
 7. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hivi serikali inapenda kuona watu wakiuwana kutokana na viongozi wasiopenda kuwajibika? Katika sekta zao hivi CDM ndo ilowatuma wananchi wa Mivumoni kuwashambulia wale wavamizi wa aridhi(mabaunsa)kule Tegeta mbona viongozi wabovu ndo watakaoizika tanzania yetu??????????????
   
 8. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  songa mbere mura!
   
 9. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu mmoja kwenye ccm aliwaambia wakija hao wazomeeni wambie hatutaki sasa leo yamewakuta wao wanyewe, Bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi
   
 10. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Na huu ni unabii,
  Endapo jk hataacha unafiki wa kujifanya hajui yanayotendeka kichinchini, na endapo ataendelea kuwasingizia wasaidizi wake kuwa ni wavivu, na kuwa wanamdanganya, basi atazijutia hizi dakika chache alizonazo za kujisafisha na kuwatumikia watanzania.
  Endapo serikali haitakuwa na msimamo kusimamia na kutekeleza vipaumbele vyake, na kama itaendelea kuendesha nchi eti kwa kuangalia na kufuata upepo wa siasa unavyovyuma,na ikasahau sera na vipau mbele vyake, basi ijiandae na tukio kubwa la kihisitoria litakaloikumba.

  MANENO HAYA HAYATAANGUKA CHINI
   
 11. M

  Mbwazoba Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani huyu nyamabri amelazwa wpi na huyu ndiye ugonjwa wa kuhara eegh? Au ndiye yule magahambuni........>????
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mhmm time will tell! Tarime nasikia mliwai kudai mna nchni yenu! msije mkawa ndiko mnakoelekea tena, swali kwanini mlipoteza hilo jimbo kirahisi hivyo tena kwa mtu hasiye na hata abcd.. za siasa??

  Mkisha poteza jimbo ni bora mkubali na mjifunze kutokana na makosa yenu siyo mjiandae kuunda nchni yenu! Hamwezi kunishawishi hata siku kwa tatizo la kujitakia labda mje na ushahidi kuwa mliibiwa kura lakini pia sidhani wala siamini maana mbona hawakuwaibia wakatika wa Chacha na Mara baada ya kufariki Chacha!

  Mi ni mingoni mwa watu ambao siwaelewi katika hili ingawa nyie mnaliona ni la ufahari. Bora watu wajue hii ni siasa na si vita kama hawa ndugu zetu wanavyotaka iwe vita! Naamini matumizi ya nguvu yanaweza kutumika lakini kama majibu yote yakishindikana, bado kuna jibu la sanduku la kura kuweni na Busara mtumie hiyo njia.
   
 13. M

  Mbwazoba Member

  #13
  May 19, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujaeleweka kabisaaa MURAAH!!!!!!!!!! hebu njoo tarime ufanye mkutano pale town na utoe kahotuba kako, labda watakuelewa!!!!1
   
 14. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  je umefuatilia kuhusu wizi wa kura za tarime na ukabaini haukufanyika? je unajua chochote kuhusu kesi inayoendelea kati ya nyambari na waitara? ndugu yangu fuatilia mambo kabla hujakurupuka!!!!
   
 15. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  ' mawe ni mepesi mkono lakini mazito usoni' mwisho wa kunukuu.anayebisha amuulize nyangwine maana yule wa Muleba uwenda ameshasaau uzito wake.muraaaa tz bado mmeibeba begani kwa ushujaa wenu.
   
 16. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ni kweli, nyangwine anautambua uzito wa mawe yanapotua usoni, hata ikipita miaka 100 hawezi kuusahau uzito huo.
  Na kama alivyowahi kutoa vitisho vya kuzuia mikutano ya chadema, akidai kuwa cdm haina nafasi yoyote trm eti zaid sana itachochea vurugu.
  SASA HIYO KAULI YAKE INAMRUDIA YEYE MWENYEWE.
   
 17. M

  Mbwazoba Member

  #17
  May 19, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyakarungu,


  navutiwa na hiyo misemo yako, nimependa hii ya mawe basi wewe na vijana wenzako mnatakiwa muonyeshe njia, mungu awape nguvu na uzima tuioe kesho yenu.
   
 18. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Aimen.
   
 19. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Chacha Wangwe alikuwa kiboko! Bungeni aliwahi kuita kondoms-majeneza ! Hotuba ilivunja rekodi.. Ipo kwenye hansard za Bunge!
   
 20. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wadau mie sijui lolote, mtu anaweza kuiweka ilikuwaje?
   
Loading...