Chabo murua "at angle theta"

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 


Kawaida ya mtu anayekula chabo huwa anafaidi zaidi ya mtu anayeliwa chabo.

Anaweza kuwa ni kibaka huyo anapiga hesabu zake namna ya kuwaingia hao...
 
Ila kupiga chabo ni raha sana yaani unafaidi mpaka basi
 
Ila kupiga chabo ni raha sana yaani unafaidi mpaka basi
Acha kabisa hiyo kitu unaweza uawa bure.
Nikiwa form one tukikuwa na tabia ya kuzungukia gesti zote mtaani na kupiga chabo wanaongonoka hususani siku za jumatatu.
Sasa siku moja nikaenda pekee yangu ile naona tu jamaa linamwandaa demu jamaa likazima taa kumbe lilikuwa limenistukia likazunguka dirishani likanikuta nimening'inia likatukana "wewe pimbi kwa nini unanipiga chabo?" Nilivyosikia tu sauti yake anatukana nikatoka kwa mwendokasi kama mshale nikashika barabara ambayo ndo ya kutokea hako kasenta kwa ujumla wake.
Nilikimbia nikizidi kumwacha hatua moja, tano, kumi, mwisho nikawa na uhakika wa kumwacha jamaa nikawa nimeanza kupungunza mwendo na hapo nilikuwa nimeshaanza kuingia kijiji jirani na ile senta.
Nikiwa na matumaini ya kumwacha jamaa na nikawa tu nimeanza kutembea huku nikiwaza nirudi sasa home maana nilikimbia kuelekea sehem nyingine, ghafla niliona jamaa linakuja mbio (alikuwa ni msela mwingine ila sikujua) nikatimua mbio tena. Safari hii kila nikitizama jamaa linazidi kunisogelea. Nikakimbia kama 10km jamaa lipo tu nyuma na linazidi kunisogelea.
Nilipoona nimezidiwa nilisimama na kujihami kwa kusema, "Njoo sasa si hunijui nakuua hapa" jamaa kauliza kwa uoga kwani vipi? Nikamwambia wewe si unajidai baunsa. Jamaa kasema hapana, "mimi naelekea nyumbani kijiji kile pale mbele, niliona unakimbia nikajua unaelekea huku nawe nikaamua nije kwa speed yako ili nisije tekwa pale darajani".
Baada ya kusikia maneno ya jamaa nikagundua kajamaa nilikokuwa nakapiga chabo kalinikimbiza kidogo tu kakurudi kula utamu wa demu wa kenyewe ila mimi kwa uoga nikawa nadhani kapo tu nyuma yangu hadi huyu jamaa mwingine aliponiona kama kampani kuelekea kwao.
Aisee ilinibidi nikalale kwao na huyu jamaa wa pili kwani aliniambia kurudi saivi haitawezekana utapigwa na wezi.
Chabo niliacha toka siku hiyo aiseee.
 
teh teh

Dah, mkuu umenifanya nicheke sana aisee.

Hii story yako ina mengi ya kufundisha aisee.

Ngoja nirudie kuisoma tena
 
teh teh

Dah, mkuu umenifanya nicheke sana aisee.

Hii story yako ina mengi ya kufundisha aisee.

Ngoja nirudie kuisoma tena
Mkuu nilikimbia kwa spidi ya ajabu....toka hapo sikurudia tena huo mchezo. Jamaa yule wa pili ambae nilikuwa nadhani ananikimbiza nilipomweleza alicheka sana hadi baba yake akagonga mlango ili kujua kuna nini, ikabidi jamaa amweleze tena. Mzee akaniambia " una bahati yako mwanangu yule bwana alitoka na kukimbiza, vipi angekuchoma jicho kwa spoku saivi si ungekuwa kwa Kiberiti?" Kiberiti ni dokta mtaalam wa macho kanda ya ziwa.
 
Dah, very touching.
Una ka CV katamu sana kwenye maisha yako .
ha ha ha ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…