Nikupe uzoefu wangu, mara ya kwanza nilinunua non certified android TV box, X96 Pro, kupitia ali express, nilitumia kwa muda wa mwaka mmoja kikapiga shoti,
Kwasasa natumia xiaomi mi box 4s, nikifanya comparison, non certified android tv box ilikuwa ikinipa uhuru wa kufanya modification unayotaka, kwanza kilikuja kipo rooted, unaweza uka side load any android application na ikafanya kazi sema sio kama kwenye simu, sababu hazijawa programmed kufanya kazi kwenye android TV. Nilikuwa naweza kufanya customization yoyote kama kubadirisha launcher, google chrome ilikuwa inafanya kazi vizuri GMAIL n,k
Kwa upande wa MI TV BOX niliyo nayo sasa, inaninyima uhuru kama wa non certified Android TV box, siwezi kufanya customization yoyote, siwezi ku install google chrome, natumia mozilla fire fox ambayo ipo out dated, wameondoa support kwa upande wa android TV. Nilijaribu kutafuta custom rom, bado sijafanikiwa kupata, nibebakia kutumia KODI, inayoniwezesha kufanya customization,
Pia kuna baadhi ya application kama netflix zimekuwa certified kufanya kazi kwenye hii TV box, sijajua kwa upande wa non certtified TV Box kama zinapiga mzigo.
Pia kwa upande wa casting, hii Mi tv box naona kama inasumbua, inataka ni connect kwenye same network ndio ifanye casting, kwa upande wa ile nyingine ilikuwa haina hii shida, nilikuwa naweza kufanya casting bila ku connect kwenye same network.