Celtel yamdhamini Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Celtel yamdhamini Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 4, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Ni katika harakati za kupambana na UKIMWI
  [​IMG]Na Mwandishi Wetu
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Celtel Tanzania, imetoa sh. milioni 40 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo ili ashiriki kupanda Mlima Kilimanjaro.....  Meneja Uhusiano wa Celtel Tanzania, Beatrice Mallya alisema Dar es Salaam jana kuwa Alhaj Mwinyi alikabidhiwa fedha hizo juzi mjini Moshi ikiwa ni mchango wa Celtel kumwezesha kushiriki Geita Kiliclimb Challenge kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya maradhi ya UKIMWI nchini Tanzania.

  Alisema Celtel kwa kushirikiana na kampuni ya mgodi wa madini ya dhahabu ya Geita, wamemwezesha Alhaj Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro ili kutekeleza dhamira yake ya kupambana na UKIMWI. Alhaj Mwinyi alianza kupanda mlima huo juzi (Jumamosi).

  Beatrice alisema Celtel ilianza kudhamini wapandaji Mlima Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka minne iliyopita na itaendelea kudhamini kwa vile inaamini nguvu na juhudi zinazotumika kupanda mlima huo, zinaleta matumaini ya kupambana na UKIMWI.

  "Tumefurahi zaidi kwamba mwaka huu Rais mstaafu, Alhaj Mwinyi anapanda Mlima Kilimanjaro kwa udhamini wa Celtel," alisema Beatrice na kubainisha kwamba kampuni hiyo pia mwaka huu inawakilishwa na Meneja wa Kitengo cha Fedha wa Celtel, Prisca Tembo kupanda mlima huo.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa kitita hicho cha fedha, Alhaj Mwinyi mwenye umri wa miaka 83, alisema amepata msukumo wa kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuendeleza juhudi zake katika mapambano dhidi ya UKIMWI, ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia Tanzania na kutekeleza kauli mbiu ya Serikali kwamba Tanzania inawezekana bila UKIMWI.

  "Lengo letu ni kuhakikisha jamii inaishi katika maisha salama bila kupata maambukizi ya UKIMWI kama tunavyoshauriwa na wataalamu, kuzingatia muongozo uliopo," alisema Alhaj Mwinyi.

  Alisema alijisikia furaha na kuona fahari baada ya Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Celtel Afrika Mashariki, Bw. Bashar Arafeh kumweleza dhamira ya kampuni hiyo kumdhamini ili apande Mlima Kilimanjaro.

  "Niliona ufahari! Nilikuwa na shauku ya kupanda Mlima Kilimanjaro mwaka huu, lakini ahadi kutoka kwa Bw. Bashar iliniongezea matumaini na morali ya kupanda Mlima Kilimanjaro, kwa lengo lile lile la kupambana na maambukizi ya UKIMWI kwa watu wetu na taifa letu," alisema Alhaj Mwinyi.

  Alhaj Mwinyi aliishukuru Celtel kwa kumdhamini na mchango mkubwa ambao kampuni hiyo inatoa kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali hasa elimu.

  Global Publishers - Tanzania Newspapers
   
 2. R

  Rikab Mikail Member

  #2
  Jul 4, 2009
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ya mwaka gani? Celtel nafikiri imekufa siku nyingi... je hii ni baada au kabla ya *~*?
   
 3. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  hawa naona wana agenda na huyu mzee kwa miaka hiyo 83 tusijekuambiwa sijui nini arrest!! wana uhakika ana mazoezi ya kutosha ya kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika?
   
Loading...