Kwa kuwa bunge limeisha na hakukuwa na jambo la maana nadhani ni wakati kwa viongozi wa CDM kutuunganisha ili tufanye maombolezo ya kitaifa kwa mashujaa wetu waliofariki na kuumizwa na mabomu. Tufanye hivi haraka kwa kuwa CCM imeonesha kuwatelekeza wahanga na hivyo ni sisi pekee tunaoweza kuonyesha tuko nao wakati wa dhiki na raha.