CDM mafanikio yapo mlangoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM mafanikio yapo mlangoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, May 16, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CDM mafanikio ya Oparesheni Sangara yameanza kuoneka na ushahidi ni huu hapa

  1. Mkuu wa kaya kuitisha semina elekezi haraka kuwafunda watendaji wake kukabiliana na moto mnao uanzaisha na hii inathibitisha kuwa kazi yenu imeagusa

  2. Mkuu wa kaya kuwataka maafisa habari watoe habari kwa wananchi ili upinzani ukose cha kusema

  3. Amewataka mawaziri na watendaji wakuu waende vijijini kuwafanya kazi na waache umungu mtu wanaofanya sasa hivi, sijui anataka mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, afisa tarafa, mtendaji wa kata na kijiji wafanye kazi gani?

  4. Usalama wa taifa kuthibitisha ile hoja yenu kuwa wao ni maafisa usalama wa CCM na sio taifa kwa kusambaza barua kwa masheikh mkoani ruvuma eti wananchi wasihudhurie mikutano yenu kwa kuwa ni chama cha kidini


  tofauti na haya dalili nyingine mafanikio yapo mlangni ni kuwa


  • wananchi wenyewe wanahamasika kuja kwenye mikutano pasipo kuwapelekea maloti waje katika mikutano
  • wananchi wenyewe kuhamasika kuja na mabango yao wenyewe na kueleza hisia zao
  • wanacnhi kuwaeleza matatizo yao majimboni ili hali nyinyi si watawal wa pale hii ina maana kwa wapiga kura nyinyi ndio wawakilishi wao thabiti na sio CCM waliojipa kura tena kwa hila nyingi
  • wananchi kuonyeha hali kubwa ya kukubali mabadiliko na kujutia kuchagua CC
  sasa moto mlioanzisha usiwe moto wa kifuu amabao unazimika haraka
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  Wao wako langoni, sie tusha ingia ndani
   
 3. S

  Shamwile Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo umesema kweli yaani hii operation sangara ambayo CDM wanaiendesha toka kanda ya ziwa na sasa nyanda za juu kusini ni strategy nzuri kwa maandalizi ya kuchukua dola hapo 2015, response ya wananchi inatia moyo na ni dhahiri cdm inakubalika, kwani CCM wameshindwa kutatua kero zinazo wakabili wananchi, na ndio maana kwenye mikutano ya cdm watu wanahudhuria kwa wingi na kuwaelezea makamanda kero zinazowakabili, kaza buti makamanda tupo nyuma yenu!
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CDM waendelee hivyo hivyo,non stop, province to province, region to region, disctrict to distric, division to divison, ward to ward, vilagge to village. Wakimaliza round 1 wanakuja round 2, round 3...Hivyo ifikapo 2015; jamii itakuwa tayari kukipa CDM madaraka ya kutawala nchi.
   
 5. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,075
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 280
  2015 nchi ya cdm hii. mgamba walishapoteza mvuto zzamani tu.
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  isije kuwa nguvu ya soda....
  langu jicho, can cdm survive this wave?
   
 7. O

  Omr JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni nguvu ya bangi hiyo, stimu zikishuka na wao watapoa tu. Hakuna cha CDM hapa,kelele zote hizi wakati wabunge 23. halafu mnasema tanzania tumeamka.
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  hata usipoendelea kueleza,tumeshaelewa wewd mtu wa aina gani na familia ipi. Sentensi yako ya kwanza inatueleza vizuri wewe ni nani?
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Pamoja na hii nguvu mimi nashauri CDM wajikite kwenye kupanga mikakati ya hili tatizo kubwa lwanalolalamikia la uchakachuaji wa matokeo ya kura kila mara kunapotokea uchaguzi. Ningependa wajue idadi ya wanachama, wapenzi na washabiki wa chadema waliojiandikisha kupiga kura na wanaopiga kura nchi nzima - yaani jimbo kwa jimbo; na wawahamasishe kupiga kura bila kukosa. Tutaona matokeo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
   
 10. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hata iwe nguvu ya gongO hiyo chupa ya gongo haiwekwi chini mpaka kieleweke.
   
 11. O

  Omr JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kieleweke kitu gani? Mwaka mmoja tu, CDM chali. na ngojeeni mtajua CCM ni kitu gani....mambo yanapikwa.
   
 12. N

  Nzogupata Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashauri baada ya operation warudi. Zitto, Shilinde, Lema, Mnyika, Madam wa Kawe, Mwikwabe, Dr Slaa, Mbowe na wengine hili ni kubwa na la msingi sana. Eleweni pia kuna maendeleo yanapaswa yahamasishwe majimboni mwenu. Ndio maana nasema pointi yakuelimisha umma ni kubwa na yakupongezwa sana lakini baada ya hapo badilishaneni uzoefu kuhamasisha maendeleo majimboni pia hili itajenga zaidi ya hapa mlipofikia
   
 13. O

  Omr JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanakusanya posho za safari hao.
   
 14. n

  ngurati JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  na hii nai rain shower, bado mvua yenyewe. ngoja turudi mikoa ya kati, pwani na hatimaye kaskazini. pole sana bwn nnauye
   
 15. n

  ngurati JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  na hii ni rain shower tu, bado mvua yenyewe. ngoja turudi mikoa ya kati, pwani na hatimaye kaskazini. pole sana bwn nnauye
   
 16. t

  tarita Senior Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuaijua kwa mdomo wake yenyewe imesema ni gamba, ni mafisadi, hadhi au haiba yake kwishney, ni wezi wa kura,ni watumiaji mabavu tu, ni migogoro tu,mafarakano kibao tu, wafitini, nyumba iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe, mamluki kibao,wadini( angalia cc yao, udini mtupu) waongo, wababaishaji, wazandiki wasio mstahi Baba wa Taifa, hawana mwelekeo, waoga(siku hizi hata nguo za kijani wanaogopa kuzivaa mitaani, hata wenda wazimu hawazitaki, wanazikimbia babarani) wagomvi wao kwa wao, wajinga maana wanagombana kila mahaliNape na Mkama hadharani) wameishiwa upeo wa kufikiri.
  CDM elewe sera ya ccm magamba iliyobaki mwaka 2015 ni wizi wa kura. Take counter action, hamasisheni nchi nzima kuwa kataa,sauti za watu ziungurume kama maporomoko ya maji zikiwakataa kila mahali.Kisha ungurumeni kama smba hawana ujasiri kuliko wa mubaraka,watafyata mkia.
  Mafisadi kila mwaka wengi wao hukimbia kabla ya uchaguzi. Vikaragosi vingine vitafyata mkia.
  CDM,CDM, CDM okoa Taifa hili.Tuko bega kwa bega nanyi, mi-ccm magamba wanachama wao wako nyuma yao.Vipofu wakiongozwa na vipofu kwao ni shimoni tu!!!
   
 17. baina

  baina JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachoendelea hapa nyanda za juu ni nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda, shuka kwa shuka. Hakuna kulala.
   
 18. O

  Omr JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkiondoka wanawasahau, wanasubiri mwingine awaletee t-shirt na ubwabwa.
   
 19. A

  Ame JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Arusha na Mwanza wameshaonyesha njia ya ku solve hili tatizo la wizi wa kura!
   
 20. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  nimekusoma mkuu.
   
Loading...