CDA ya Dodoma IVUNJWE.Halimashari/Manispaa inatosha

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,093
1,408
CDA ina umri wa miaka 43 hivi. Lakini ukitumia akili ya kawaida kupima mchango wake kwa miaka hiyo, utaona tija ni kidogo sana.Binfsi naona wakati ufike wa CDA kuvunjwa na mamlaka yake yote ikabidhiwe Manispaa ya Dodoma.Hii manispaa iwezeshwe, ili kuweza kutekeleza majukumu yake vizuri, hasa kitengo cha ardhi..

There is no logic kuwa na taasisi 2 sehemu moja zinazoshughulika na jambo moja.Haya ni matumizi mabaya ya pesa ya walipakodi.Na mara zote mazingira ya namna hii hushusha ufanisi ktk kuwahudumia wananchi. Muda mwingi utatumika kugombana badala ya kuwahudumia wananchi.

Dar,Arusha,Mwanza hakuna CDA.Kazi zote zinafanywa na Local Government. Naamini mambo yote yakifanywa na Manispaa ya Didoma, wananchi watapata huduma kwa ufanisi mkubwa,kwasababu Manispaa ni mali ya wananchi na inawajibika kwa wananchi.Na wananchi wana fursa ya kuiwajibisha(check and balance) wakati wa uchaguzi. Wananchi hawana mamlaka ya mojakwamoja ya kuiwajibisha CDA. CDA haiwajibiki kwa wananchi.

Uwepo wa CDA mpaka leo unapingana na DEVOLUSION policy(ugatuzi wa madaraka kwa wananchi). Kwa kuzingatia masilahi mapana ya mji wa DODOMA na nchi kwa ujumla, sioni umuhimu wa uwepo wa CDA leo. Kwa unyenyekevu mkubwa napendekeza CDA ivunjwe.Let it go for good,hata kama kuna watu wataumia.
 
Wanavunja nyumba za watu balaa, viwanja kuuzwa zaidi ya Mara moja, ukiritimba wa huduma rushwa duh. Ivunjwe tu.
 
Dodoma maeneo mengi hayapimwa, wakati CDA imekuwepo kwa miaka zaidi ya 40.Kuna Halimashari nyingi zimepima maeneo mengi zaidi ya CDA. Sasa wakati umefika Manispaa ifanye kila kitu. Wafanyakazi wa CDA wahamishiwe kwenye taasisi nyingine za umma.Na wengine washauriwe kustaafu.
 
Back
Top Bottom