Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,207
- 829,193
Wengi naamini bado mnakumbuka mada ya kinga za kiroho, haina tofauti sana na hii na haina tofauti na kinga za kimwili.... Kinga za kimwili zilizozalisha kitu kinachoitwa UKIMWI...
UKIMWI sio ugonjwa, UKIMWI sio maradhi.... Ugonjwa/magonjwa ni kiambishi cha maradhi... Tafsiri ya UKIMWI ni Upungufu wa Kinga Mwilini... Mambo ya selihai nyekundu na selihai nyeupe...
Kinga ya mwili inapopungua basi unakuwa kwenye hatari ya kuvamiwa na ugonjwa wowote ule ambao hatimaye huzaa maradhi yenye kutesa sana
Katika maisha pia tuna kinga za kiroho CD4 za kiroho.. Hizi zikiwa vizuri basi hata afya yako ya maisha itakuwa nzuri.. Utakuwa na nuru... Kila utendalo litafanikiwa.... Mabalaa kwako ni kitu cha nadra.... Mambo yako mengi yatakuwa kwenye mstari na changamoto zako zitakuwa nyepesi na zinazotatulika...!!!
Baba wee CD4 za kiroho zikishuka.... Nyota yako hugubikwa na wingu zito jeusi... Changamoto hazitakuishia, magonjwa na wewe... Wewe na magonjwa... Hakuna kitakachosimama... Hakuna utakachogusa ufanikiwe
Mambo mengi utaanza kwa mafanikio lakini hayafiki popote, usipodhulumiwa, utaibiwa.... Usipoibiwa utapoteza... Usipopoteza utaharibu.....!!!!
Kwa akili yetu ya kibinadamu kuna wajanja wachache wenye kutumia mwanya huo kuumiza wengine kwa kuwatapeli fedha na mali kwa ahadi ya kuwasaidia kusafisha nyota ama kuwarekebishia mambo yako yanyooke....
CD4 zozote ziwe za kimwili ama za kiroho zina chanzo chake, zina asili yake
. Mafarakano katika familia
. Dhuluma
. Kijicho
. Ushirikina
. Ubinafsi
. Chuki
. Roho mbaya
. Laana za ukoo
. laana za familia
. Maagano
. Viapo na mambo mengine yote yanayofanana na hayo?
Je unahisi CD4 zako za maisha zimeshuka? Jichunguze tatizo limeanzia wapi