CCM Zanzibar yarudisha mfumo wa chama kimoja

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Wahafidhina wamefanikiwa kuongoza nchi kwa mkono wa chuma kijeshi ,sasa Shein apewe status gani ?Jeneral au Dictetor?
Written by makame silima // 23/03/2016 // Habari // Maoni 3


IMG-20160323-WA0028.jpg




Wanaposema wahafizina tuko tayari kufa njaa?

Jee wamewakusudia nani wakufa njaa? Sizani kuwa makeke haya na majikazo na majivuno haya ni kwa wao kufa njaa no.

Nazani wamekusudia wananchi wakawaida ambao walikataa na wanaendelea kuikataa ccm na vitimbi vyake vya Kutawala kimabavu na kibaguzi.

Hii kauli ni kama kuwajejea wananchi kua kwavile mumeikataa ccm kwahio kufeni na sisi tutaindelea kuwanyonya ili tupate kuishi kwa hicho hicho tutakacho wakamua kutuka kwenu.

Hakuna shaka kua Shein atakuwa na wakati mgumu katika utawala wake wakulazimisha ,kwani itakuwa ni itakuwa ni utawala wakimabavu nguvu , kibaguzi kutokana na itikadi za kivyama na utakao shindwa kuheshu sheria na haki za kibimadamu.

Yote hayo yameshaanza kujitokeza siku tatu tu tulizoelekea kwenye uchaguzi tumeshuhudia vitimbi vingi.

Uvamizi wa kijeshi watu kuteswa kubaguliwa kulazimishwa kupiga kura kwa vitisho na utekaji nyara na kuwaingilia kinguvu wananchi.

Serekali ukiona inatumia hali hio kwa raia wake? Basi ujuwe imepoteza STATUS yakua Serekali .

Inabakia kuwa gange la kihuni kuwaonea raia wasio na hatia na kuweza kujitetea .

Kwa hali hio ndivyo itakavyokua Serekali ya Dr Ali Mohammed Shein na Gainge lake.

Serekali ya Shein itakuwa ya mkono wa chuma kwavile imepoteza imani kwa wananchi na hivi sasa haina budi kulazimisha mambo.kinguvu nguvu na kukanya haki za binadamu.

Tusahau kua tulipata unafuu wa serekali ya umaja wa kitaifa SUKau GNU hii total imeshakufa na imeuliwa maksudi na wahafidhina ili kukizi kiu yao .

Sasa Serekali itakayokuweko kwa mujibu wa uchaguzi au uchafuzi wa Jecha Salim Jecha ni Serekali ya chama kimoja na itikadi moja .

Kwa hio watakao ingizwa na kuchaguliwa humo ni kada mawaziri wa ccm na mawakala wao.

Na katika uwajiri wa kazi utakuwa ni wa upendeleo kivyama na hilo limesha jitokeza katika upigaji kura wa juzi wajiriwa wa serekali walifosiwa kwa vitisho kufika hadi kuambiwa ama kazi au wapotelee mbali.

Hawakuwa na uhuru wao wa kuchagua mamuzi wanayo yataka ,wengine waliambiwa eti wende tu kwenye vituo ili kioo cha dunia kione watu wamejitokeza lakini kilichoko nyuma ya pazia ni chengine.

Nazani ulimwengu umeshuhudia mara hii kilichoko nyuma ya pazia maana Maaalim Seif aliwafunulia kuona.

Ulimwengu ulichazoweleshwa kua Zanzibar imejigawa makundi mawili kutokana na historia yake ya nyuma ya vyama.

Ulimwengu ulizowea kudanganywa kua matatizo ya Zanzibar ni U-Arabu na U-Afrika wakulinda mapinduzi.

Hii ilikua ndio kasumba kubwa walio kua wakiisimamia na kua ngao yao wahafishina ambao hawakubaliki kwa wananchi walio wengi wa Zanzibar wenye kutaka mabadiliko na kupuza kasumba hizo zilizopitwa na wakati.

Kwa hio ulimwengu umewashtukizia na umeshtukizia Tanzania kwa kipindi cha nusu karne imekua ikitumia kivuli hicho ili kufunika maovu yao.

Ndio kusema kwa hali viongozi wa Ccm hawako mbali sana na THE HAGUE hivi sasa jinsi watakavyo iongoza Zanzibar kimabavu na kumlazimisha Punda kunywa maji.

Hee Mungu ibariki Zanzibar na watu wake na uwalinde wale viongozi wetu wenye uzalendo na wanao simamia haki ya Wzanzibar .
 
Back
Top Bottom