Joshi Kanji
Member
- Mar 1, 2008
- 75
- 43
Labda Mbowe alichanganya majina. Hivi Mzee Karume (RIP) alikuwa wa darasa la ngapi? Mbona naye alikuwa kiongozi mzuri tu aliyetuletea Muungano na kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo yaliyolenga watu kwa kuwajengea nyumba za kisasa? Wakati mwingine hicho kigezo cha elimu wala si hoja kwa sababu jitu linaweza kuwa na MaPhd kibao lakini lisiwe na busara wala uwezo wa kuongoza!
ni sawa mtu ambaye ni mtundu na mjuaji hata kama hajasoma anaweza kutuongoza....lakini ukweli wengi wa aina hii walikua ni makandamizi wengine hua goigoi hawajui chochote cha ulimwengu wa kisasa...zamani sawa lakini sio karne ya 21..huyu tuna mashaka naye....makamu bomu....labda mbowe alichanganya majina. Hivi mzee karume (rip) alikuwa wa darasa la ngapi? Mbona naye alikuwa kiongozi mzuri tu aliyetuletea muungano na kuwaletea wananchi wa zanzibar maendeleo yaliyolenga watu kwa kuwajengea nyumba za kisasa? Wakati mwingine hicho kigezo cha elimu wala si hoja kwa sababu jitu linaweza kuwa na maphd kibao lakini lisiwe na busara wala uwezo wa kuongoza!
Zarau kama hizo kwa wa Zenj ndio maana wanaanza kurudisha mipaka ya nchi yake:shocked:
Kumlinganisha mgombea wetu na waasisi kama Mhe Karume waliotawala miaka ya 60 ni kurudisha nyuma hali halisi na kupotosha ukweli. Hata kama Karume alitawala akiwa na elimu ya darasa la saba, hali ya miaka ya sitini ni tofauti sana na sasa. Wakati ule wasomi walikuwa wachache sana na pia kiwango cha elimu alichofikia kilikuwa juu sana ukilinganisha na std 7 ya sasa. Haiingii akilini chama makini kama CHADEMA kumsimamisha std 7 karne hii kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz. Hiki ni kichekesho kwa jamii. CCM mgombea wao wa std 7 ni mmoja tu tena mgombea ubunge.
Ni kweli Mzee Idrisa Abdulwakil (RIP) elimu yake ilikuwa ni STD VII