Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Jitihada za makusudi zinafanywa na CCM Bara la kulifufua Azimio la Arusha na kuliingiza Zanzibar kinyemela kupitia mgongo wa CCM. Azimio la Arusha ni jinamizi la TANU ambalo lilipigwa marufuku na Rais wa ASP na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye mkutano wa hadhara, na kutamka bayana kuwa "Azimio la Arusha mwisho Chumbe". Chumbe ni kisiwa kimoja kidogo kabla hujaingia mjini Zanzibar kutoka Tanganyika.
Hayati Karume hakukurupuka tu na kulipiga marufuku lakini alichukua muda kuangalia utekelezaji na maudhui yake, ndipo alipoliona halifai na lina kwenda kinyume na desturi,maadili,ustaarabu na Imani ya wa zanzibari walio wengi. Aliwakumbusha wazanzibari jinsi dini yao inavyowahimiza kuwa na KHATIMA...KHATIMA...KHATIMA.
Toleo rasmi la serikali na chama cha ASP baada ya kifo cha Karume linsema " Rais Karume ameuwawa, kilichokufa ni kiwilikiwili chake tu; Mawazo, fikira, hekima, busara ...... vitabaki pale pale....vitaenziwa milele...."
Wakati marais wote walopita Zanzibar waliendeleza msimamo wa kutolitambua Azimio hilo kwa kuendelea kuzienzi fikira za Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hayati Karume itakuwa si busara leo CCM Zanzibar wakakubali kirahisi kutia ulimi puani.
Inaeleweka kuwa CCM Bara wanajaribu kupenyeza na kuhinikiza kila watakacho kwa kutumia udhaifu wa CCM Zanzibar wakati huu chama hicho kinapoendelea kupoteza mvuto na umaarufu kutoka jamii ya wazanzibari wazalendo.
Mhe. Polepole wewe ni msomi na muelewa, kwa hili liwachie Zanzibar wapumue. Waachie wazienzi fikira za kiongozi, baba wa Taifa la Zanzibar,Hayati Abeid AMANI Karume.