Ccm your always reactive and not proactive-aibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm your always reactive and not proactive-aibu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KOMBAJR, Apr 17, 2012.

 1. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanabodi Imekuwa ni kawaida kwa CCM kupitia Viongozi na Makada wake kutoa kauli mbali mbali pindi panapotokea matukio ya kukimbiwa na wanachama wake.

  Lakini kauli hizi wakati mwingine CCM bila kujua Zinawaacha Uchi na kuonyesha wananchi ni jinsi gani wasivyo na uwezo wa kusimamia yale wanayo yasema au kuyahubiri kila siku, hayaitaji mtu kuwa na PHD kuyatambua au kuyaona.

  Agenda ya Kujivua GAMBA...... Ilikuwa ndiyo wimbo ambao kila kada na viongozi wa CCM alikuwa anauimba na wakaenda mbali mpaka wakawataja hao ambao wao walidhani kuwa ndiyo ambao ngozi zao zimegeuka kuwa magamba na inapaswa kuvuliwa swali likaja JE wahusika watajivua wenyewe au chama kitawavua hayo magamba? washahili wanasema ni "bora ukasafisha kidonda chako kabla nesi ajaja coz yeye hatakuwa na huruma kwako"
  Mwimbo huo wa kujivua Gamba umeshapoteza mvuto masikio mwa wananchi kama CCM walifikiri hiyo Singo ingebeba albamu imekuwa kinyume chake.

  CCM haina MENO wa Uthubutu! kama mmeshagundua kuwa wanachama hawa wamekwenda kinyume cha taratibu zenu kwanini musiwafukuze ili muonyeshe kweli kuwa hamfungamani na hizo tabia zao mbaya?Kuna kitu kinaonekana hapa kuwa CCM wanawaogopa wanachama ambao wameonekana kama wamekuwa maarufu kuliko chama.

  Rostam alipostep down mlizungumza mengi na yeye alieza mchezo mchafu Gulter Politics, Jana Millya amejiondoa mmeongea sana na yeye amesema yake. Swali Je hayo mnayosema leo mlikuwa wapi kuyasema na kuyachukulia hatua mapema?Nani Muongo sasa wanachama waliojitoa au nyinyie mlikondani ya chama?

  Hivi hamuoni aibu pale mtu anapojitoa Kwenye chama chenu halafu mnakwenda kwenye media nakuanza kusema potiohh1bora ametoka alikuwa mzigo kwa chama! to whose expenses?Mlichukua hatua gani kama alikuwa mzigo kwani chama chenu ni ghala na kutunzia mizigo?

  kwa hali hii dhana ya uwajibikaji haipo kama mnashindwa kuwajibisha wanachama wenu wakiwa ndani ya chama mpaka watoke ndiyo muanze kuongea kwakifupi mnajidhalilisha hata kwa watoto wadogo.

  Kwanini Msiwe na Courage ya kumface mwanachama akaambiwa maneno haya ambayo unayasema baada ya kujiondoa coz mnachofanya ni "Post mortame"

  Mytake: Kauli ambazo zimeshatolewa na zinazoendelea kutolewa kuhusu Ole Millya ni vizuri mkajipima wenyewe kabla hajasema.

  Naomba kuwasilisha!Nakaribisha nyongeza na majibu kwa maswali husika!
   
Loading...