CCM yazoa viti vingi vya udiwani

Kuna tatizo la ushabiki ambao unakupelekea kukudhalilisha tu.Haina maana kuharibu image yako kwa mambo ambayo huwezi kuyatetea mbele ya waungwana.Kwanini katika taarifa yake wameshindwa hata kukopi hapa JF matokeo ya Ifakara na Bashnet au Sengerema?
 
Tulimshauri "KAMANDA" wa mabua Nasary, asikimbie JKT hakutusikia, sasa ameona madhara yake KAKOFI kamoja tu damu kibaao puani hadi kulazwa........ huu sasa ndo ukamanda legelege....

Anyway taarifa njema ni kuwa ADC imeanza kupata umaarufu kupitia matokea yaliyotolewa jana,

mkuu huwezi kuwa mtanzania!?
 
Pin ya bomu na maganda ya risasi yaliyookotwa katika uwanja wa soweto Arusha na wanajeshi yamegundulika kuwa ni toleo la kisasa mno na pia ni bidhaa za kiwanda cha China na zimezalishwa mwaka huu ktk kiwanda husika.
Bidhaa hizi zimekutwa zote zimetengenezwa katika kiwanda kimoja na ni bidhaa zilizowekwa serial numbers za mwaka huu na zinafuatana kwa kupishana degits chache sana, jambo ambalo linadhihirisha kuwa mtupaji/watupaji wa bomu na mpigaji/wapigaji wa risasi za moto ni kundi moja au ni mtu moja.

Mwanajeshi mmoja aliyekuwepo kwenye operation husika ametonya kuwa uchunguzi huu ulifanyika kwa maamuzi yao binafsi baada ya kushangazwa na aina ya Pin inayodhaniwa kuwa imesalia baada ya bomu husika kulipuka kuonekana kuwa ni unique sana tofauti na aina za mabomu waliyoyazoea na wanayoyamiliki kama jeshi. Wamegundua mabaki ya silaha hizi ni bidhaa mpya ambazo bado hazijawahi kutumika katika majeshi ya TZ(hasa bomu husika).

Waliamua kukagua maganda ya risasi za moto na pin husika na kuchukua serial numbers wakaingia kwenye search engines na ndipo wakagundua kuwa bidhaa hizo ni za mwaka huu na zimezalishwa ktk kiwanda kimoja cha serikali ya China.

CCM walikua na Ziara China Mwaka huu,na walitembelea viwanda mbalimbali.
 
:llama:Taarifa zilizopo mpaka saa sita usiku wa kuamukia leo ni kama ifuatavyo:

  1. Chadema wameshinda katika kata zifuatazo;

  • Nyamulukano
  • Lugata
  • Iyela
  • Bashnet
  • Dongobeshi
  • Iseke
  • Ifakara

  1. CCM wameshinda katika kata zifuatazo

  • Genge
  • Minepa
  • Makuyuni
  • Dalai
  • Mbalamaziwa
  • Mianzini
  • Tingeni
  • Stesheni-Mtwara
  • Ibugugile

 
Iwapo tutafanya siasa za kidemokrasia, mtazamo huu wa siasa za sasa hutauona na utakushangaza, ccm inatumia mbinu chafu za ujambazi,kuuwa,kuiba kura,kutishia...hii ina maana haijiamini,matokeo yake pande pinzani nazo zikiamua kubalance mambo hatutakuwa na amani nchi hii
 
Matokeo Jimbo la Chambani:

CUF: 2,751
CCM: 399
ADC: 112
CHADEMA: 12
Zimeharibika: 16

Hivi haya majina ya vitongoji ya huko Zanziba na pemba ni ya kiswahili au ya lugha zao za asili?. Majina kama Chambani, mchamba wima, kibanda maiti huwa yananiacha hoi.
 
CCM haiwezi kujivunia ushindi inaoupata kigaidi baada ya kupiga, kuteka na kumwaga damu za raia
 
Huyu mwandishi mnazi wa kutipa hivi CDM inanyakua kata mbili tu? Mbona kuna Ifakara, Sengerema Sindiga hajazisema??? Huu ndiyo ukanjanja.

Mnazi kupita maelezo kauli nzuri hapo ilikuwa ccm yajaribu kutetea viti au yapoteza viti baadhi ya viti vyake
 
CCM haishindi popote pale ila ni dhuluma tu. Eti CCM yajizolea ingekuwa hivyo ingehangaika kwenda kuwauwa watu ili mradi tu itawale? Wewe mleta mada mshabiki wa chama cha mfu.
 
Hii habari ilitakiwa kuandikwa na Uhuru mwananchi....maana umesema viti vigi, halafu hujavisema!

Chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika sehemu mbalimbali ziligubikwa na vurugu wakati hali ilikuwa mbaya zaidi huko Makuyuni mkoani Arusha ambako Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipigwa na wafuasia wa CCM na kulazimika kulazwa hospitalini.
Pamoja na vurugu hizo, CCM iliendelea kudhihirisha umwamba wake katika ulingo wa siasa baada ya kujizolea viti vingi vya udiwani wakati wa chaguzi ndogo zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini.
Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa walikuwa wanafuatilia kwa kina chaguzi hizo ili kupima joto la kisiasa nchini.
Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Makuyuni wilayani Monduli ambako Mbunge wake ni mwanasiasa maarufu Edward Lowassa.
CCM iliibuka kidedea huko Makuyuni na kufanya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Lowassa ana misuli ya kuifanya CCM ishinde huko Monduli.
Lowassa alikuwa na kibarua cha kukabiliana na Chadema waliokuwa wanataka kujipenyeza Monduli ambako hawajahi kuwa na kata tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
Hata hivyo, bado CCM haijapata dawa ya ushindi Pemba kwani kilishindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi wa ubunge wa Chambani.
Chadema kwa upande wake kilitoa changamoto kwa CCM katika chaguzi hizo za kata na hata kujizolea kata mbili za Iyela huko Mbeya na wilayani Hanan’g huko mkoani Manyara.
Nassari apata kichapo Makuyuni
Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM, akiwa katika harakati za uratibu wa shughuli za upigaji kura za udiwani katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.
Nassari aliyekuwa wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliomshambulia kwa fimbo na
Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura.
Source:mwananchi 17 juni 2013
 
hivi pamoja na tulipofikia kumbe kunawatu bado wanaipigania ccm kiasi hicho kweli!? Naanza kupata wasiwasi na 2015

Transporter, wanaopigania ccm wamebaki wachache. Ni wale wenye maslahi ndani ccm especially wafanyakazi serikalini, wafanyakazi ndani ccm, wajumbe wa nyumba kumi na possibly members wa familia zao. Lakini kwa kuangalia mwelekio wa kisiasa katika nchi, Idadi yao inakadiriwa itakuwa <50% ya wapiga kura ifikapo 2015. Hii ni kutokana na kukua kwa uelewa wa mambo miongoni mwa watanzania na wapiga kura
 
:llama:Taarifa zilizopo mpaka saa sita usiku wa kuamukia leo ni kama ifuatavyo:

  1. Chadema wameshinda katika kata zifuatazo;

  • Nyamulukano
  • Lugata
  • Iyela
  • Bashnet
  • Dongobeshi
  • Iseke
  • Ifakara

  1. CCM wameshinda katika kata zifuatazo

  • Genge
  • Minepa
  • Makuyuni
  • Dalai
  • Mbalamaziwa
  • Mianzini
  • Tingeni
  • Stesheni-Mtwara
  • Ibugugile

Asante kwa taarifa yako mkuu! Ungeongeza na CUF (Chambani)
Napata shida na uandishi wa gazeti la Mwananchi: Hivi huko ndiko kuzoa viti vingi? Kati ya viti 17 kwa orodha yako mkuu - CCM 9; CHADEMA 7 na CUF 1. Hapo hatujazungumzia viti 4 vya arusha ambako uchaguzi umeahirishwa.
 
Mungu Ibariki Tanzania tusifkie huko tuendako
Z

 
mbona mnatuletea majungu badala ya taarifa za uchaguzi?
Kama kuna mtu ana taarifa alete tujue what is going on badala ya kubishana.
 
Tulimshauri "KAMANDA" wa mabua Nasary, asikimbie JKT hakutusikia, sasa ameona madhara yake KAKOFI kamoja tu damu kibaao puani hadi kulazwa........ huu sasa ndo ukamanda legelege....

Anyway taarifa njema ni kuwa ADC imeanza kupata umaarufu kupitia matokea yaliyotolewa jana,

Watu 30 wenye fimbo hata ungekuwa meja jenerali huwawezi. Wakati mwingine uwe na utu upumbavu wako usikubali ukuzidi.
 
baada ya kuua na kujeruhi zaidi mia nne ndani ya kata 26, vipi uchaguzi mkuu mwaka 2015..

Nadhani uchaguzi wa 2015 wapiga kura wote watauwawa na kutakuwa hakuna wapiga kura na ushindi utapatikana bila kura na mawe,mito,wanyama,barabara,majumba ndivyo vitakavyo tawaliwa.
 
asante kwa taarifa yako mkuu! Ungeongeza na cuf (chambani)
napata shida na uandishi wa gazeti la mwananchi: Hivi huko ndiko kuzoa viti vingi? Kati ya viti 17 kwa orodha yako mkuu - ccm 9; chadema 7 na cuf 1. Hapo hatujazungumzia viti 4 vya arusha ambako uchaguzi umeahirishwa.

pia
analysis nzuri ingetuambia viti vingapi vilikuwa vimeachwa na chama gani na kwa sasa ni chama kipi kimechukua/poteza. Wengi hawajui kuwa hata ingekuwa kupoteza kiti kimoja, endapo ccm ilikuwa na viti vyote 26 ikapoteza 1, haiwezi kusema imepata ushindi wa tsunami.
 
Back
Top Bottom