CCM yazidi kutabiriwa kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yazidi kutabiriwa kifo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Apr 7, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 07 April 2012 08:14 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Leon Bahati na Frederick Katulanda, Mwanza
  MAKADA wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wamewahi kushika nafasi nyeti ndani ya chama hicho wamesema kuwa mfumo wa uendeshaji wa chama hicho, unajenga makundi ambayo sasa yanakitafuna na hatua za haraka zisipochukuliwa, kifo chake kinakaribia.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, makada hao ambao ni wabunge wa zamani; Lepill Ole Molloimet (Monduli) na Dk Raphael Chegeni (Busega), wamesema kuwa umefika wakati kwa CCM kufanya mabadiliko ya dhati, vinginevyo baada ya 2015 kitageuka kuwa chama cha upinzani.

  Kauli za makada hao zimekuja siku chache baada ya makada wengine wa chama hicho Dk Hassy Kitine, Joseph Butiku na Dk Ibrahim Kaduma pia kukitabiria kifo chama hicho kisipobadilika.

  Molloimet na Dk Chegeni walisema hayo walipokuwa wakitoa tathmini yao kuhusu uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo mgombea wa CCM, Sioi Sumari alishindwa kukitetea kiti hicho kilichoachwa wazi baada ya kifo cha baba yake na kunyakuliwa na Jushua Nassari wa Chadema.

  Molloimet alielezea kuwa mpasuko uliopo ndani ya chama hicho kwa muda mrefu imeigawanya CCM kwenye makundi mawili yanayokinzana kuhusu ufisadi.

  Alidai kuwa makundi hayo yaliingia kwenye uchaguzi wa Arumeru Mashariki yakiwa yanasigana tangu mchakato wa kura za maoni na hadi uchaguzi ulipoanza.

  Molloimet ambaye aliwahi kuwa mkuu katika wilaya sita nchini alitoa lawama nyingi akisema makundi hayo yanatokana na watu wenye fedha kuonekana kuwa na nguvu zaidi ndani ya chama.

  "Hali hiyo imekifanya chama sasa kuonekana siyo cha wanachama tena, ni cha matajiri wa CCm kwa maslahi yao," alilalamika Molloimet akiongeza kuwa kwa sasa maslahi ya CCM siyo kwa wanachama tena bali kimegeuzwa kuwa mali ya matajiri, wanaoonekana kukiweka mifukoni mwao.

  Bila kutaka kutaja majina, Molloimet alidai kuwa chama hicho kilifanya makosa tangu kundi hilo la wana CCM kufanikiwa kujijengea nguvu ndani ya chama na serikali.

  Kwa upande wake Dk Chegeni alisema kuwa CCM itaendelea kuanguka katika chaguzi mbalimbali kama ilivyotokea Arumeru Mashariki iwapo mfumo wake wa uchaguzi hautabadilika pamoja na kuacha kutumia matusi katika kampeni badala yake kueleza sera.

  “Hapa hakuna wa kumlaumu bali tujilaumu wenyewe CCM. Mfumo wetu wa kura za maoni unazalisha makundi, hii ukiangalia majimbo yote ambayo tulishindwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 kama vile Ukerewe, Mbeya na hata Iringa, kote kulitokana na makundi ambayo yamezalishwa ndani ya kura za maoni,” alisema Chegeni.

  Alisema kuwa kwa sasa CCM ni kama wamepokonywa dola kwa vile wapinzani wameanza kukamata majimbo muhimu ambayo ni kama ngome kuu za CCM.

  Alibainisha kwamba hiyo ni ishara ya wazi kwamba chama tawala kinatakiwa kujitathmini na kujisahihisha makosa yake, pamoja na kuweka mfumo mpya wa namna ya kumpata mgombea kupitia kura za uwiano ambazo hutumika zaidi katika nchi ya Rwanda na Afrika Kusini.

  Alisema kuwa CCM inapaswa kuangalia mfumo wa kura za maoni na ikiwezekana kutafuta mfumo mpya kama ule wa kura za wawakilishi au kura za uwiano sambamba na kuwaondoa watu wote wasio waaminifu katika chama kwa vile pia wanakigharimu sana chama.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. E

  Elliot Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  my take kifo nitayari ni mazishi tuu yaliyobaki.....hamna jambo geni kwani siku zote wamekuwa wakishauriwa kuhusu mambo ya msingi yanayolilenga taifa hili kwa sasa yakiwemo uchumi, ajira, ugumu wa maisha nk lakini wanaona ni kama ngojera na watanzania waleo si wa miaka 5 au 10 uliyopita...hawasomi alama za nyakati...wananchi wamechoshwa kabisa na wakae wakijua watabaki kama historia tuu kwa wananchi wa Tanzania....
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  chegeni analalama baada ya kupigwa chini kwenye kura za maoni hana jipya huyu
   
 4. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mawazo haya ndiyo yanayoiua ccm! Endeleeni kuamini hivyo ili Tukizike chama hicho!!
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Na hawa kina Ole Molloimet, Butiku, Dk.Kitine na Dk.Kaduma wanalalama sababu ya mini? Inadhihirisha ni jinsi gani tusivyoweza kujitathmini kwa haraka. Maranyingi tunatafuta sababu za kufuta ukweli ulio wazi.
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Utaratibu wa mazishi unaendelea;

  Ndugu na jamaa watajulishwa.
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  vita ya panzi furaha kwa kunguru
   
 8. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Teethless dogs. Wanalalama tuu wakati they have nothing to do to rescue the situation na pia wanaogopa kuhamia chadema
   
Loading...