CCM yazidi kugawanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yazidi kugawanyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Facts1, Jan 3, 2010.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  CCM yazidi kugawanyika

  Na George Marato
  3rd January 2010
  Mgawanyiko mkubwa umekikumba chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Musoma mjini kufuatia viongozi kadhaa kusimamishwa nyadhifa zao kwa kutuhumiwa kupokea wanachama wanaoonyesha nia ya kugombea ubunge jimbo la Musoma mjini.
  Viongozi waliosimamishwa ni pamoja na mwenyekiti wa kata, Mwigobero Mussa Kerenge, katibu wa CCM Kata ya Nyamatare, Rashid Mohamed na katibu wa CCM kata ya Iringo, Alex Maiga ambao tayari wamekabidhiwa barua za kusimamishwa uongozi.
  Kwa mujibu wa barua hizo ambazo zimeandikwa na katibu wa CCM wilaya ya Musoma mjini, Haula Kachwamba na nakala zake kupelekwa kwa mbunge wa Musoma mjini Vedastus Mathayo na katibu wa CCM mkoa wa Mara zimewasimamisha viongozi hao na kutakiwa kukabidhi vitu vyote vya ofisi mara moja.
  Kwa mujibu wa barua hizo za Desemba 18 mwaka jana zimesema viongozi hao wamekiuka utaratibu wa chama kwa kuanza kafanyia wana-CCM wengine kampeni kabla ya muda rasmi kutangazwa na chama hicho.
  Hata hivyo, viongozi hao wakizungumza na Nipashe mjini Musoma walisema hatua hiyo imefanywa kwa fitina na uongozi wa chama kwa shinikizo la mbunge huyo wa Musoma mjini kwa kutumia uwezo wake wa fedha.
  Walisema hawakukiuka maadili ya chama kama ilivyodaiwa kwa vile walipokea kila mwana CCM ambaye anaonyesha nia ya kugombea ubunge jimboni humo na kumsikiliza kama ilivyotangazwa na chama makao makuu na si kampeni.
  Walisema kitendo hicho cha fitina kilichofanywa na uongozi wa CCM kwa manufaa ya mtu mmoja kinakipeleka chama katika shimo ambalo ni hatari kwa siku za usoni hasa katika uchaguzi mkuu ujao.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...