CCM yawasimamisha mawakala wake Lindi, Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawasimamisha mawakala wake Lindi, Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 31, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huko Lindi CCM imewasimamisha viongozi 50 wa ngazi mbalimbali kwa tuhuma za kuhujumu chama.

  Huko Arusha nimeletewa habari za kuamninika na mmoja wa walioko kwenye kampeni za mgombea ubunge kuwa CCM waliwaita mawakala wao wanaokadiriwa kufikia 300 na kuwakusanya katika ukumbi.

  Baada ya wote kuingia ukumbini milango ikafungwa na kisha wakaanza kusema kuwa ndani yao kuna mamluki/ mapandikizi toka upinzani.

  Hivyo wakawaleta Polisi kama wanane kisha wakakubaliana waite jina moja moja.

  Kwa sababu ya wingi wa watu na udogo wa ukumbi na muda wa kuita majina kuwa mrefu watu wakaanza kukosa hewa na kuwa katika hali mbaya.

  Ikaamuriwa milango ifunguliwe na sasa zoezi lifanyike kwa wao kutoka nje na majina yakiitwa warudi ndani.

  Vurugu ilitokea baada ya baadhi ya mawakala kukasirikia kitendo hicho na kutoa lugha kali kisha kiasi kinachokaribiwa robo ya mawakala hao wakaondoka kwa hasira.

  Ilibidi uongozi wa CCM utafute mbinu za kutafuta mawakala wengine wa kujazia pengo.

  Kwa kuwa walikuwa wamekwisha kuapishwa , upinzani ukapewa habari za kutaka kuongezwa mawakala wapya wakalalamika na hivyo CCM hawakuweza kuongeza mawakala.

  Habari za uhakika zinasema hata kuhonga au kuiba kura inakuwa vigumu wakati huu kwa kuwa sehemu kubwa ya wasimamizi wa uchaguzi ni watu walioamua kuunga mkono jitihada za mabadiliko. CCM hawana uhakika na mawakala wao wanaogopa kuna mapandikizi. Hawana hakika na viongozi wao, waogopa baadhi wana urafiki na walioshindwa kura za maoni. Kuna wasimamizi wanaosubiri kuona wataambiwa nini ili wachukue hatua sahihi za kufichua na kutoa taarifa.

  Kuna mawakala nchi nzima wanaosubiri kwa hamu kuona pesa zikitolewa kuhonga ili wanaotoa wakione cha moto. HALI SIO SALAMA CCM.

  Hawana uhakika na wasimamizi wanaogopa kuwa kuna wenye misimamo ya haki.

  Mwisho katika hali ya kushangaza Mchungaji mmoja ambaye ni mbunge wa kuteuliwa wa CCM aliamua kugawa kanga za CCM katika moja ya mikesha ya kanisani kwake bila kuwaambia waumini wake neno lolote.
  Mkesha ulipoisha walikuta kanga hizo zikiwa zimeraruliwa hapo nje.

  HALI YA NCHI IMEBADILIKA. WATU WAMEIVA NA KUKOMAA.

  Nyie mnaoogopa kuibiwa kwa kura ondoeni wasiwasi.

  Njia pekee inayowezekana kuibiwa kwa kura ni kuanzishwa kwa vurugu ili utokee mwanya wa kupenyeza masanduku.

  Epuka vurugu hata ukipigwa usirudishe. Kaeni mbali sana na Vituo vya kupiga kura.

  Waelewesheni watu wote kuwa wasikae karibu na kituo. Wala ikitokea vurugu wasikubalia kuingilia.

  Hali ni mbaya kupita maelezo CCM. Nimeongea na observer mmoja na akanieleza kuwa kulingana na tathmini yao ya haraka hakuna namna CCM katika hali ya kawaida kushinda uchaguzi huu kutokana na mwenendo mzima wa kampeni na mwamko mkubwa wa watu kupiga kura.
   
 2. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mambo ni ya Hofu kubwa kwao. Endeleeni kuhubiri suala la utulivu kwani Vurugu ndiyo njia pekee ya kuweza kuiba kura. Hakuna tumaini jingine kwao. ULIWAONA USONI WAKATI KIKWETE AKIHUTUBIA. Wamejulishwa ukweli.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Imekaa njema.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  CCM bye bye
   
 5. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CCM wanajua hali yao ni mbaya ndio maana wakamwibua Mkapa jana na isiwe kabla.
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Hali mbaya kwa vyama sababu wanalipa hela ndogo, na baadhi ya vituo havina mawakala
   
 7. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #7
  Oct 31, 2010
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kavirondo ameripoti kupitia Channel Ten kuwa uko Nyamagana kuna wasimizi wa vituo wawili wamechukuliwa na polisi baada ya kuonekan kuwapo kwa vituo hewa.
  nafikiri wanajamii tungejigawa kwani Channel Ten wanafanya live coverage, TBC1, ITV na Capital pia. Na mara zote wanakwenda live na maripota mikoani.
   
 8. K

  King kingo JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu endelea tu kutuhabarisha maana huku kwetu Tanesco wameshafanya mambo yao na wengine tuna zamu ya kuangalia vituo vyetu..
   
 9. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  siku zote vibaka hutegemea vurugu ili kuiba inabidi watu tujitenge na vurugu ili mambo yaende vizuri.
   
 10. c

  chanai JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks for this. Inatia moyo kuona jinsi gani watanzania walivyokuwa na kiu ya mabadiliko
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mungu saidia, tuingie kwenye mageuzi bila fujo..!
  Lakini ushindi ni wetu...napata hisia hizo mud wote!
   
 12. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2010
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Duhi! Hii imetulia kama nini natumai Nyerere anatabasamu anapo haya yakitokea ndani ya nchi yake. Umpumzike kwa amani mpiganaji, tunamshukuru Mungu ametuinulia mwingine; ndani ya lichama kuna mazonge tupu; siku hizi ni baba, mama na wana; tehe tehe eee eeeeeee
   
Loading...