CCM yavuna wanachama wa CHADEMA 380 Tunduma kwenye maadhimisho ya Miaka 40

enockino

JF-Expert Member
Oct 14, 2014
273
171
WANACHAMA 380 katika Mji wa Tunduma Mkoani Songwe, kutoka vyama mbalimbali vya upinzani kikiwemo chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wamejiunga na chama cha Mapinduzi

CCM wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa chama hicho, wakidai kufurahishwa na utendaji kazi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Pombe Magufuli.

Sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi katika Mikoa ya Mbeya na Songwe zimefanyika katika Mji wa Tunduma Mkoani Songwe jimbo ambalo ni ngome ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo Chadema ,ambapo Chama cha mapinduzi kimefanikiwa kuvuna wanachama 380,ambao wamerejesha kadi za vyama vyao na kupewa kadi za CCM lakini wakaomba ulinzi zaidi.

Mwenyekiti wa CCM katika Mikoa ya Mbeya na Songwe ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akaagiza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Songwe kuwachukulia hatua za kisheria wanaotishia usalama wa wengine.

Awali maadhimisho haya yameaanz na upandaji wa miti katika shule ya msingi Manga iliyopo Mji mdogo wa Tunduma.
Source:Muungwana Blog
 
Sisi hatuna tena muda wa kufuatilia uzushi kama huu.

Hivi CCM lini mtaacha kuandika uzushi na vitu vya kutunga?

Wanachadema hawakati tamaa kwa hizi pumba zako hapa.
Hivi Mbowe alidai wabunge wamehongwa biliioni kumi mbona haeleweki?
 
Hao watakuwa matahira tu na figure za kutengeneza. Washapewa mil 50 ,watoto wao washapata ajira, ndugu zao watumishi washapata promotion na nyongeza za mishahara, bei ya sukari na byakula vingine viko juu au chini, haki yao kikatiba kuihoji serikali ikoje? Kama wanaweza kujibu haya maswali basi Ninajua wao ni wazima wa Akili.
 
Watu wanakabidhi kadi ww kwako ni maigizo.Tuchukue hatua mapema kabla ya chadema kufilia mbali.

Wanachapisha kadi za Chadema kisha wanawagawia wana CCM wenzao waje wazirudishe na kudai kuwa wametokea Chadema, Ni ujinga tu.
 
Eti waliomba ulinzi...nyambafu yaani chama kinachotumia dola kunyanyasa wapinzani wanaigiza kuomba ulinzi tena!
 
Back
Top Bottom