CCM yauteka umma katika uzinduzi wa kampeni Uzini

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
[h=3]CCM WAZINDUA KAMPENI UZINI(JANA)[/h]

Dk.Karume ndiye aliyezindua kampeni hizi

Umati wa wana CCM kwenye uzinduzi wa kampeni jimbo la Uzini jana

Kampeni sasa zimepamba moto katika jimbo la Uzini Zanzibar baada ya CCM nayo kuzindua kampeni zake jana katika viwanja vya Ghana nyuma ya CHADEMA na CUF.Kwa kulinganisha kwa macho mkutano huu wa CCM umekuwa na watu wengi kuliko ile ya CHADEMA na CUF.Midundiko ya CCM na ngoma nazo zimeanza na jana vijana wa CCM nusura wapigane a wale wa CHADEMA baada ya kupita jioni barabarani wakipiga mziki,vijana na wanawake wa chadema walijikusanya na kuanza kuwazomea CCM jambo ambalo lilizua tafrani lakini likatulia baada ya gari iliyokuwa na vijana wa CCM kuondoka eneo hilo.Baadaye CHADEMA nao wakapita wakiwa na fuso lao kubwa la matangazo wakipiga wimbo wa CCM presha inapanda na kushuka huku vijana wengi wakiwa juu ya gari hilo.Hata hivyo hakuna vurugu kubwa zilizotokea.Uzinduzi wa CCM ulihudhuriwa pia na Mh.Pius Msekwa.
 
Jimbo linachukuliwa na CCM, maana wale wengine walikwenda kutambulisha chama chao kuwa nacho kipo japo kwa Zanzibar kilikuwa hakitambuliki.
 
mbona unauliza maswali na kujibu mwenyewe? si uache watu wachangie, umati unaosema upo wapi mbona watu wa kawaida hao.
 
vyama vitatu ndivo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo.CCM,CUF na CDM
 
Katika kampeni hizo wawaeleze wananchi kwamba kodi zetu zinatumika vipi watu kujilipa huko na zile zinazosalia kwa ajili ya kutuletea maendeleo.

Jimboni Uzini siasa ziwe ni za hoja zenye maslahi kwa umma si si kuuza sura na kusafirisha wafuasi toka sehemu za mbali kote nchini kwenda kuziba aibu ya CCM jukwaani.
 
Hao wamesombwa na batavuzi na chai halage hawajaenda kwa hiari
 
wote ni viongozi wa ccm hamna raia . umasikini wa zanzibar ulivyo nadhani wanfuata nguo za kuvaa
 
uchaguzi wa zanzibar kwangu ni sawa tu na wa cambodia au vanuatu
 
[h=3]CCM WAZINDUA KAMPENI UZINI(JANA)[/h]

Dk.Karume ndiye aliyezindua kampeni hizi

Umati wa wana CCM kwenye uzinduzi wa kampeni jimbo la Uzini jana

Kampeni sasa zimepamba moto katika jimbo la Uzini Zanzibar baada ya CCM nayo kuzindua kampeni zake jana katika viwanja vya Ghana nyuma ya CHADEMA na CUF.Kwa kulinganisha kwa macho mkutano huu wa CCM umekuwa na watu wengi kuliko ile ya CHADEMA na CUF.Midundiko ya CCM na ngoma nazo zimeanza na jana vijana wa CCM nusura wapigane a wale wa CHADEMA baada ya kupita jioni barabarani wakipiga mziki,vijana na wanawake wa chadema walijikusanya na kuanza kuwazomea CCM jambo ambalo lilizua tafrani lakini likatulia baada ya gari iliyokuwa na vijana wa CCM kuondoka eneo hilo.Baadaye CHADEMA nao wakapita wakiwa na fuso lao kubwa la matangazo wakipiga wimbo wa CCM presha inapanda na kushuka huku vijana wengi wakiwa juu ya gari hilo.Hata hivyo hakuna vurugu kubwa zilizotokea.Uzinduzi wa CCM ulihudhuriwa pia na Mh.Pius Msekwa.

Toa upupu hapa.Umekosa kazi ya kufanya
 
Nimeambiwa kulikuwa na watu wengi sana kuzidi waliosimama kumpokea Papa John Paul II au Mandela siku alipokuja Tanzania kwa mara ya kwanza.

Kwa kweli CCM walifunika sana sana. Hata Maalim Seif alionekana kuwapigia makofi wakali hawa. CCM Oyeeee!!!
 
Back
Top Bottom