Naamini kuwa hapa JF kuna magreat thinkers, lakini pia naamini hapa JF kuna watu ambao hata kama siyo great thinkers lakini wanaweza kutoa mchango muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.
Kwa maana hiyo basi ningeomba suala la posho ya wabunge litusaidie kutanua bongo zetu kuona jinsi gani tunaweza kusimamia masuala ya fedha ya nchi yetu (na hili tulifanye kuwa suala muhimu ndani ya katiba yetu). Kwa nini nasema hivi? Nina sababu kubwa zifuatazo:
- Siyo mara ya kwanza kwa wabunge wa bunge letu kujiongezea posho. Mtakumbuka wakati awamu ya nne inaingia wabunge waliomba kuongezewa posho na Spika wa wakati huo akasisitiza. Ingawaje Rais alijibu kuwa wabunge kwa sababu ni watu wazima watakuwa wamesikia kilio cha wananchi, lakini wote tunajua kuwa posho hizo ziliongezwa na wanachi hawakuweza kufanya kitu.
- Sasa hivi wabunge wameongezewa posho, Katibu wa Bunge kwanza alisema hakuna kitu kama hicho lakini Spika baadaye akakiri kuwa jamaa wameshaanza kulipwa posho mpya (ingawaje magazeti mengine wanasema Rais kakataa kusaini, kitu ambacho siwezi kuamini kwa sababu Wizara ya Fedha ilitowaje pesa kwenye kitu ambacho hakijapitishwa na serikali?). Hapo pia wananchi wameishia kuangalia tu na kupiga kelele
- Spika ni kiongozi wa wabunge hivyo yuko pale kwa matakwa ya wabunge. Sasa kama wabunge wanataka posho, je Spika anaweza kuwazuia? Hapa lazima tujiulize huku kwa Spika kuwajibika kwa Wabunge je hakuwapunguzii nguvu Maspika mbele ya wabunge. Suala hapa je nini kifanyike (au kwa maneno mengine wananchi wawe na sauti gani?) linapokuja suala ya maslahi ya wabunge? Kwa mtazamo ni lazima tuwe na chombo ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia maslahi ya viongozi wetu (hapa siyo wabunge tu na viongozi wa mihimili mingine).
- Posho za mhimili wa Mahakama hasa kwa majaji hatuzijui. Wao maslahi yao yanasimamiwa vipi na kwa kiasi gani posho zao zinaweza kudhibitiwa na wananchi. Je kama majaji wakitaka maslahi makubwa je Jaji Kiongozi kwa mfano anaweza kukataa? Na asipokataa nani anayeweza kukataa? (Hapa ningependa kujua posho zao ni kiasi gani pia kuanzia hakimu wa mahakama ya mwanzo hadi Jaji wa mahakama ya rufaa.
- Posho za mhimili wa serikali (yaani wafanyakazi wa serikali kuu kama vile makatibu wakuu, wakurugenzi) ambazo nazo hatuzijui kwa uwazi ni shilingi ngapi. Je ni kwa kiwango gani zinaweza kudhibitiwa na wananchi? Je wakitaka posho zaidi huwa inakuwaje?
- Vile vile posho za viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kama Polisi, Jeshi, Usalama nk ambazo nazo hatuzijui pamoja na maslahi yao. Je ni kwa kiwango gani zinaweza kudhibitiwa na wananchi? nk nk
Hizi zinanifanya nione kuwa suala la posho ya wabunge tulitumie kama "eye opener" litufungue tuone jinsi gani tunaweza kuboresha mfumo wetu wa usimamizi wa fedha. Suala la posho litumike kutuonyesha matundu mengine yako wapi?
Nawakilisha