CCM yatoa tamko kupanda kwa posho za vikao kwa wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yatoa tamko kupanda kwa posho za vikao kwa wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Apta Kayla, Dec 11, 2011.

 1. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika tamko hilo lililosainiwa na Nape Nnauye, CCM imepinga ongezeko hilo na hasa sababu iliyotolewa na Spika Makinda.
  Kwa taarifa zaidi fungua hapa http://www.mjengwablog.com
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Utapeli mtupu.Ukisikia usanii ndio huu.Si ajabu tamko hilo hilo litasainiwa na cuf kesho.Chadema wakishasema kitu madomokaya watafuata hivyo hivyo!
   
 3. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  duh, hakya nani siasa ni unafiki jamani...walofikia uamuzi wa kupandisha posho ni CCM hao hao chini ya makinda halafu saizi tunaambiwa hao hao sisiemu wanapinga posho duuuuuuuuu, hiii kali!! labda kama makinda na mwenzie katibu wamehamia chadema ndo tutalielewa tamko la CCM
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  WIZI NA USANII MTUPU!!!!! Rais wa nchi hajui lolote kuhusu posho mpya, Waziri wa Fedha ambaye ndiye mpangaji wa bajeti ya Serikali hajui chochote kuhusu posho mpya ila anayrfahamu kuhusu hili ni Spika wa Bunge!!!!! Halafu wengine ndani ya Magamba wanadai hazijalipwa wakati yule January Makamba anadai baada ya kikao cha masaa mawili aliletewa karatasi ya kusaini ili apokee mshiko wake wa posho mpya na akakataa kusaini. Serikali hii ni Serikali taahira, mambo yako shakalabaghala hakuna hata mmoja ajuaye nini kinachoendelea ndani ya Serikali.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  CCM wanajua kucheza game! Tushapigwa bao la kisigino!
   
 6. u

  ukudani Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii inaleta kichefuchefu,serikali gani haifanyi kazi pamoja,kila mmoja anakurupuka na lake.Waache kutuchanganya sisi wananchi,utawala uliyogawanyika hauwezi kudumu,wanatufanya kuwa matambara ya kufutia miguu yao
   
 7. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hii ni nitoke vipi baada ya sherehe za miaka 50 ya Tan... (sorry, nimesahau hiyo nchi iliyotimiza miaka 50 inaitwaje?
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu marekebisho hapo kwenye quoted red ni kwamba ile haikuwa posho mpya bali ilikuwa posho ya kuhudhuria kikao cha wizara ya nishati na madini ambacho kilikaa kwa masaa mawili, posho yake ilikuwa hiyo 280,000.

  Kwa maneno mengine kwa kuwa kukaa nje ya bunge masaa mawili hakutahesabiwa kwamba hujahudhuria vikao hizo posho nyingine zina remain intact hivyo ni something plus!

  Hii ndiyo serikali yetu pendwa ya wazee wa kuthubutu.
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Inakuwaje tena? Hivi nape anajisahau kwamba ni jana tu Spika Makinda alipewa nishani ya CCM kwenye sherehe za miaka 50 ya TGY?
   
 10. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Usimwamini muongo hata kama akisema ukweli
   
 11. A

  Ame JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Huku mwenyekiti wa chama (CCM) akimtunukia nishani spika huyo ambaye ameleta utata katika posho; Haijapita hata siku anakuja msemaji wa CCM anasema wanapinga posho...Hivi watanzania tunaongozwaje na watu wa kaliba hii jamani? kama wao wenyewe hawaelewani katika kauli na misimamo yao ndo watusaidie sisi na matatizo yetu lukuki? Kutegemea maendeleo kwa watu wa jinsi hii ni kama kumwomba kipofu akurembee binti yako anayeenda kwenye hafla ya harusi yake!
   
 12. A

  Ame JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Sikuwa nimeona comment yako hii nami nika post yangu yenye mshangao kama wako...Naomba Mungu sana katika nyakati kama hizi nisikutane na kiongozi yeyote wa CCM kwenye official discussion zozote maana nahisi naweza ishia magereza maisha yangu yote. Mungu naomba uniepushe kabisa these people can provoke jamani sijui wanafanya kusudi?
   
 13. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hawa jamaa wanatuona sisi makenge sana au?

  Nasema hivi, ipo siku watanzania watajua jinsi ya kutengeneza na kutumia molotov cocktail. Ipo siku, na wanaileta wao.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Hivi karibuni kumeibuka mjadala juu ya ongezeko la posho za wabunge kwa karibu ya asilimia 200, kutoka sh. 70,000 hadi sh. 200,000. Malipo hayo yaliyoibua mjadala baina ya wadau mbalimbali, ni yale yanayohusisha posho ya kikao cha bunge kwa siku. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefuatilia kwa makini suala hilo la nyongeza ya posho hiyo ya wabunge kama lilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na baadae kutolewa maelezo na Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila na Spika wa Bunge Anne Makinda.

  Kwa namna suala lenyewe linavyopewa msukumo, CCM imeona si vema kukaa kulikalia kimya na hivyo imetoa msimamo wake kama ifuatavyo:-

  1. [*=left]Linapotekelezwa jambo lolote kwa kigezo cha ugumu wa maisha au kupanda kwa gharama za maisha, ni lazima jambo husika lilenge kutatua ugumu huo wa maisha kwa makundi yote katika jamii na si kwa makundi machache ndani ya jamii.
   [*=left]Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo/tofauti ya mapato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.
   [*=left]Bunge ni chombo muhimu cha kutunga sheria, kinapoibuka na madai kwamba sababu za kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma kama alivyoainisha Spika wa Bunge, ndiyo inasababishahofu na mashaka miongoni mwa Watanzania. Na kwa kweli swali kubwa kwa Watanzania hao ni je, maisha yanapanda Dodoma pekeake na kwa wabunge tu?

  Hivyo basi CCM inashauri kwa kuzingatia masilahi mapana ya nchi na jamii yetu kwa ujumla, waheshimiwa wabunge wetu na mamlaka zingine zinazohusika na swala hili, kulitafakari upya jambo hili.


  Tunaamini busara itatumika kuachana na jambo hili, kwani kuendelea nalo kunaweza kutafisiriwa ni kuwasaliti watendaji katika sekta nyingine wakiwemo Walimu, askari, Madaktari na wengineo.


  Ni muhimu ifahamike kuwa kuongoza ni kuonesha njia, hivyo si sahihi kwa wabunge kuonesha njia kwa kujiongezea posho peke yao kwa kisingizio cha ugumu wa maisha huku wakiwaacha wananchi ambao ndiyo wanaowawakilisha bungeni wakikosa nafasi ya kupunguza ugumu wa maisha unaowakabili, jambo ambalo ni hatari.


  Katika hatua nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawapongeza sana Watanzania kwa ujumnla wao, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kwa kushiriki kwa amani na utulivu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

  Ushiriki wao kwa pamoja, umeyafanya maadhimisho hayo yafane sana. CCM inaamini kuwa maadhimisho haya ya miaka 50 yatatumika kuendelea kujenga uzalendo, umoja na mshikamano wan chi yetu katika kufikia maendeleo.

  Imetolewa na:-
  Nape M. Nnauye,
  KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA​
  ITIKADI NA UENEZI​

  11/12/2011​

   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mnyonge mnyengeni lakini haki yake mpeni. Kwa tamko hili nimefurahishwa na CCM kuwaunga mkono wananchi dhidi ya ubinafsi wa wawakilishi wetu bungeni. Kwani wanaangalia masilahi yao binafsi badala ya uwatetea watumishi wote wa umma. Licha ya posho hizo kulalamikiwa na wabunge wa upinzani na kada mbalimbali nchini hapo awali, lakini wabunge wamekuwa kama wameweka pamba masikioni wakiongozwa na Speaker wao Anna Makinda kujitajirisha kupitia bosho za vikao na biya haya wanazidi kuongeza kiwango cha posho hizo zaidi ya asilimia 80.
   
 16. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ah wapi! Wamejipiga bao wao wenyewe. Tangu lini Chama kinachoongoza serikali watendaji wake wakatoa matamko yanayotofautiana na msimamo wa chama? Hapa imekula kwao. Tunawasubiri 2015 waje na LOWASSA au MEMBE wao.
   
 17. j

  jozzb Member

  #17
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi karibuni kumeibuka mjadala juu ya ongezeko la posho za wabunge kwa karibu ya asilimia 200, kutoka sh. 70,000 hadi sh. 200,000.

  Mtandao huu umefuatilia kwa makini suala hilo la nyongeza ya posho hiyo ya wabunge kama lilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na baadae kutolewa maelezo na Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila na Spika wa Bunge Anne Makinda.

  Kwa kuzingatia maoni yao pamoja na tamko la chama cha Mapinduzi ,CCM,lililotolewa jana na katibu wa halmashauri kuu ya Taifa,itikadi na uenezi,mtandao huu umeona ni bora ukumbushe mambo yafuatayo:

  Ugumu wa maisha au kupanda kwa gharama za maisha, ni suala linalowakabili wananchi wote wa Tanzania.

  Tunawaomba waheshimiwa Wabunge na Serikali yetu wakumbuke kuwa mkoa wa Dodoma una wakazi wengi,tena kutoka sehemu mbali mbali za nchi.

  Hii ni pamoja na WANAFUNZI WA VYUO VIKUU,ambao wengi wao wanatoka mikoani,WAFANYAKAZI WA SERIKALI NA TAASISI BINAFSI,pamoja na WANANCHI WENYEWE WA MKOA WA DODOMA.Kwa hali kama hii,ingekuwa ni busara zaidi kama jambo hili lingelenga kutatua ugumu huo wa maisha kwa makundi yote katika jamii na si kwa makundi machache (WENYE UWEZO) ndani ya jamii.

  UNGANA NASI HAPA <<UGUMU WA MAISHA UNATUKABILI SOTE>>
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  imeshapigwa chini hiyo
   
 19. F

  Festo3010 Member

  #19
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nami ntashanga sana kama raisi we2 atasaini huo ujinga!
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hilo tamko liendane na utekelezaji kwa vitendo,tuone amri inatekelezwa kivitendo,nampongeza vuvuzela lakini akumbuke kuwa yeye ni boss na msimamizi wa hao wabunge waliojiongezea posho kinyemela huku wakijua nchi inakabiliwa na matatizo lukuki likiwamo la kuporomoka kwa uchumi na kupanda kwa gharama za maisha nchi nzima (SIO DODOMA PEKEE).

  Akina shibuda na joseph selasini nao wadhibitiwe waache kutoa matamko na kauli tata.
   
Loading...