CCM yatamba kuendelea kubaki madarakani 2015

CCM yatamba kuendelea kubaki madarakani 2015

mwanakidagu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
208
Reaction score
78
CCM kupitia kada wake Mzee Bulembo,wameapa kusalia madarakani kwa gharama zote.

Source,gazeti la uhuru
 
Hata Mobutu alikuwa na fikra kama zao ila leo yuko wapi?
 
Bulembo mwenyewe ni Kihiyo so hawa ndo viongozi wa magamba.
 
mi naogopa sana haya maccm yanaposema ht kwa gharama yeyote, au watawateka wanaharakati wote wa mapinduzi na kuwapeleka mabwepande km ulimboka! Au watatumia bunduki kuzuia wananchi kumpata kiongozi wa chama wanayemtaka? Ila tu bulembo atambue kuwa '' it was and that has no longer'' hvy acjidanganye kwa kujiapiaza kn kwamba wana ht ya kutawala milele na ccm yao.na zaidi tunataka wakamatwe wale waliomteka dr. Ulimboka na wale wote walificha mabilion ya mapes uswis.
 
Ukiangalia matukio na kauli za viongozi wa vyama vikubwa vya siasa utagundua kuna vita kubwa ya chini chini juu ya uchaguzi wa 2015. Kwa mtazamo wangu nimegundua Chadema silaha yao ni nguvu ya umma, ccm wanatumia plani A, B na C zote kwa wakati mmoja, plani A; kuhakikisha chadema inasambaratika kabla ya 2015, hapa ccm wanatumia vyombo vya dola, pesa na mapandikizi yao ndani ya Chadema,plani B; kuhakikisha katiba mpya haiwi tayari wakati wa uchaguzi 2015, marekebisho ambayo yaliyotakiwa kufanywa kwenye mchakato wa katiba hayajafanywa yote, hii imepelekea chadema kujitoa ktk mchakato huo, huo ulikuwa ni mpango wa ccm ili mbeleni waseme chadema ndiyo wamechelewesha kupatikana katiba mpya, plani C; kuhakikisha kunakuwa hakuna amani ifikapo 2015, hivyo kuhairisha uchaguzi. Huu ni mpango wa mwisho lkn maandalizi yake yanafanyika sasa hivi, hapa wanatumia dini kutuchonganisha wakrito na waislam, ukiangalia kwa undani utagundua serikali inahusika kwa namna moja au nyingine ktk vurugu za kidini, nia kubwa ni kutaka kuona wakristo wanajibu mapigo ili mpango uwe umekamilika, hapa itakuwa vita kati ya wakristo na waislam, wao watakuwa wakitafuna nchi huku wamezungukwa na ulinzi mkali wao na familia zao.
 
Sadam mwenyewe alichomolewa madarakani pamoja na maisha mazuri waliyokuwa nayo walibya but aliondoka madarakani mpaka wakaona wamwue tu itakuwaje ccm ambayo ni uvundo wa uongozi
 
Sadam mwenyewe alichomolewa madarakani pamoja na maisha mazuri waliyokuwa nayo walibya but aliondoka madarakani mpaka wakaona wamwue tu itakuwaje ccm ambayo ni uvundo wa uongozi

du! sadamu na libya!!!!
 
Ccm hawatakubali kutoka mwaka 2015, na ndo maana wameshabaka mchakato mzima wa kupata mabaraza ya katiba!
 
Kuondoka madarakani CCM ni lazima mwaka 2015 hata wakitumia mabavu vp maana Umma wa Tanzania Uko tayari kuupokea ushindi wa Chadema mwaka 2015
 
MLENGWA WA MLIPUKO ALIKUWA BALOZI WA VATICAN?

(Naona mods wana watu wao wenye haki ya kuanzisha threads, sisi wengine haturuhusiwi)

Ndugu WanaJamvi;

Kwa muda sasa kumekuwa na hoja mbali mbali juu ya uhalali wa uwepo wa Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania. Katika hili kuna, kuna pande kuu mbili zinazokinzana - wanaopinga na wanaounga mkono kama ifuatavyo:-

(1) Wanaopinga: wanajenga hoja kwamba kwa kuwa Vatican ni nchi ya kidini (Kikatoliki) na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba, Tanzania haina dini hivyo sio sahihi kwa "nchi" hiyo kuwa na ubalozi wake hapa nchini. Wengine wanaenda mbali zaidi kiasi kwamba hawataki kukubali Vatican ni nchi. Hata hivyo "wanalegeza" masharti kwamba kama Vatican ina ubalozi wake hapa basi ni halali kwa Tanzania kama nchi kuwa mwanachama wa taasisi za kidini kama OIC. La kushangaza hapa ni kwamba kwao uhalali wa Ubalozi wa Vatican utakuwepo endapo Tanzania itakuwa mwanachama wa hizo taasisi za kidini vinginevyo sio halali.

(2) Wanaounga mkono:hawa wanajenga hoja kwamba; kwanza Vatican ni nchi huru, yenye mamlaka kamili, na inayojitegemea kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno "nchi" lilivyo na linavyotambulika kimataifa. Na wanaenda mbali zaidi kwamba sio tu kwamba Vatican ni nchi bali inatambulika hivyo rasmi na UN. Hivyo, kwa hoja hii, ni sahihi kabisa Vatican na Tanzania kuwa na mabalozi wanowakilisha nchi zao.

MLIPUKO WA LEO:

Kati ya viongozi wakuu wa Kanisa waliokuwepo kwenye shughuli ya leo kule Olasiti, Arusha, ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania ambaye pia ana hadhi ya Askofu Mkuu. Hivyo zimeanza kuzagaa habari pengine kutokana na ukinzani wa baadhi ya makundi kutotaka Vatican kuwa na ubalozi wake hapa nchini, kuna uwezekano pia mlengwa mkuu alikuwa Balozi husika. Mimi sijui, ila kama GT tudadavue na hili.

LAWAMA:

Lawama pia zimeanza kuelekezwa kwa serikali kwa kutochukua hatua madhubuti na kwa wakati pindi zinapotokea chochoko kama hizi katika jamii. Kwa mfano, hili la upotoshoji wa uhalali wa Ubalozi wa Vatican hapa nchini propaganda zake zimeenezwa kwa muda mrefu sana kwa njia mbalimbali kama mihadhara, ibada, na hata kwenye media mbalimbali. Badala ya serikali kutolea ufafanuzi wa uhalali wa huo ubalozi, imekuwa kimya bila kujali athari za baadaye za propaganda hizi chafu pengine kwa falsafa ya "ni upepo tu utapita". Je, ni kweli serikali inastahili lawama katika hili?

HITIMISHO:

Je, kama serikali ikitekeleza madai YOTE ya haya makundi, kuna uwezekano wa chokochoko hizi kukoma na hivyo nchi yetu kuwa ya amani na utulivu kama ilivyoachwa na waasisi wetu? Lakini je, walengwa wa haya matukio ni wakatoliki peke yao? Au ni pamoja na makundi mengine? Haya matukio yana uhusiano wowote na siasa za nchi yetu? Mimi sijui, nalileta kwenu wakuu.
 
CCM kupitia kada wake Mzee Bulembo,wameapa kusalia madarakani kwa gharama zote.

Source,gazeti la uhuru
"Kama kichaa, na ukichaa wake ameweza kuwaongoza wasomi wote na kuwafungulia Tawi (kuwachorea picha ya mlango ukutani) na wakamfuata, Basi aliowaongoza ni misukule" Watanzania watakuwa misukule wote kuirudisha CCM!!!!!!!!!!!!
 
ivi hata yakizungumziwa ya maana mnaleta hoja ya cdm humu? mkoje jf
 
Back
Top Bottom