CCM yapoteza majimbo 51


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,379
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,379 280
Matokeo ya uchaguzi mkuu yanavyozidi kutangazwa imefahamika kuwa Chama tawala CCM kimepoteza m ajimbo 51 nchini kote.Meneja wa kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana amekiri mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuwa CCM imemepoteza majimbo has 29 Tanzania Bara na majimbo 22 Visiwani Zanzibar.
Kinana amekiri kuwa athari ya kuanguka kwa CCM inatokana na migogoro ya kura za maoni .

Hata hivyo amesema CCM inatarajia kupata kura za rais kwa kiwango cha asilimia 78.4. Endelea kupata habari zaidi


=====================================================================
Shein rais ZanzibarButahe

CCM jana ilifanikiwa kunyakua tena kiti cha urais baada ya mgombea wake, Dk Ali Mohamed Shein kuibuka mshindi kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili akimshinda mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.Dk Shein, ambaye anamalizia kipindi chake kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano, sasa anakuwa rais wa saba wa Zanzibar, ambayo inaundwa na visiwa vya Pemba na Unguja akimbadili Abeid Amani Karume pia wa CCM.

Lakini Dk Shein atakuwa na changamoto kubwa ya kuwa kiongozi wa kwanza kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa na atashirikiana na Maalim Seif, ambaye kwa mujibu wa marekebisho ya katiba baada ya kufikiwa kwa maridhiano, anakuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Akitangaza matokeo hayo, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), Khatib Mwinyichande alisema Dk Shein alipata kura 179,809 ambazo ni sawa na asilimia 50.1.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Maalim Seif, ambaye amegombea urais kwa mara ya nne, alipata kura 176,338 ambazo ni sawa na aslimia 49.1 ya kura zote 358,815.

Alisema kuwa vyama vilivyosimamisha wagombea urais katika uchaguzi huo ni pamoja na AFP, CCM, CUF, Jahazi Asilia, NCCR-Mageuzi, NRA na Tadea.

"Matokeo yanaonyesha kuwa mgombea wa NRA amepata kura 480 sawa na asilimia 0.1, wa CCM kura 179,809 sawa na asilimia 50.1, wa CUF kura 176,338 sawa na asilimia 49.1, Jahazi Asilia kura 803 sawa na asilimia 0.2, NCCR kura 363 sawa na asilimia 0.1, NRA kura 525 sawa na asilimia 0.1 na Tadea kura 497 sawa na asilimia 0.1," alisema Mwinyichande.

Tofauti na ilivyokuwa kwenye chaguzi zilizopita, jana hali ilikuwa shwari wakati mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) akitangaza matokeo ya urais. Shangwe zilizofuata baada ya Dk Shein kutangazwa kuwa mshindi, hazikunakshiwa kwa vijembe vya kuudhi wapinaani kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye chaguzi zilizopita.

Hata Maalim Seif alikuwepo wakati wa hafla hiyo na akakubali kwenda mbele kutoa hotuba ya kukubali matokeo ambayo ilijaa hekima na busara ikieleza umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili kuu, huku ikitaharidha kuhusu vitendo vinavyoweza kuvuruga maridhiano hayo.

"Kwa mara ya kwanbza uchaguzi umefanyika kwa amani, bila ya vitisho. Kampeni ziliendeshwa kiungwana na kwa ustaarabu," alisema Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

"Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Dk Ali Mohamed Shein kwa kupata ridhaa ya Wazanzibari atuongoze kwa miaka mitano inayokuja.

"Dk Shein ana uwezo, uzoefu na mahaba kwa nchi yake. Tunatumaini ataongoza kwa busara na hekima kwa lengo la kuunganisha nchi yetu. Naamini kuwa Wazanzibari walifanya maamuzi sahihi Julai 31. Tarehe hiyo waliamua kuunda serikali shirikishi."

Seif, ambaye alikuwa akizungumza kwa utulivu, alisema uamuzi huo umeweka enzi mpya ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwamba Wazanzibari wamempa Dk Shein jukumu la kuongoza kwa mara ya kwanza serikali ya umoja.

Lakini mkongwe huyo wa siasa visiwani Pemba na Unguja hakusita kutoa tahadhari kwa Dk Shein na CCM wakati akitaja mambo makuu matatu muhimu.

"Kwanza ni shukrani kwa Tume ya Uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi ambao ulikuwa na afadhali kulinganisha na chaguzi nyingine," alisema.

"Lakini kuna dosari ambazo ni lazima zirekebishwe. Mwenye matatizo si wewe mkurugenzi... ni baadhi ya maofisa wako."

Alieleza matatizo ambayo maofisa wa uchaguzi wamekuwa wakiyafanya akisema yanasababisha watu wasiwe na imani na tume.

"Jambo la pili ni kwamba Dk Shein ni rais mteule. Ametangazwa tu kuwa mshindi, lakini hakuna mshindi. Washindi ni Wazanzibari wote na Shein ni mteule tu."

Dk Shein alionya katika suala lake la tatu kuwa baada ya matokeo hayo kusiweo na siasa za kubezana.
"Siasa za kubezana zitachafua hali ya hewa kabisa," alionya Maalim Seif akimtaka Dk Shein afikishe ujumbe huo kwa viongozi wenzake wa CCM na wanachama wao.

Naye Dk Shein, ambaye huzungumza kwa utaratibu na mpangilio, alimshukuru Maalim Seif kwa hotuba yake, aliyoielezea kuwa ilijaa busara na hekima na kuahidi kutekeleza yote ambayo kiongozi huyo wa CUF aliyazungumzia.

"Nafahamu fika kuwa kazi hii ni nzito... Mungu anisaidie, anipe hekima na busara ili niifanye kwa uadilifu," alisema Dk Shein.

Shein sasa atakuwa na changamoto jipya la kuwa rais wa kwanza kuongoza Zanzibar akishirikiana na chama kikuu cha upinzani, CUF baada ya pande hizo mbili kufikia maridhiano ambayo yalilifanya Baraza la Wawakilishi kuridhia kupitisha sheria inayoruhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwa mujibu wa muundo mpya wa Serikali ya Zanzibar, mshindi wa uchaguzi mkuu ndiye ataingia Ikulu akiwa rais na mgombea aliyeshindwa atakabidhiwa nafasi ya makamu wa kwanza wa rais.

Muafaka huo ulifikiwa baada ya viongozi wakuu wa vyama hivyo viwili, Rais Amani Abeid Karume kukutana kwa faragha Ikulu na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad Novemba 4, 2009.
Taarifa iliyotolewa baada ya faragha hiyo ilieleza kuwa wawili hao walizungumzia haja ya kudumisha amani na utulivu pamoja na kuwa na maelewano na ushirikiano baina ya wananchi wote wa Zanzibar.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
inols

inols

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2010
Messages
285
Likes
16
Points
35
inols

inols

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2010
285 16 35
Namuona handsome boy in the greens, atafikiri awamu hii mpaka kichwa kitapasuka, I salute you my president but i've this message to give you...... "We are fade up with your part and you yourself, i just want to let you know that your days are numbered even if you're going to be appointed as the president for this term" pole sana. It's real sad to allow the part to collapse in your hands and there is nothing at all you can do may be if you turn to the living God and not otherwise.Bye byeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 

Forum statistics

Threads 1,250,278
Members 481,278
Posts 29,726,867