CCM yamgeuka Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamgeuka Lowassa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 24, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MGOGORO wa kisiasa wa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, unaweza kuzaa mpasuko siyo tu kwa wakazi wa Arusha, bali hata kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba, kutofautiana na mmoja wa makada wake maarufu, Edward Lowassa.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Makamba akionesha kutofurahishwa na kauli
  ya Lowassa ya kutaka mgogoro huo wa umeya wa Arusha umalizwe kwa amani kwa kuzikutanisha pande zinazohusika, alisema taarifa ya Lowassa iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, imemshitua sana.

  Pamoja na kuzungumzia amani, Lowassa pia alisisitiza wahusika kuelimishana ili kuunusuru mji huo wa Arusha na Taifa kwa ujumla, usitumbukie katika ghasia.

  Lowassa alivitaka vyama hivyo kukaa meza moja kumaliza vurugu zilizotokana na uchaguzi wa
  kumpata meya wa jiji hilo ambapo iliripotiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisababisha vurugu na kukamatwa na polisi ambapo baadaye aliachiwa.

  Jana, baadhi ya magazeti yalimnukuu Lowassa akisema juzi katika mkutano mjini Arumeru kuwa, “leo nimekuta Mji wa Arusha ukiwa umezingirwa na askari Polisi na sehemu zingine kulikuwa na gari la maji ya kuwasha kwa ajili yakulinda usalama wa mji na watu wake.

  “Hali hii imetokana na uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, nawaomba viongozi wa vyama
  vinavyovutana, wakae haraka ili kuondoa hali hii ili Arusha isije kuwa kama Ivory Coast…Arusha ni yetu sote.” Alisema.

  Hata hivyo Makamba kutokana na taarifa za vyombo vya habari alisema:“Nimeshitushwa sana na taarifa hiyo, nimeshituka kwa vile namjua vizuri Mheshimiwa Lowassa.

  Ni kiongozi makini, hakurupuki, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na anazijua sana taratibu za Chama.

  Hawezi kukikemea Chama chake kupitia magazetini. “Anapo mahali pa kukikosoa kama kimekosea. Ni katika vikao. Nadhani amenukuliwa vibaya.”

  Makamba alisema vurugu zinazoendelea Arusha haziwahusu na wanaopaswa kukemewa kwa kutaka kuigeuza Arusha kuwa Ivory Coast, siyo CCM kwani wao wanaamini uchaguzi uliendeshwa vizuri na mgombea wa chama chao ndiye Meya wa Arusha kwa sasa.

  Makamba alisema hoja ya Lowassa kuwataka wakae meza moja na Chadema, haina msingi
  ambapo alisisitiza “hatuna ugomvi na Chadema na mgombea wetu ameshinda, upande usioridhika na matokeo unapaswa kuyapinga kwa mujibu wa taratibu zilizopo.”

  Alisema uchaguzi huo haukusimamiwa na CCM, bali Mkurugenzi wa Jiji la Arusha hivyo kasoro kama zipo, CCM haipaswi kulaumiwa, akifafanua kuwa “upande ambao hauridhiki na matokeo hayo, unapaswa kuyapinga kwa mujibu wa taratibu zilizopo.”

  Lakini akizungumza kwa simu jana jioni kutoka nyumbani kwake Monduli, Lowassa alisema hajayaona magazeti ya jana yalivyoandika, lakini alichokisema juzi ni kwamba vyama husika vikae na kuzungumza namna ya kumaliza tofauti zao kwa sababu vurugu hazina maslahi kwa Arusha na Taifa kwa ujumla.

  “Niko Monduli, sijaona magazeti ya leo (jana), lakini nilichokisema juzi ni kwamba vyama husika, vikae na kuzungumza kwa nia ya kumaliza tofauti zao. Sijamkemea mtu, sijasema nani mshindi, nani ameshindwa. Nimetoa ushauri, kwa sababu sitaki amani ivurugwe,” alisema Lowassa.

  Alisema katika ushauri wake, hakutaja jina la chama chochote, na anaweza kuwa amenukuliwa
  vibaya, lakini la msingi alilosisitiza ni kuwa suala la kuelimishana.

  “Pengine hawajui utaratibu, ni suala la kuelimishana. Tusipigane mitaani, tuwaelimishe wenzetu. Nisingependa kuona Arusha inakuwa na vurugu, tunahitaji mji wetu uwe na amani,” alifafanua Mbunge huyo wa Monduli.

  Chadema juzi iliandaa maandamano na vijana wa chama hicho kuingia mitaani na kulifanya Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa maji ya kuwasha.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Is Lowassa the hero?
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  No siyo hero he is the loser
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  But chadema are the heroes
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Lowasa anawajua CDM na pepos power ndio maana alishaona kitakachofuata...Makamba yeye annafikiriaa mlungula na kuwatisha wahindi wachangie chama...na yeye...hana fikra kama aliemuweka!!!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwa hili Lowassa was right na tumeona aliyoangaliza...:faint2:
   
 7. T

  The Man Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee makamba nafikiri anamatatizo ya akili na kimsingi sija wahi kumuelewa.....kauli zake nyingi ni mbofumbofu na ni za kukurupuka. Ni wazi hili swala la arusha ni zito na linahitaji ufumbuzi wa haraka , kama inafikia mpaka watu wanauawa baada ya kupata vibali halali vya kuandamana hili ni suala la kitaifa na sio la chama tena. Pia lazima ajue kuwa we have freedom of expression , Lowasa amezungumza kama yeye na sio kwa niaba ya chama. Kuna watu kibao ambao wamewahi kutoa maoni yao na si kupitia chama lakini Makamba hakutoa tamko kama hili mfano..Mkapa , Sumaye , Warioba etc kwenye suala la Katiba, mbona hakutoa tamko la kuwapinga kama hili......!! huyu ni mnafiki ambaye anastahili shahada ya UNAFIKI ULIOTUKUKA!!!!. Aibu itampata pale serekali itakapo ridhia kurudia uchaguzi..... kama aibu ilivyo mpata kwenye suala la serikali ya mseto zanzibar na suala la Katiba.....!!!
   
 8. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Lowasa alisoma alama za nyakati..mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  EL anajua kilichotokea Arusha ndiyo maana anaomba pande zote zikutane!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  cha kujiuliza, ni kwanini ccm wanaendelea kumuacha pale wakati yeye ndiye anayekiangusha chama?
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  CCM imekosa dira
   
 12. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Baniyani Mbaya lakini kiyatu chake ni dawa Heko Lowassa sasa amekubali uliyoyasema wiki hivi nyuma endelea kuwa na msimamo wako asikunyime usingizi kitaka taka makamba na kukuzonga .
   
 13. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  No he is not a hero. Lowassa anaelewa kwamba uki-provoke watu wa Arusha fujo itakua kubwa, na watu watakimbilia kuteketeza vitega uchumi vyake vilivyoko Arusha. Ni hilo tu! Tunaweza kusema anajua kuisoma jamii yake vizuri lakini he is still fisadi papa.
   
 14. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mimi huwa najiuliza siku zote ivi bado kuna watu wanaosikilizwa na chama kwenye CCM zaidi ya kikwete na Makamba. Pamoja na kwamba most of them ni mafisadi lakini busara ndogo ndogo nazo hamna kabisa? Nilifikiri wale wazee waliokuwapo kipindi cha Nyerere na Mwinyi bado watakua na busara fulani yakukishauri chama kuepusha mambo kama ya Arusha. Where is Malecela, Msuya, Msekwa, Kingunge, Mwinyi, Kimiti, Bomani, Warioba, Kahama etc etc etc. Sitaki kuamini na wao wanamuogopa Rostam.
   
 15. L

  Leornado JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyu Makamba hana presha ajifilie mbali?? tumemchoka sana.
   
 16. T

  The Future. Member

  #16
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijamuelewa vizuri makamba alivyosema uchaguzi wa meya ulisimamiwa na mkurugenzi na wala si CCM,nakaka kujuzwa mkurugenzi anachaguliwa au anateuliwa kama RC na DC? Kama anateuliwa bila shaka serikali ya ccm si ndio imemuweka madarakani?logically ni mmoja wao tu,kwa hili hawawezi kunidanganya.
   
Loading...