CCM yamfukuza mwanachama wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamfukuza mwanachama wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tina, Oct 21, 2009.

 1. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Unyamikumbi, katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida amefukuzwa uanachama kwa madai kwamba alikuwa akifanya kampeni za kuvisaidia vyama vya siasa kambi ya upinzani kupata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Okt, 25, mwaka huu.

  Hatua ya mjumbe huyo wa kamati ya siasa, Zakaria Mkuki kufukuzwa imekuja siku chache tu baada ya kugombea kwake nafasi mbili ikiwemo nafasi yaw mwenyekiti wa Kijiji cha Kisaki pamoja na ujumbe,nafasi ambazo hakufanikiwa kuzipata.

  Hata hivyo inasemekana kuwa baada yaw mwanachama huyo kukosa nafasi hizo kwenye kura za maoni za uchaguzi huo ndipo Mkuki alipoanza kufanya kampeni za chini chini za kutaka wagombea wa vyama vya upinzani katika nafasi mbalimbali walizoomba wanakibwaga chama cha mapinduzi.

  Habari za uhakika kutoka katika Kijiji cha Kisaki,kilicho umbali wa takribani kilomita kumi kutoka mjini singida zinasema kwamba mjumbe huyo alifukuzwa na mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Unyamikumbi, Jakobo Lamba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha NgÂ’aida wakati wa kampeni za chama hicho.

  Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zimethibitishwa pia na mjumbe mmoja kutoka katika Kata hiyo ambaye si msemaji wa chama zinasema kuwa baada ya Mwenyekiti kubaini mchezo huo mchafu wa mjumbe wake dhidi ya vyama vya upinzani, ndipo aliamua kumfukuza uanachama kwenye mkutano huo wa hadhara.

  Kwa mujibu wa mtoa habari huyo katika majibizano baina ya mwenyekiti na mjumbe huyo,huku mwenyekiti akitaka mjumbe kurudisha kadi ya CCM, lakini mjumbe Mkuki alikataa kata kata mbele ya mkutano huo kwa madai kuwa kadi aliyonayo ni mali yake kwani aliinunua kwa fedha zake mwenyewe.

  Hata hivyo kutokana na sakata hilo uongozi wa ngazi ya juu katika kata hiyo unatarajia kukutana kabla ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa ili kutoa tamko rasmi kuhusu sakata hilo .

  Habari zaidi kutoka katika Kijiji hicho cha Kisaki zinasema kuwa huenda viongozi wa chama watakaokutana wakaamua kumfuta uanachama mjumbe huyo ili kujenge nidhamu ndani ya chama hicho kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi hapo baadae mwakani.

  Sakata hilo limekuja siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote siku ya Oktoba 25 mwaka huu, kwa kuchaguliwa viongozi katika ngazi za mitaa, vitongoji na vijiji.

  Hivi karibuni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida,Bi Naomi Kapambala alidai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida tayari kimeibuka na ushindi kwa zaidi ya asilimia 62 kati ya vijiji 415 vya mkoa wa Singida wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupitia tiketi ya CCM wamepita bila kupingwa kwenye jumla ya vijiji 261.
   
 2. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  kweli 2010 hiyooooooooooooo...................
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Karibu NCCR Mageuzi au TLP
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  iko kazi ...mbio kuelekea kwenye 2010
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teh teh huyu naye kwa nini hakuomba msamaha kama spika 6?wangemsamehe tu si mwenzao wametoka naye mbali
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Halafu anafukuzwa jukwaani? yeye anajitetea kadi alinunua??
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Je ni kikao gani kilifanyika na kumvua uanachama? Je mwenyekiti wa chama wa kijiji au wilaya anaweza kumvua mtu uanachama bila kufanyika kikao cha chama mtuhumiwa ajieleze?
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Rev.
  Kwa CCM ya leo lolote linawezekana.
   
Loading...