CCM yalaani vikali kuteswa kwa Kibanda

CCM yalaani vikali kuteswa kwa Kibanda

hugochavez

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
1,907
Reaction score
1,009
[h=5]CHAMA CHA MAPINDUZI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia Jumatano Machi 6, 2013.

Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa Absalom Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na Watanzania wote.

CCM tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na kukomesha matukio ya namna hiyo.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda, wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.


Imetolewa na:

Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI

08/03/2013[/h]
 
Vipi alivyouwawa MWangosi mulikuwa wapi???

Hii ni style ya kujipiga kofi mwenyewe kisha unalia. Ngoja tuone mwisho na safari hii wakenya wote wapo kwao kwenye uchaguzi.
 
Ha ha ha mbavu zangu !!!! Kwi Kwi Kwi ...du Kweli Tz hakuishi vituko
 
Hakika Nape Nnauye ni flip-flop , si wewe ndio ulikuwa unatoa tuhuma kwa chadema kwenye mitandao? Mbona hapo hujuaandika ulicho kiandika kwenye mitandao? Mbona hamjiamini? Tangia lini mwizi akajichunguza? Mmezoea kuropoka wewe na wanao wakina Mtela Mwampamba nilitegemea uyaandike kwenye taarifa ya vyombo vya habari yale uliyo yaandika fb!

Hii inaonesha jinsi usivyo mwanaume kamili, kwani mwanaume kamili hayumbi kwenye misimamo yake!

Ni dhahiri cccm imejifia na wamebaki waropokaji tuuu!
Cc Juliana Shonza Mtela Mwampamba!
 
Last edited by a moderator:
Vipi kuhusu Daudi Mwangosi na Dr.Ulimboka?

Wanafiki utawajua tu!
 
Muulize mbona hajaandika aliyo yaandika yeye na wanae kule fb?
Anaogopa nini?
Vipi alivyouwawa MWangosi mulikuwa wapi???

Hii ni style ya kujipiga kofi mwenyewe kisha unalia. Ngoja tuone mwisho na safari hii wakenya wote wapo kwao kwenye uchaguzi.
 
Muulize mbona hajaandika aliyo yaandika yeye na wanae kule fb?
Anaogopa nini?

Huyu jamaa sidhan kama anafikiriaga cha kufanya. Ila yote ipo siku moja haya yote yatakwisha ispokuwa hapa dunian hata ahera.
 
matendo kama haya ni ya kulaaniwa kwa nguvu zote..........haiwezekani binadamu akateswa hivi halafu yaishe kirahisi tu
 
Serikali SIKIVU ya CCM imetakiwa na CCM kuwatafuta WAHALIFU na kuwafikisha kwenye vyombo vya sharia. Mwenyekiti wa CCM ndiye RAIS, AMIRI JESHI MKUU na MKUU wa vyombo vyote vya usalama hapa nchini.
 
Hajawai, hatowai kuwa na uwezo wa kufikiri kamwe!

Huyu jamaa sidhan kama anafikiriaga cha kufanya. Ila yote ipo siku moja haya yote yatakwisha ispokuwa hapa dunian hata ahera.
 
siku hizi CCm ni kushoto kulia geuka, yaani haina mabega wala kichwa, kwa kuwa kiongozi wao Mnauye hana jipya.
 
Hizo nguvu zote ni zipi na sheria inachukua mkondo wake kwa akina mm ili liwe fundisho kwa wengine, where's Ighondu!!!!!!!!!
 
Nilitegemea kuona kauli na matamko kama haya yakitolewa na vyama vingine kama chadema na vingine kama ilivyokuwa kwa mwangosi na wengineo. ila ukimya wao unatoa picha tofauti na tafsir zisizo na majibu ya moja kwa moja.
 
CCM na Nape mnajichanganya saana.
Hivi watu wangapi wamefanyiwa unyama na ninyi kama chama chenye serikali tawala hamjachukua hatua.

Mumewahi kuihoji serikali yenu juu ya unyama wa Uliomboka na kwanini kesi imefichwa achilia mbali series za Kova.

Mumewahi kuhoji kuhusu Mwangosi na nini kimetokea baada ya mauaji.

Sheikh Sarago kamwagiwa Tindikali, nani amefikishwa mbele ya sheria

Orodha ni ndefu sana, ninachotaka kusema hapa ni kuwa uharaka wa makamu wa rais kwenda Muhimbili unaonyesha jinsi gani mnajishuku.

Kuna njama za makusudi za kutaka kulihusisha tukio hili na kazi ya kibanda hasa baada ya kuhama.
Njama hizo zinalenga chama cha upinzani.

Utakuwa ni ujinga kuamini kuwa hilo ndilo tatizo huku tukijua fika kuwa matatizo ya akina Uliomboka, Mwangosi na wengine wengi hayajafanyiwa kazi na wala hayatafanyiwa kazi.

Kwanza wananchi wanataka kujua nini kilimtokea Ulimboka na Ramadhan yupo wapi akiwa ametajwa.
Tunataka kujua uchunguzi wa raia wa Kenya aliyeko rumande bila makosa.
Haki gani mnaitaka wakati mumeweka mtu rumande bila hatia.

CCM, lazima kwanza mujibu tuhuma lukuki na wala hili lisiwashugulishe
 
Vibaka wa Chadema kwa kujibaraguza bhana!!!! Sasa mumpige nyie kwa kukerwa na makala zake za kuisifia CCM then mje hapa mnachongaaaaaaaaaaa! Nyambafu zenu
 
Back
Top Bottom