CCM yakatataliwa msibani DSM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yakatataliwa msibani DSM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by pilau, Sep 30, 2012.

 1. p

  pilau JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olympic Tanzania marehemu Erasto Zambi (aliyewahi kuwa mwalimu wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati anasoma shule ya sekondari Kibaha) kuligubikwa na sintofahamu baada ya msimamizi wa utaratibu wa shughuli za mazishi MC a.k.a. (msema chochote) kutangaza kuwa jeneza la mwili wa marehemu wakati linaingia katika maeneo ya nyumbani kwake litabebwa na wananachama wa CCM wa Kata ya Makuburi - Ubungo, tangazo hilo lilileta malalamiko na minong'ono miongoni mwa waombolezaji wakiwemo ndugu wa karibu wahusika wa msiba huo, kwani watu walishangaa kauli ya MC huyo kwani hapakuwa na mawasiliano yoyote ya CCM Kata hiyo na marehemu kabla hajafariki na hapakuwa na msaada wowote katika kumuuguza uliotoka katika kata hiyo au viongozi wa CCM walio shiriki katika kumuuguza kwa njia moja ama nyingine katika siku za mwisho za ugonjwa wa marehemu, Malalamiko hayo yalisababisha MC huyo kutamka hadharani kuwa swala la itikadi katika msiba huo limeleta UTATA na kutangaza kuwa jeneza la marehemu Erasto Zambi litabebwa na watu wote bila ya kuzingatia itikadi za vyama vya siasa, hii inasemekana sio mara ya kwanza kwa vyama vya siasa kuingilia taratibu za mazishi katika sehemu mbalimbali nchini je Tunakwenda wapi? kwani hata baada ya kubeba jeneza na kulivika bendera ya chama husika hakuna misaada yoyote inayopelekwa kwa wafiwa na familia baada ya mazishi.
   
Loading...