CCM yakanusha tuhuma za CHADEMA

CCM yakanusha tuhuma za CHADEMA

Nape afadhali umekanusha Kaka ! Sasa naomba nikuulize swali la kizushi , Hivi ni kweli kwamba ulipanga kuzunguka na Juliana nchi nzima ? Kwa nini usizunguke na Mbabe wako Lowasa ? Mbona huyo ni maarufu sana kuliko Juliana ! Si umeona juzi ubwabwa wake ulivyopata wafuasi wengi !
 
by Yericko Nyerere.
Taarifa za kuaminika toka ndani ya ccm zinasema kuwa kumeibuka sekeseke la aina yake juu ya hatima ya masalia waliofukuzwa chadema,

Hasira za wanaccm zimeibuka baada ya siri kuvuja kuwa katibu mwenezi wa ccm ndugu NAPE NNAUYE aliwaahidi masalia wa chadema kuwa ikiwa watafukuzwa hasa (Juliana Shonza), ccm itawapokea kwa sherehe kubwa na kulikuwa na makubaliano zaidi kuwa aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa BAVICHA ndugu Juliana Shonza atapatiwa nafasi ya UONGOZI ccm!

Taarifa hii imewachefua wanaccm wengi hasa vijana, huku wakisema wao wamejipanga mstari tangu 2010 kusubiri nafasi za ungozi, hivyo hawezi kutokea mtu tu tena asiyeijua ccm akajichomeka mbele ya mstari nakupata uongozi wa chama ghafla tu,
Wameapa kuwa hilo hawakubali kuliona likitendeka, heri chama kife kuliko kudhalauliana tu!

Katika kuthibitisha kuwa upepo ndani ya ccm ni mbaya, tangu juzi tarehe 07/01/2013 mawasiliano ya Shonza na Nape yamekuwa makubwa lakini kipengele cha kupewa uongozi ndani ya ccm pindi akijiunga tu ndicho kinakuwa kizito kwa Nape kumthibitishia Shonza!

Mfano: ujume ulionaswa wa Nape kwenda kwa Shonza unasema, "Juliana tunaandaa mapokezi mazito na tutazunguka na wewe nchi nzima"

Lakini kuthibitisha kuwa Shonza aliupata ujumbe huo anajibu,

"Mkuu nipo tayari, vp lakini nafasi ya uongozi? Fanya kama tulivyokubalia nafasi yoyote ambayo itaendelea kuniweka mbele ya jamii, mimi ni mwanasiasa bwana"


Muono wangu:

Kazi iliyofanywa na Chadema ni adhimu na murua, hakuna chama cha upinzani barani afrika kilichoweza kuchukua maamuzi magumu kama haya tena katika kipindi cha hatari kama hiki cha mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi,

Matokeo ya maamuzi haya yameisambaratisha ccm na sasa wanaweweseka tu kutafuta mbinu mbadala za kudhoofisha upinzani!i

Mimi kama mwanachadema ninaamini waliofukuzwa ni vidagaa tu, lakini mapapa wa uasi wapo ndani ya kamati kuu ya Chadema,

Naiomba ifanye maamuzi magumu zaidi ili kuizika kabisa ccm na vibaraka wao waliokuwa ndani ya Chadema!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema na wanyoofu wake!

Reply Report Post

hii ilitakiwa kuwa topic ya kujitegemea
 
Kwani nani alitegemea akubali kwamba wanashirikiana kuhujumu. You dont need to use your resources to deny facts meeen!!! Kuna mengine mengi tu ya kutolea maelezo. Kesho utamsikia Mwigulu naye anajibu!!! CC-M-ajamabazi bwana!!!
attachment.php


SIKU moja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), kudai CCM inashirikiana na baadhi ya viongozi wake kukisaliti chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amekanusha tuhuma hizo.

Nape alisema CCM haihusiki na mgogoro wowote ndani ya chama hicho, hivyo wanapaswa kumtafuta mchawi wao siyo kukilaumu chama chake. “Mchawi wanaye wenyewe ndani ya chama chao,hatuhusiki na lolote hivyo wanapaswa kujipanga na kuulizana kubaini tatizo linalowasumbua,” alisema.

Aliongeza kuwa CCM haina muda wa kuhujumu chama hicho, ila wana muda wa kutekeleza ilani za chama maeneo mbalimbali nchini.
Nape alisema kutokana na hali hiyo, CCM imejipanga kuhakikisha ahadi zinatekelezwa kwa vitendo, ikiwamo maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.Baadhi ya viongozi wa BAVICHA wanaodaiwa kushirikiana na CCM kudhooficha CHADEMA na
wengine walifukuzwa uanachama.

Miongoni mwa viongozi hao ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza,Habib Mchange, Mtera Mwampamba, Gwakisa Burton na Joseph Kasambala.
 
Ngoma ikivuma,ikavuma,ikavuma tena,vuvuu,vuvuu mwisho upasuka R.I.P CDM

Toka Burton sat shop.


Ndugu yangu siasa ni sayansi na si ushabiki tu wa kipropaganda.Hata mpira wa miguu ni sayansi pia wala si ushabiki tu , inahitaji utekelezwaji wake kuwa madhubuti.Hakuna chama kilichojipanga kimkakati kama CDM na ndo maana kinapendwa.Jiulize miaka kama kumi CDM ilikuwa na wabunge wanne leo ina wabunge 49.Huo ni mkakati mkubwa wa kupongezwa.Jamii pia inazidi kuiunga , angalia mikutano yake na maandamano utaona jinsi jamii inavyoiunga mkono CDM.mfano mzuri uchaguzi arumeru mashariki , NASARI ni kijana mdogo sana, alishinda kwa nguvu ya umma kumuunga mkono , hivyo kusema CDM itakufa hizo ni posho za nape.Nakukumbusha kikao tendaji cha BAVICHA kimewafukuza uanachama akina SHONZA kukiwa na ushahidi tosha , kiasi kwamba waliotajwa kama s.wasira na shibuda wametajwa.Si hao tu hata ccm imetajwa.CDM huwa haikurupuki , jifunze nawewe kutokurupuka CDM haiwezi kufa kwa mikakati isiyo na tija.NAPE kukanusha ni blabla anajua ukweli.
 
UMENIFURAHISHA, KWELI IVO NDO VITUKO VYA NEPI VUVUZELa

Ni kupoteza muda kuwasikiliza propagandist kama nape. Unaweza kuendelea kukisikiliza chama ambacho kimeua miiko ya uongozi na kuleta umasikini kwa watz. Jambo muhimu ccm na viongozi wake kutambua ni kwamba hata cdm ikifa leo haimaanishi ndio ccm kupendwa na wananchi....! Watz makini na wazalendo hawawezi kuwaambiwa porojo na uzushi wa ccm wakakupa nafasi ya kukusikiliza. Ni watz wale tu wanaofaidi ufisadi na hujuma zinazofanyika dhidi ya raslimali za nchi wanaounga mkono ulaghai wa ccm kwa raia wake masikini hasa kule vijijini pale chaguzi zinapokaribia.
 
Nilisha sema huko nyuma kwamba ccm hasa sekretarieti ni wepesi muno kwa kwa sababu ya kukosa viongozi wachambuzi wa hoja na matatizo yanayolikabili taifa badala yake umma wa watz umeshuhudia viongozi wakubwa hasa naibu katibu mkuu, mhe. Nchemba wakipiga propaganda na siasa za uzushi dhidi ya vyama vya upinzani. Nilishangaa siku moja kwenye Startv Nchemba akilidanganya taifa kwamba vyama vya upinzani ktk nchi jirani vilivyobahatika kushinda uchaguzi na kuunda serikali eti vilifanya hivyo mara moja na vyama vya zamani kuendelea kutawala. Huyu ni kiongozi mkuu lkn hana kumbukumbu kuwa alichokiongoza kenyatta kupata uhuru kenya ni historia, chama alichokiongoza kaunda kupata uhuru zambia ni historia, uganda, malawi, rwanda, drc congo nk nk. Ccm baada ya kuona kimekosa mvuto kwa raia ss kinakimbilia kununua wanachama wa vyama vya upinzani ili kuleta mgawanyiko, vyombo vya habari ss vinaimba kila siku utekelezaji wa ilani! Yote hii ni kutapatapa kwa ili kiungwe mkono na raia lkn it is too late to catch a moving train! Chama kilichoongoza nchi zaidi ya miaka 50 kinaangaika kujitangaza kila siku kuonesha nini kimefanya! Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Watz wa sasa wanaona wenyewe, serikali haina sababu ya kutumia pesa za walipa kodi kwa kulipia matangazo kwenye vyombo vya habari kutafuta umaarufu uliopotea. Hii ni tz wenye vijana wa.com wasiosubili serikali iwambie imefanya nini! Wanajua wenyewe kama imefanya na kwa ubora upi! Purukushani zote zinaonesha ccm sasa inatapatapa na kweli haiponi kwa mipango hii.
hapo mwanangu umesema kweli nakuunga mkono, uzushi utakaofuata wa wanamagamba ni kutangaza kwamba Chadema ni chama cha Wakristu ili kuwaadaa waislamu,au watasema kwamba ni chama cha wachaga.
 
hapo mwanangu umesema kweli nakuunga mkono, uzushi utakaofuata wa wanamagamba ni kutangaza kwamba Chadema ni chama cha Wakristu ili kuwaadaa waislamu,au watasema kwamba ni chama cha wachaga.

JAMAN TNAHITAJI KUJIAMIN, KWA SASA CHADEMA IS V STRONG, CCM WANAUMWA KWA NGUVU HII, WAFUATILIE KILA MWANACCM ANAHOMA INAYOITWA CHADEMA, KOKOTE WAWAPO CHADEMA NDO NENO LAO MDA WOTE, NA HAKUNA PIGO KUBWA TMEWAPA CCM KM KUWATIMUA AWA MASALIA WASALITI, NI USHUJAA WA AJABU UMEFANYWA NA BAVICHA, TUWAUNGE MKONO KWA MAAMUZ AYA, KWANI NAAMINI NAPE, WASIRA, MCHEMBA NA WENZAKE WALIWEKEZA PESA NYINGI KWA AWA WASALITI NA SASA WAMENG'OLEWa, RIL TMEWAPA PIGO KUBWA, WAT WE NEED NI MSHIKAMANO NA IMANI KWA VIONGOZ WETU, VIVA CHADEMA VIVA M4C
 
by Yericko Nyerere.
Taarifa za kuaminika toka ndani ya ccm zinasema kuwa kumeibuka sekeseke la aina yake juu ya hatima ya masalia waliofukuzwa chadema,

Hasira za wanaccm zimeibuka baada ya siri kuvuja kuwa katibu mwenezi wa ccm ndugu NAPE NNAUYE aliwaahidi masalia wa chadema kuwa ikiwa watafukuzwa hasa (Juliana Shonza), ccm itawapokea kwa sherehe kubwa na kulikuwa na makubaliano zaidi kuwa aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa BAVICHA ndugu Juliana Shonza atapatiwa nafasi ya UONGOZI ccm!
du! Mkuu kwann hii habar ucipatie page yake.naona inauzitowake wa kipekee
 
Mi naona ni kweli mchwawi wa CDM yuko CDM. masalia na PM7 wapo ndani ya CDM na siyo CCM.Kamati kuu ifanye maamuzi mazito dhidi ya uasi ndani ya chama.
 
Ccm haijui siasa na sasa wameshikwa pabaya kila wazimu wanaoujaribu kuvuruga Chadema jamaa wanawaumbua kwa kuzimilia mbali njama zao!!Tangu lini CCM ikafanya siasa bila kutisha kuhujumu upinzani kutisha watu kudharau raia wa Tz kudhalilisha watumishi wa Umma na ujinga mwingine mwingi tu?Siku za Ccm zimeisha na wananchi wanaanzisha ukombozi kupitia Chadema na Mungu wa haki aibariki chadema na kuilaani Ccm iendelee kuchakaa kila kuchao

Anasahau kwamba baadhi ya viongozi wa serkali ,ambao ni wana-CCM wamesikika mara kadhaa wakitangaza hadharani kuwa CDM itasambaratishwa kabla ya 2015 (WASSIRA).
Huo ni mkakati wao na hawawezi kamwe kukiri hilo.
 
attachment.php


siku moja baada ya baraza la vijana la chama cha demokrasia na maendeleo (bavicha), kudai ccm inashirikiana na baadhi ya viongozi wake kukisaliti chama hicho, katibu wa itikadi na uenezi, nape nnauye amekanusha tuhuma hizo.

Nape alisema ccm haihusiki na mgogoro wowote ndani ya chama hicho, hivyo wanapaswa kumtafuta mchawi wao siyo kukilaumu chama chake. “mchawi wanaye wenyewe ndani ya chama chao,hatuhusiki na lolote hivyo wanapaswa kujipanga na kuulizana kubaini tatizo linalowasumbua,” alisema.

Aliongeza kuwa ccm haina muda wa kuhujumu chama hicho, ila wana muda wa kutekeleza ilani za chama maeneo mbalimbali nchini.
Nape alisema kutokana na hali hiyo, ccm imejipanga kuhakikisha ahadi zinatekelezwa kwa vitendo, ikiwamo maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.baadhi ya viongozi wa bavicha wanaodaiwa kushirikiana na ccm kudhooficha chadema na
wengine walifukuzwa uanachama.

Miongoni mwa viongozi hao ni aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bavicha, juliana shonza,habib mchange, mtera mwampamba, gwakisa burton na joseph kasambala.

ukweli umeuficha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ATI BETLEHEM, FISADI, MWIZI PIA JAMBAZI MKUBWA WEWe
thibitisha kauli yako kwa ushahidi madhubuti.ukithibitisha nitakubaliana na wewe usipothibitisha ntakushauri uache fitna na ushabiki kwenye mambo ya msingi kwani fitna ni dhambi miongoni mwa madhambi mazito.
 
Ukweli, mimi nitashangaa sana kuona hapa jamvini watu wanamlaumu NAPE, WASIRA na huyo MGUU WA CHEMBA, hvi tunategemea wao wafanye nini? Siasa ni ushindani ingawa theorically ni ushindani wa hoja lakini kwenye grass root si hivyo bali ni ushindani wenye mbinu chafu tena wakati mwingine za kutisha sana. Ili kuweza kuongoza nchi ni lazima uwe na mifumo wenye nguvu na weledi, mfumo wa chama chetu cha CDM wa kuchukua wanachama hovyo hovyo kwa kudhani kuwa wingi wa wanachama ndio wingi wa kura ni UPUUZI unaokigharimu chama. Ni lazima CDM itengeneze mifumo yake ya kuendesha chama na kwa hali ilivyo sasa kwani mfumo wa CDM na vyama vyetu vingine ni 95% unafanana na CCM hivyo ni lahisi sana CCM kuwasambatisha kwa sababu wao wana uzoefu wa mfumo huo kwa zaidi ya miaka 50 lakini CDM hata miaka ishirini tu bado. Huwezi anzisha TIMU ukaiga mfumo wa uchezaji wa mwenzako mwenye uzoefu, wachezaji wenye vipaji, rasilimali, marefa, uwanja na uzoefu alafu eti utegemee USHINDI. Hiki ndicho kipindi cha kuangalia uwezo wa viongozi wetu, hatuwezi kupima uwezo wa viongozi kwa kuangalia uwezo wa kusema jukwaani tu, HAPANA ni pamoja na uwezo wa kuplan, kutengeneza mifumo bora ya uendeshaji wa chama kwa ujumla na jinsi ya kupambana na changamoto. Binafsi nachukia sana huu mfumo wa kila kitu kusubiri sijui kamati kuu ikae mara sijui kikao gani? HAPANA ni lazima mfumo uwape FURSA ya kutosha viongozi wetu watendaji kufanya kazi na vikao vya juu vibaki na kazi ya kubariki implementation tu. Haya mambo ya kamati kuu kuwa kama direct implementer ni mambo ya CCM. Ni lazima tufanye tathmini yamifumo yetu ya uendeshaji wa chama, tuangalie kanuni zetu vizuri na kuzitengeneza vizuri ziweze kuwabana wasaliti, Haiwezekani leo eti makam mwenyekiti wa BAVICHA anamkashifu kwa maandishi katibu mkuu wa chama tena hadharani pasipo kujificha eti unafanya uchunguzi wa tuhuma na kupeleka maazimio kwenye kikao na kuwapa fursa wajumbe ndio waamue adhabu tena kwa kupiga kura HUU ni utaratibu Mbovu sana na unatoa fursa kubwa ya RUSHWA, UONEVU na MAKUNDI ndani ya chama, kwa kesi kama hii kanuni tu zinapaswa kumuondoa then yeye ndie akakate rufaa huko kwenye vikao vya juu wakati akiwa pembeni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom