CCM yakanusha tuhuma za CHADEMA

CCM yakanusha tuhuma za CHADEMA

Uzuri wa Vita ni kuwa ukishajua Maadui zako, mbinu zao na nguvu zao basi Utashinda vita hiyo kwa kishindo.

Bravooooooooooo, makachero wa CDM
 
Kwa mtu ambae ana akili timamu kuishangilia ccm ni sawa na kufuraia kupata ngoma.we beza cdm moto wake utauona tu..fichadi we
 
Kwani mtu akisema kama alivyosema Nape ndio inatosha kusemwa kuwa Nape amekanusha? Mbona hakuna ushahidi kama ulioko kwenye taarifa ya BAVICHA? Kama ni hivyo,basi kukanusha ni rahisi sana...
 
Kwani mtu akisema kama alivyosema Nape ndio inatosha kusemwa kuwa Nape amekanusha? Mbona hakuna ushahidi kama ulioko kwenye taarifa ya BAVICHA? Kama ni hivyo,basi kukanusha ni rahisi sana...

Ukishasema taarifa fulani ni uwongo tayari umekanusha.
 
Hiyo ni kazi kwelikweli,kuwa kiongozi wa chama cha upinzani tanzania unahitajika uzalendo,ujasiri na kutokuwa na tamaa!
 
jamani humu pamekuwa hovyo siku hiziii!!Hakuna zaidi Ya Chadema na Ccm.Hamna hata mambo ya maana ya kujadili?Chadema wanachosema ni kweli,pesa zinarubuni watu na kusaliti Cdm.Ila mwisho upo tu,kuna watu maalum ambao hawahitaji mabadiliko kwa kuwa wanaishi paradiso.Wanang'angana kweli
 
Hivi ukijiuliza yaaanikabisa Nape ndani ya moyo wake anaona CCM ni chama safiii kabisa. yaaani tukiacha unafki au kuendekeza njaa zetu...Nchi hii bado tuna mwendo mrefu sana kufikia uzalendo wa kweli, kwasababu tumejiweka kununuliwa nunuliwa au kujikomba kwa mabwana wakubwa. hata kma unajua unachoongea ni uongo mkubwa na usaliti kwa kizazi cha watanzania wenye mapenzi mema ili mradi uvimbishe tumbo lako, ipo siku yaja wala si mbali watu watalia na kusaga meno
 
attachment.php


SIKU moja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), kudai CCM inashirikiana na baadhi ya viongozi wake kukisaliti chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amekanusha tuhuma hizo.

Nape alisema CCM haihusiki na mgogoro wowote ndani ya chama hicho, hivyo wanapaswa kumtafuta mchawi wao siyo kukilaumu chama chake. “Mchawi wanaye wenyewe ndani ya chama chao,hatuhusiki na lolote hivyo wanapaswa kujipanga na kuulizana kubaini tatizo linalowasumbua,” alisema.

Aliongeza kuwa CCM haina muda wa kuhujumu chama hicho, ila wana muda wa kutekeleza ilani za chama maeneo mbalimbali nchini.
Nape alisema kutokana na hali hiyo, CCM imejipanga kuhakikisha ahadi zinatekelezwa kwa vitendo, ikiwamo maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.Baadhi ya viongozi wa BAVICHA wanaodaiwa kushirikiana na CCM kudhooficha CHADEMA na
wengine walifukuzwa uanachama.

Miongoni mwa viongozi hao ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza,Habib Mchange, Mtera Mwampamba, Gwakisa Burton na Joseph Kasambala.

moja ya tuhuma mbaya kwa chama tawala. CCM inalazimika kujisafisha vizuri kwa tuhuma hizi maana issue ishakuwa public agenda!
 
Sijui hapa Kilaza Le Mutuz atakuja na ngonjera Ipi maana Jana kajitahidi kumsifu Nape na Wasira pia akadai nae anahusika kuisambaratisha CDM.Ndo maana Magamba wanamtosa Le Mutuz maana hajui kusoma Nyakati.
 
Unadhani CCM bila kuvihujumu vyama vya upinzani makini, ?mbona ingekuwa ishaondolewa kwenye orodha ya vyama tawala siku nyingi tu!!!
 
Musitafute mchawi cdm,musipo changa vzr karata zenu mtamwagikana.
 
Nape kibaraka wa udaku wa CCM!
Ningeridhika kama CCM ingekuwa inakanusha na kujigamba kwa 'matendo' mema.
Ipo siku nitamdhamini Nape kurekodi album ya umbea na kama atakubali nitamdhamini pia kufungua chuo cha "kuchonga" na kudandia mambo ya watu!!!
 
moja ya tuhuma mbaya kwa chama tawala. CCM inalazimika kujisafisha vizuri kwa tuhuma hizi maana issue ishakuwa public agenda!

Hata kifo cha Mwangosi na tuhuma Dr. Ulimboka si walikanusha? Asingekanusha Watanzania tungemshangaa maana siyo kanuni ya ccm.
 
Musitafute mchawi cdm,musipo changa vzr karata zenu mtamwagikana.
 
hata mwizi akipelekwa mahakamani huwa anajitetea kwamba hajaiba! ila tumshukuru Mungu wanafiki wasiowatakia mema watanzania wanaopigwa na mawimbi ya umaskini katikati ya lundo la utajiri wa raslimali, wanazidi kuanikwa hadharani. CDM baada ya kusafisha 'uchafu' ni vema wangewaambia watanzania nini kilikuwa kimetokea ktk chama maana migogoro hii iliyopandikizwa imekuwa ikiwa-shake vichwa!
 
Ushauri wa namna ya kutatua migogoro ndani ya chama (kama ipo) Hatuwezi kupatiwa na Nape wala CCM. They dont qualify kutoa ushairi.
 
Madhala ya kupeana vyeo kama embe, Nape hajui kabisa anachozungumza. Hayo ndio mambo yanayochangia kuleta uvunjifu wa amani. CCM nendeni kwa wananchi, tatueni matatizo yetu, shughulikia mafisadi na 2015 tutawalipa
 
Nnape...Tunajua mchawi wetu mnamjua...si mmemtumia nyie?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom