SIKU moja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), kudai CCM inashirikiana na baadhi ya viongozi wake kukisaliti chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amekanusha tuhuma hizo.
Nape alisema CCM haihusiki na mgogoro wowote ndani ya chama hicho, hivyo wanapaswa kumtafuta mchawi wao siyo kukilaumu chama chake. Mchawi wanaye wenyewe ndani ya chama chao,hatuhusiki na lolote hivyo wanapaswa kujipanga na kuulizana kubaini tatizo linalowasumbua, alisema.
Aliongeza kuwa CCM haina muda wa kuhujumu chama hicho, ila wana muda wa kutekeleza ilani za chama maeneo mbalimbali nchini.
Nape alisema kutokana na hali hiyo, CCM imejipanga kuhakikisha ahadi zinatekelezwa kwa vitendo, ikiwamo maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.Baadhi ya viongozi wa BAVICHA wanaodaiwa kushirikiana na CCM kudhooficha CHADEMA na
wengine walifukuzwa uanachama.
Miongoni mwa viongozi hao ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza,Habib Mchange, Mtera Mwampamba, Gwakisa Burton na Joseph Kasambala.
by Yericko Nyerere.
Taarifa za kuaminika toka ndani ya ccm zinasema kuwa kumeibuka sekeseke la aina yake juu ya hatima ya masalia waliofukuzwa chadema,
Hasira za wanaccm zimeibuka baada ya siri kuvuja kuwa katibu mwenezi wa ccm ndugu NAPE NNAUYE aliwaahidi masalia wa chadema kuwa ikiwa watafukuzwa hasa (Juliana Shonza), ccm itawapokea kwa sherehe kubwa na kulikuwa na makubaliano zaidi kuwa aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa BAVICHA ndugu Juliana Shonza atapatiwa nafasi ya UONGOZI ccm!
Taarifa hii imewachefua wanaccm wengi hasa vijana, huku wakisema wao wamejipanga mstari tangu 2010 kusubiri nafasi za ungozi, hivyo hawezi kutokea mtu tu tena asiyeijua ccm akajichomeka mbele ya mstari nakupata uongozi wa chama ghafla tu,
Wameapa kuwa hilo hawakubali kuliona likitendeka, heri chama kife kuliko kudhalauliana tu!
Katika kuthibitisha kuwa upepo ndani ya ccm ni mbaya, tangu juzi tarehe 07/01/2013 mawasiliano ya Shonza na Nape yamekuwa makubwa lakini kipengele cha kupewa uongozi ndani ya ccm pindi akijiunga tu ndicho kinakuwa kizito kwa Nape kumthibitishia Shonza!
Mfano: ujume ulionaswa wa Nape kwenda kwa Shonza unasema, "Juliana tunaandaa mapokezi mazito na tutazunguka na wewe nchi nzima"
Lakini kuthibitisha kuwa Shonza aliupata ujumbe huo anajibu,
"Mkuu nipo tayari, vp lakini nafasi ya uongozi? Fanya kama tulivyokubalia nafasi yoyote ambayo itaendelea kuniweka mbele ya jamii, mimi ni mwanasiasa bwana"
Muono wangu:
Kazi iliyofanywa na Chadema ni adhimu na murua, hakuna chama cha upinzani barani afrika kilichoweza kuchukua maamuzi magumu kama haya tena katika kipindi cha hatari kama hiki cha mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi,
Matokeo ya maamuzi haya yameisambaratisha ccm na sasa wanaweweseka tu kutafuta mbinu mbadala za kudhoofisha upinzani!i
Mimi kama mwanachadema ninaamini waliofukuzwa ni vidagaa tu, lakini mapapa wa uasi wapo ndani ya kamati kuu ya Chadema,
Naiomba ifanye maamuzi magumu zaidi ili kuizika kabisa ccm na vibaraka wao waliokuwa ndani ya Chadema!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema na wanyoofu wake!
Reply Report Post