CCM yaipeleka rasimu kwa wanachama wake

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
  • CCM YAONYESHA UKOMAVU
  • YAIPELEKA RASIMU KWA WANACHAMA WAKE
  • YAJIVUNIA IDADI KUBWA YA WANACHAMA MILIONI SITA ILIYOKUWA NAO

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa;

Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.
Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity
 
Attachments

  • 5.jpg
    5.jpg
    14 KB · Views: 135
  • 3.jpg
    3.jpg
    14.4 KB · Views: 116
  • 1.jpg
    1.jpg
    35.4 KB · Views: 104
Tayari CCM wameshaingia kwenye mtego hawawezi kujinasua sanasana wawaelekeze makada wao kupinga baadhi ya vifungu lakini si skeleton ya katiba inayobebwa na 1. serikali tatu, 2. tume huru ya uchaguzi, 3. mgombea binafsi, 4. rais kupunguziwa madaraka, 5. bunge kubariki wateule wa raisi na mwisho 6. matokeo ya rais kupingwa mahakamani, nawashauri wawe wapole.
 
CCM hawana lolote lile.
Eti ikajadiliwe na wanachama!!!
Wamekosa majibu na wanaogopa kivuli chao hao. Aibu tu zimewajaa.

CCM ilikuwa ama waikubali, waikatae au waikosoe hususani hoja ya Serikali tatu.
 
Ni vema kuwapa fulsa wananchi wachague mbichi na mbivu zao wenyewe.
 
CCM hawana lolote lile.
Eti ikajadiliwe na wanachama!!!
Wamekosa majibu na wanaogopa kivuli chao hao. Aibu tu zimewajaa.

CCM ilikuwa ama waikubali, waikatae au waikosoe hususani hoja ya Serikali tatu.
Mkuu mbona umechukia na unajaribu kuwachagulia majibu kwani upo kwenye vichwa vyao mkuu.
 
Wanachama wenyewe hawa hata wasiojuwa kusoma na kuandika wanajuwa hata maana ya rasimu ya katiba? thamani yao ni ubwabwa tu.

CCm2010.jpg 72207_1630755205240_1127403497_31793227_2798227_n.jpg
 
Swali la ufahamu: Kama ninaelewa vizuri, rasimu hii ilivyotolewa, ilizingatia maoni ya walio wengi wakati ya kupendekeza katiba mpya. Je mabaraza ya katiba yanayotakiwa kukaa na kuichambua rasimu hii, wanayo haki ipi kati ya hizi:
1. kuboresha rasimu iliyotolewa bila mkuongeza kipya, 2. Kuboresha, na au kufuta kabisa baadhi ya vipengele ndani ya rasimu na kuweka vipya, 3. kuboresha rasimu na kuongeza vipengele bila kuathiri mapendekezo makuu toka kwa wananchi? Kwa mfano, wananchi wengi wanataka serikali tatu (Tanganyika, Zanzibar na Muungano), Je mabaraza wanauwezo wa kukataa na kusema serikali mbili (Zanzibar na Muungano). Na kama mabaraza yatasema wanataka serikali mbili, je hii itakuwa kuwakilisha matakwa ya walio wengi? (wananchi waliopelekea rasimu kuandikwa Vs Mabaraza ya katiba)
 
  • CCM YAONYESHA UKOMAVU
  • YAIPELEKA RASIMU KWA WANACHAMA WAKE
  • YAJIVUNIA IDADI KUBWA YA WANACHAMA MILIONI SITA ILIYOKUWA NAO

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa;

Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.
Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity

Wanachama Mil 6 watoke wapi? Mimi mwenyewe na wale waliorudisha Kadi za CCM juma la jana kule visiwani bado anasema Mil 6??!! Nape na MAGAMBA wenzake waache kujitekenya wenyewe.

Kwa Tanzania ya leo hakuna Idadi kama hiyo kwa CCM. Labda kama wana Misukule.

Na hii ni moja ya mbinu zao za wizi wa kura kwa kujinasibu kwamba wana wanachama Mil 6 ili waje kutangaza kura za Mil 5 kwa kuaminisha waTanganyika kwamba nyingi zimetoka kwa wanachama wao.

MAGAMBA TUMEMISHTUKIA.
 
Ni vema kuwapa fulsa wananchi wachague mbichi na mbivu zao wenyewe.

Kwani wamesema wananchi au WANACHAMA WA CCM? Kwa vile mme- BINAFSISHA AKILI umeshindwa kutambua kwamba wananchi watapiga kura ya kuikubali au kuikataa rasimu ya Katiba Mpya muda utakapo wadia!! Au MAGAMBA mmesha sahau hilo ndio maana mnahamanika kiasi hicho?
 
Tayari CCM wameshaingia kwenye mtego hawawezi kujinasua sanasana wawaelekeze makada wao kupinga baadhi ya vifungu lakini si skeleton ya katiba inayobebwa na 1. serikali tatu, 2. tume huru ya uchaguzi, 3. mgombea binafsi, 4. rais kupunguziwa madaraka, 5. bunge kubariki wateule wa raisi na mwisho 6. matokeo ya rais kupingwa mahakamani, nawashauri wawe wapole.

Mkuu hawa magamaba wameogopa reaction ya wananchi kama wangetoka na tamko la kuipinga rasimu. Kitakachofanyika ni kwamba wanapeleka maagizo/maelekezo kwa wananchama wao ambao ndio wengi katika mabaraza ya katiba ya wilaya juu ya nini wanakikubali na nini hawakikubali.

We subiri tu mabaraza ya wilaya yaanze ndipo utashuhudia sarakasi za magamba.
 
bora upunguze stress za matatizo yanayokukabili kwa kuwaza kuisngusha ccm,mie nawaambia tuko hapa chadema 2015, mtaangkia pua

Nakushanga sana ww mtanzania usiye ipenda nchi yako hv unajua anayeitakia mabaya chadema huyo ni mtu mbaya sana na anaye itakia mabaya nchi yake
 
Akiongea katika kikao cha chama chao mjini Dodoma kuhusu kujadili rasimu ya katiba mpya amesema (sio nukuu rasmi) kuwa rasimu hii inahitaji mabadiliko kwani haijakidhi matakwa ya umma, kwamba michakato ya kuirekebisha rasimu bado inahitajika.
Msome hapa

Nape ndugu usiwe unakurupuka kama tulivyokueleza kwenye thread yako
 
Back
Top Bottom