CCM yaiga mikakati ya CHADEMA

CCM yaiga mikakati ya CHADEMA

Kata Funua sijapenda hilo neno.. ni la kihuni sana
 
CCM wamekubuhu kwa kupiga chabo darasani, hata M4C mlisema ni Magufuri for change kwahiyo ushahidi tunao ninyi ni mwendo wa kuiga tuu


Potezeaaaa basi... kwani kuiga mazuri tatizo liko wapi..? Yaliyopita si ndwele..!!
 
tuzungumze mambo ya msing muda mwengne kwan kadi ze ki electronic ni kitu cha ajabu au chadema ndio chama cha kwanza kua na hzo kadi
 
Atakae tekeleza hiyo ahadi akiwa wakwanza ndio atakaekuwa alijipanga kweli kuanzisha hiyo kitu mda utaongea
 
Hawana ubunifu wowote walianza kuiga Elimu Bure mpaka sasa wameshafeli hawana uwezo kugundua vitu bila kuiga walijua uraisi ni kupiga push up
 
Ubunifu wao ni kufuta sherehe za kitaifa na kuzirudisha mwaka mwingine na kufuta Matokeo ya uchaguzi yanayompa mpinzani ushindi tuu hawana jipya.
 
Nakumbuka kipindi cha kampeni walikopi had Ile logo ya M4C
 
Katika siasa ni KUIGA mambo MAZURI na kuacha yasiyokusaidia Inafanyika duniani kote. Wakati fulani katika UCHAGUZI wa Uingereza Labour Party walikuja na WAZO zuri sana lilohusu AFYA.
Likawaingia wapiga kura.
Conservative Party waliokuwa chama TAWALA waka HIJACK/WAKATEKA nyayra wazo la Wapinzani na kuwaambia wapiga kura "SISI ndo tunataka kufanya hivyo"
Hivyo WAKAWAPIKU. Na chama tawala kikashinda.
Hizo ni mbinu za SAYANSI ya KISIASA/POLITICAL SCIENCE!!
CCM hawajacheza faulo bali ni mbinu!
 
Nikionyeshwa hizo kadi za kielectronia za chadema natembea uchi....

Ccm WAMEKATA FUNUA
 
Halmashauri Kuu ya
CCM (NEC) iliyokutana leo imeadhimia
kupunguza wajumbe wa kamati hiyo
kutoka 34 hadi 24 pia wajumbe wa
Halmshauri Kuu kutoka 388 hadi 158.
Akizungumza mara baada ya kikao
hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye amewaambia
wanahabari leo mbali na hao pia
kamati kuu imeadhimia kupunguza
wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa
na wilaya sanjari na idadi ya vikao.
“Kamati Kuu imeazimia kufanya
uhakiki wa wanachama wake, tumeona
ipo haja ya kufanya uhakiki wa
wanachama wetu na jumuiya zake ili
kujua idadi sahihi ya wanachama wetu
kwa wakati huu kwa sababu kila
kukicha wanachama wanaongezeka na
kuna hisia wapo wengine ni hewa,”
alisema Nape
Aliongeza kuwa uhakiki huo utafanyika
kwa kutumia kadi kieletroniki na
kuachana na kadi za kawaida na
mchakato huo utakwenda sambamba
na kufuta kadi za cha jumuiya za
chama.
Mbali na Nape ambaye ni Waziri wa
Habari, Sanaa ,Utamuduni na Michezo,
amesema Mwenyekiti wa CCM Dk John
Magufuli amemteua Rodrick Mpogolo
kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu
Bara, awali ilikuwa ikishirikiriwa na
Rajabu Luhavi aliyeteuliwa kuwa
balozi.
Kamati hiyo imemteua Kanali Lubinga
Ngemela kuwa Katibu wa Halmshauri
Kuu ya Taifa ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa awali nafasi hiyo ilikuwa
ikishikiliwa na Dk Asha Rose Migiro
aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uingereza.
Hongera sana CCM well done.
 
Hebu ngoja namie nijaribu,

"HONGERA SSIEMU"

wadau nipo kwenye mafunzo ya kusifia sifia hapa lumumba nimeanza leo
 
Vyeo visivyotambulika kikatiba kufutwa,cheo cha Ole sendeka hakikuwepo kikatiba ndio maana kapewa ukuu wa mkoa kabla ya NEC kuanza ili asipate msongo wa mawazo!
 
Back
Top Bottom