CCM yaiga CHADEMA


M

Msharika

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
937
Likes
4
Points
35
M

Msharika

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
937 4 35
CCM yaiga CHADEMA
• Yawaengua Rostam, Aboud, Somaiya kamati ya ushindi

na Martin Malera


amka2.gif

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinajipanga kukusanya sh bilioni 40 za kampeni za uchaguzi mkuu kwa kutumia mbinu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuchangisha fedha wanachama wake kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms).
Ili kufanikisha lengo hili, CCM imeunda kamati ya watu 12 kuchangisha fedha hizo kwa ajili ya kufanikisha kampeni za kumwezesha Rais Jakaya Kikwete kushinda tena kiti hicho.
Mbali ya kuchangisha fedha kwa njia ya ujumbe mfupi, chama hicho kimesema kitakusanya mabilioni mengine ya fedha kupitia harambee ambazo nyingi zitaendeshwa na viongozi mbalimbali wa CCM.
Chanzo chetu kinadai kuwa hiyo ni sehemu ya mkakati wa CCM kuachana na pesa za watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, ambao walikiwezesha kushinda mwaka 2005.
Hata hivyo, chama hicho hakijasema kama kitakataa michango ya watuhumiwa hao, ambao baadhi yao ni wafadhili, wanachama na viongozi wake waandamizi.
Mwaka jana, CHADEMA ilitangaza kuanzisha mpango wa kuchangisha fedha kutoka kwa wanachama wake kwa kutumia ujumbe wa simu kwa ajili ya kampeni zake za uchaguzi.
Hii ni mara ya tatu CCM wananakili mawazo ya CHADEMA na kuyafanyia kazi.
Mwaka 2005 katika kampeni za uchaguzi mkuu, mgombea urais wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alihutubia wananchi wa Dodoma Mjini, akasema iwapo angechaguliwa kuwa rais angeufanya Dodoma kuwa mkoa wa elimu kwa kujenga vyuo vikuu, ambavyo vingesaidia kukuza uchumi wake.
Mara baada ya uchaguzi mkuu, Rais Jakaya Kikwete aliamua kuanzisha Chuo Kikuu cha Dodoma; wazo ambalo amewahi kujisifia kuwa ni lake binafsi kwa kuwa halikuwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mwaka huo huo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya machimbo ya Mererani, mkoani Manyara, Mbowe pia alisema kuwa iwapo CHADEMA ingeingia Ikulu, ingepitia upya mikataba yote ya madini kwa kuwa iliyopo ni ya kinyonyaji; inawapendelea wageni na makundi ya watawala.
Miaka miwili baada ya uchaguzi, Rais Kikwete aliunda kamati ya kuchunguza mikataba ya madini na kupendekeza namna ya kuipitia upya.
Kamati hiyo iliongozwa na Jaji Mark Bomani, ikiwa wa wajumbe; Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA).
Wajumbe wengine walikuwa ni David Tarimo, Maria Kejo, Salome Makange, Mugisha Kamugisha, Edward Kihundwa na Idd Simba.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM, vinasema kamati mpya ya kumwezesha JK ashinde, ina wajumbe 12, na inaongozwa na Mhazini wa CCM Taifa, Amos Makala, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) ya CCM.
Wajumbe wengine ni Ramadhani Madabida, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Mary Nagu, Waziri wa Uchumi na Fedha, Mustafa Mkulo, Zakia Meghji, Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Judice Tumbau na wengine.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Kapteni Mstaafu John Chiligati, amelithibitishia gazeti hili kuwapo kwa kamati hiyo.
Hata hivyo, alisema Makala ndiye mwenye taarifa zaidi juu ya kamati na wajumbe wa bodi.
“Mimi niko Loliondo, lakini mambo yote kuhusu kamati yetu muulize Makala, yeye anawajua wajumbe wake na wanajua watakusanya kiasi gani na mikakati yao ya kukusanya fedha na mambo mengine yote,” alisema Chiligati.
Makala hakupatikana jana kuzungumzia kamati hiyo. Simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokewa.
Kamati hii iliyoteuliwa na NEC, inaifuta rasmi kamati ya awali iliyokuwa imeteuliwa na Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, ambayo ilikuwa inaundwa na wajumbe watano: Rostam Abdulrasul Aziz, Tanil Somaiya, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi, Mohammed Dewji na Aziz Aboud.
Habari kutoka ndani ya kikao cha NEC kilichomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, zilisema kuwa CCM imeamua kuachana na kamati ya awali kwa sababu wajumbe wake wanaipa sura ya kifisadi kwa sababu wamekumbwa na tuhuma nyingi zinazokichafua chama hicho.
Kwa mujibu wa habari hizo, chini ya mpango huo, CCM inayodai kuwa na wanachama wanaokadiriwa kufikia milioni nne, wanatarajia kupata zaidi ya sh bilioni 40 kama kila mwanachama atachangia sh 1,000.
Hata hivyo, baadhi ya wana CCM wanasema kuwa wajumbe hao watano walioondolewa ndio wanaotarajiwa kuwa wachangiaji wakuu wa kampeni hizo. Na baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanasema CCM haiwezi kuwaepuka hao kwa sababu wana uwezo mkubwa wa kifedha ambao chama hicho kinauhitaji.
Wanadai kwamba ingawa CCM inasema itachangiwa na wanachama wake, wengi wa wanachama hao ni watu hohehahe, ambao wenyewe wanahitaji kuchangiwa, na baadhi yao wanatarajia kuutumia mwaka wa uchaguzi kama fursa ya kuchuma, si kuchangia chama ambacho kwa asilimia kubwa kinaendeshwa na matajiri wakubwa wazalendo na wenye asili ya Kiasia.
Wakati Rostam amekuwa akitajwa katika tuhuma za ukwapuaji wa sh bilioni 40 kupitia Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited na kutajwa pia katika kashfa ya Richmond/Dowans, Karamagi anahusishwa na mkataba mbovu wa madini wa Buzwagi uliosainiwa nje ya nchi na katika mazingira ya kutatanisha.
Kagoda ilisajiliwa Septemba 29, 2005 na ndani ya siku tano baada ya kusajiliwa ikachotewa sh bilioni 40 kutoka BoT.
Mabilioni haya ya shilingi, au sehemu yake kubwa yanadaiwa kutumiwa na CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Somaiya anatajwa katika kashfa ya ununuzi wa rada ya kijeshi kutoka Kampuni ya BAE System ya Uingereza ambako wahusika wanadaiwa “kulainisha” mikono ya watendaji serikalini ili inunuliwe kwa bei ya juu kuliko gharama yake ya kawaida.
Makamba amekuwa akikanusha bila mafanikio tuhuma kwamba ufisadi ndani ya BoT ndiyo ulikuwa nguvu kuu ya kifedha katika chama chake. Makala alisema CCM imefikia uamuzi huo ili kutoa fursa kwa wanachama wake kupata nafasi ya kukichangia na kuondokana na kutegemea fedha za wafadhili ambazo nyingine ni za ufisadi. Kwa muda wa miaka minne na ushei sasa, CCM imeshindwa kujinausa katika tuhuma kwamba kampeni zake za mwaka 2005 zilifanikishwa na pesa za wizi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,506
Likes
4,879
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,506 4,879 280
wataendelea kunakili tu na kufanya vizuri kabisa, Chadema watageuka kuwa consultant wa political parties!

usisahau pia vyama hivi vinaigana kwenye mambo mengi tu.
 
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
21
Points
135
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 21 135
CHADEMA pia imeiga CCM namna ya kuahirisha matatizo yake badala ya kutatua. Martin mbona hili umesahau?
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,506
Likes
4,879
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,506 4,879 280
CHADEMA pia imeiga CCM namna ya kuahirisha matatizo yake badala ya kutatua. Martin mbona hili umesahau?
Nimesema, we vichunguze hivi vyama, vinafanana sana, yaani inakuwa vile alternative za Nyerere ambazo hakuzitekeleza CCM ziko Chadema, ila root na kila kitu ni kile kile!

maneno mengi!
 
Shalom

Shalom

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2007
Messages
1,315
Likes
8
Points
135
Shalom

Shalom

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2007
1,315 8 135
wataendelea kunakili tu na kufanya vizuri kabisa, Chadema watageuka kuwa consultant wa political parties!

usisahau pia vyama hivi vinaigana kwenye mambo mengi tu.
Waberoya wewe vaa tu shati la kijani mzee, sisi tutafika tu Mungu Mkubwa
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Hili la UDOM halina hata ubishi Nakumbuka sana Wakati Mbowe anahutubia na kuonyesha na kusema kuwa kuna mji upo Netherlands ambao hauna rasimimali za kutosha kama Dodoma lakini ni vituo vya elimu. Hongera CHADEMA na CCM endeleeni kuiga yote mazuri
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,506
Likes
4,879
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,506 4,879 280
Waberoya wewe vaa tu shati la kijani mzee, sisi tutafika tu Mungu Mkubwa
Mimi siyo mtu wa kijani mkuu, sina chama natafuta lakini katika hivyo CCM sitakuja kuingia.

Mungu Mkubwa? mbona mnampa kazi nzito, huoni a adui yako wa kisiasa atasema hivyo hivyo? huoni akina RA na tuhuma zote wanatoa misaada makanisani?
 
M

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Messages
7,373
Likes
1,524
Points
280
M

MkamaP

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2007
7,373 1,524 280
Mimi siyo mtu wa kijani mkuu, sina chama natafuta lakini katika hivyo CCM sitakuja kuingia.

Mungu Mkubwa? mbona mnampa kazi nzito, huoni a adui yako wa kisiasa atasema hivyo hivyo? huoni akina RA na tuhuma zote wanatoa misaada makanisani?
Mkuu
kuna nyimbo nzuri sana kama hapa kama una spika hebu nakuomba uusikilize.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=SXQkCE5p81Y&feature=related"]YouTube- naona pendo[/ame]
 
Injinia

Injinia

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
850
Likes
4
Points
0
Injinia

Injinia

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
850 4 0
Mh, wanaCCM mkichangia hivyo vi 500 vyenu mmeliwa!
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,506
Likes
4,879
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,506 4,879 280
Mkuu
kuna nyimbo nzuri sana kama hapa kama una spika hebu nakuomba uusikilize.
YouTube- naona pendo
Wow!

Haleluyah ni Pendo kubwa, eeh! Mungu nakuomba nijaze pendo lako tele

Na sote tuwe na umoja katika Pendo la Mwokozi..

Huyu dada nilichelewa kidogo tu nilikuwa nimwoe! duh! umenikumbusha mbali.
Ukiingiza mambo ya Mungu kwenye siasa , basi utapata jibu CCM waendelee kutawala tu, na tuwasamehe yoote waliyotukosea!
 
M

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Messages
7,373
Likes
1,524
Points
280
M

MkamaP

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2007
7,373 1,524 280
Wow!

Haleluyah ni Pendo kubwa, eeh! Mungu nakuomba nijaze pendo lako tele

Na sote tuwe na umoja katika Pendo la Mwokozi..

Huyu dada nilichelewa kidogo tu nilikuwa nimwoe! duh! umenikumbusha mbali.
Ukiingiza mambo ya Mungu kwenye siasa , basi utapata jibu CCM waendelee kutawala tu, na tuwasamehe yoote waliyotukosea!
Na mwingine huyu hapa
Hawa wananikonga kweli, kwanza maudhuhi na kila kitu.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=NJUTExb7nsc&NR=1"]YouTube- Ahadi Zake[/ame]
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Dawa kama Wananchi wanataka CCM waendelee kuiga mengi toka CHADEMA ni kuacha kuwachagua CCM na kuwachagua CHADEMA na ndio wanaweza kuisaidia Serikali kufanya vizuri lakini ile sera ya mafiga matatu ni ya kuacha nayo
 
Kilasara

Kilasara

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2008
Messages
578
Likes
8
Points
0
Kilasara

Kilasara

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2008
578 8 0
Kama mobile phone yako ni ZAIN au VODA peleka message "CHADEMA" to No. 15710 na kuchangia Shilingi 350 kwa Chama chenye ubunifu na kinachoonyesha dalili za kuwa na viongozi wazalendo, waadilifu na wanaojali kwa dhati matatizo ya wanyonge.
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Waberoya wewe vaa tu shati la kijani mzee, sisi tutafika tu Mungu Mkubwa
Avae mara ngapi yeye kila chama ni kibaya atachagua sana dunia ndiyo hii hii na vyama ndivyo hivi hivi namshauri asubiri sayari ya Mars nasikia wamegundua maji huko labda atakuta chama perfect anachokitaka sisi tutajiunga na hivi hivi vyetu kama mtu unashindwa kupata chama angalau kimoja kati ya 20 lazima utakuwa na sababu au....
 
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2008
Messages
421
Likes
8
Points
0
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2008
421 8 0
Kama mobile phone yako ni ZAIN au VODA peleka message "CHADEMA" to No. 15710 na kuchangia Shilingi 350 kwa Chama chenye ubunifu na kinachoonyesha dalili za kuwa na viongozi wazalendo, waadilifu na wanaojali kwa dhati matatizo ya wanyonge.

Hapana siwezi kuchangia NGO hata siku moja labda CCJ wakija vizuri naweza kuwachangia lakini CHADEMA hapana tena nawaambia wanaochngia wameliwa bora mkatoe fedha zeni kanisani na misikitini.
 

Forum statistics

Threads 1,237,174
Members 475,465
Posts 29,280,272