CCM yafumaniwa

CCM yafumaniwa

hoja za upinzani nyingi huwa zinafanyiwa utafiti wa kina kabla hazijaletwa hadharani,hili swali limeanza kupigiwa kelele mda sana,na hata cuf nao wamelisemea sana,lakini warioba kaziba pamba masikioni,ubinafsi na wa viongozi wetu hasa wa chama tawala ndiyo umetufikisha hapa tulipo,kwa kuamini wao wako perfect kwa kila kitu,kuna watu wanaweka utaifa mbele kimuonekano ila kimatendo ni tofauti kabisa.

katiba hii haikutakiwa kuingiliwa na chama chochote cha siasa,na wajumbe wa tume hii pia walitakiwa wawe huru na wengi watoka kwenye taasisi kama jukwaa la katiba,ama asasi za kiraia na sio vyama vya siasa,vyama vingetoa wawakilishi tu,lkn leo kumejaa waasisi wa Tanu na badae ccm unadhani tutakuw na katiba nzuri plus tume huru ya uchaguzi?<tutaitamani katiba ya kenya mpk kufa kwetu ila daima hatutafikia ubora wake labda kizazi cha watoto wetu not us>
Mwigulu,asha rose migiro,nape,kinana,mnakoipeleka nchi hii siko mnakodhani nyie,kizazi chenu kitawalaani sana kwani mawazo yenu hayawezi kuiwakilisha Tanziania nzima na wala hayataendana na kasi ya ukuwaji wa ubongo wa kazazi kijacho
Pamoja sana mkuu. mimi roho imeniuma sana, haswa vile nilijenga imani yangu kwa warioba, kumbe nilijidanganya. mzee ni hovyo kabisa
 
Hakuna sababu ya kupoteza mabilion mengi namna hiyo kwa kutengeneza katiba ya kipuuzi. ushauri wangu ni, Tuchukue kaiba ya kenya iwe pia ya kwetu. couse nimeisoma imenifurahisha mno. ipo kwa maslahi ya taifa kiukweli na siyo kwa maslahi ya genge la majambazi wachache
 
Wkati watu wako busy na mchakato wa katiba, CHADEMA ilkuwa busy na maandamano! Mnategemea nini?

Well, katiba haizungumzii CCM bali mustakbali wa wananchi wote na sio kwamba wakishaamua hao wajumbe wa mabaraza ya katiba basi katiba inapitishwa kuwa sheria.

Katiba ni mchakato na mwisho wa siku itakuja tena kwetu kwa ajili ya kuipigia kura. Ni mapema mno kukata tamaa kwamba tuliyoyataka hayatakuwemo.

Hao wajumbe wa CCM walichofanikiwa kupata ni ajira ya muda tu si vinginevyo.
Wee bocho acha kujifanya kipofu wakati unaona,na hata ukijifnya huoni wenzio wataon kwa niaba yako!! Hata mulipojifanya hamuoni umuhimu wa katiba yenyewe mukidai hii ya sasa inatosha kuna wenye macho waliowasaidia kuona sio tu matundu,bali mapango yaliyokuwa kwenye katiba hii,mukaona aibu,mukainamisha vichwa,mukakubali shingo upande kwa masharti meengi,sasa tena unajifanya huoni monopolism iliyokitwa na chama chako kwenye mchakato huu!!anyway Hata ujifanye hujui naamini unajua na unaomba mungu wengine wasijue.
 
New World Order inaitafuna Tanzania...tutakoma mbona
 
Wee bocho acha kujifanya kipofu wakati unaona,na hata ukijifnya huoni wenzio wataon kwa niaba yako!! Hata mulipojifanya hamuoni umuhimu wa katiba yenyewe mukidai hii ya sasa inatosha kuna wenye macho waliowasaidia kuona sio tu matundu,bali mapango yaliyokuwa kwenye katiba hii,mukaona aibu,mukainamisha vichwa,mukakubali shingo upande kwa masharti meengi,sasa tena unajifanya huoni monopolism iliyokitwa na chama chako kwenye mchakato huu!!anyway Hata ujifanye hujui naamini unajua na unaomba mungu wengine wasijue.

CHADEMA wakati mchakato wa mabadiliko ya katiba ukiendelea, wenyewe walikuwa wanaandaa maandamano!

Ningekuwa na nafasi ya kushinikiza hili, basi kuna mmoja kati ya viongozi wa CHADEMA alipaswa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia vema mchakato mzima wa katiba.

Tegemeo la wanachama wenu ni kuwa CHADEMA ingesimama kidete katika kila hatua kuhakikisha wananchi wanapata hichi ambacho mnakisimamia.

Lakini kutokana na kukosa umakina, CHADEMA ikadakia non issues wananchi wakiwa hawajui wajipange vipi mpaka mabaraza yakaundwa ndio mnashtuka shuka ilhali kumekucha!

Learn a lesson next time.

Bahati yenu nzuri ni kwamba kama katiba haikuwapa wazanzibari mamlaka kamili basi haipiti. Ila wakiweka tu hicho kipengele, aa basi inapita Tanzania bara na ZNZ bila kupingwa.
 
CCM ni chama cha ajabu....ndio maana hata kagame anaweza kutuonyesha show game ya ukweli...
 
Sasa msingi wa katiba mpya ni nini, ili tujuwe kama ni hayo mabaraza? Sisi nyumba kwetu hatuanzi na msingi, tunaanza na Plan ya jengo lenyewe kwanza.

Utaanzaje kujenga nyumba kwa kuanza msingi ilhali hujuwi kama bajeti inatosha kwa aina ya jengo unalolitaka? GT vipi?

Ukweli unabaki palepale kuwa unapojenga nyumba msingi ndio huanza kujengwa
Hoja yako dhaifu.
 
Ukweli unabaki palepale kuwa unapojenga nyumba msingi ndio huanza kujengwa
Hoja yako dhaifu.

Hiyo mimi ndio fani yangu, ujenzi. Nyumba haianzi na msingi ila inaanza plan ya kujenga! Nenda ukaulize wenye fani zao!

GT
 
sasa mkuu ikipita hiyo katiba mbovu wewe binafsi utakuwa unanufaika nini?



CHADEMA wakati mchakato wa mabadiliko ya katiba ukiendelea, wenyewe walikuwa wanaandaa maandamano!

Ningekuwa na nafasi ya kushinikiza hili, basi kuna mmoja kati ya viongozi wa CHADEMA alipaswa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia vema mchakato mzima wa katiba.

Tegemeo la wanachama wenu ni kuwa CHADEMA ingesimama kidete katika kila hatua kuhakikisha wananchi wanapata hichi ambacho mnakisimamia.

Lakini kutokana na kukosa umakina, CHADEMA ikadakia non issues wananchi wakiwa hawajui wajipange vipi mpaka mabaraza yakaundwa ndio mnashtuka shuka ilhali kumekucha!

Learn a lesson next time.

Bahati yenu nzuri ni kwamba kama katiba haikuwapa wazanzibari mamlaka kamili basi haipiti. Ila wakiweka tu hicho kipengele, aa basi inapita Tanzania bara na ZNZ bila kupingwa.
 
sasa mkuu ikipita hiyo katiba mbovu wewe binafsi utakuwa unanufaika nini?

Katiba itakayopita haiwezi kuwa mbovu. Matumaini yangu ni kuwa itakuwa bora kuliko ya sasa ambayo kimsingi ni hatua muhimu sana kwa ustawi wa taifa.
 
Waraka wa Pongezi toka kwa Kamati Kuu ya CCM kuelekezwa kwa Watendaji wa chama hicho umenaswa. Waraka huo unapongeza kufikiwa malengo ya kumiliki Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.


Katika Mabaraza hayo Tanzania nzima CCM ina wajumbe asilimia 90. Waraka husika una jedwali linaloonesha mikoa,idadi ya wajumbe wa CCM,vyama vya upinzani na wale wasio na vyama. Alipoulizwa Mwigulu juu ya waraka huo,aliruka bila kutoa hoja ya msingi.


Waraka huu unathibitisha tuhuma zilizotolewa na CHADEMA kupitia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria,Tundu A. Lissu(Mb) pamoja na Jukwaa la Katiba linaloongozwa na Bwana Deus Kibamba kwamba CCM imeuingilia na kuuharibu mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya hasa katika uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba.


Chanzo: Gazeti la Mawio la Alhamisi tarehe 30/5/2013;Toleo Nambari 0045


Mimi: Waungwana wa Tanzania, hapa patapatikana Katiba ya nchi au ya chama tawala?


Cc Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Ritz Sumu MwanaDiwani et al


Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Tatizo lenu CHADEMA mnapenda sana kulia kulia, jata kwenye swala la mchakato wa katiba bado mnalia lia utafikiri mmeshikiwa bunduki kichwani kuwepo kwenye mchakato wakati ni ninyi wenyewe mlienda kugombea kwenye mabaraza ya katika yanayoratibiwa na tume na mkapigwa chini.

Napenda mfahamu kuwa, mabaraza ya katiba yako ya aina mbili kama mwongozi unavyobainisha na kusema,
Kifungu cha 18 (6) kinaeleza aina nyingine ya Mabaraza ya Katiba kwa kueleza kuwa Tume inaweza kuruhusu Asasi, Taasisi au Makundi ya Watu kuwasilisha maoni yao kuhusu Rasimu ya Katiba.

Kwa Msingi huo, Tume imeamua kuwa Mabaraza ya Katiba yatakuwa katika makundi mawili yafuatayo:-

1.1 Mabaraza ambayo Tume itayasimamia na kukusanya Maoni (Mabaraza ya Katiba ya Wilaya – Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa).

1.2 Mabaraza ambayo Tume haitayasimamia. Mabaraza hayo yatajisimamia yenyewe na kukusanya maoni yatakayowasilishwa kwenye Tume kwa mujibu wa maelekezo. (Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taa

Katika mabaraza ambayo tume haitasimamia uteuzi wake, yatakuwa na wajumbe kutoka makundi yafuatayo.
1. Jumuiya ya kidini.
2. Chama cha siasa.
3. Asasi ya kiraia.
4. Taasisi ya elimu ya juu.
5. Chama cha wafanyakazi.
6. Chama cha wakulima.
7. Chama cha wafugaji.
8. Chama cha Wanahabari.
9. Mabaraza ya Watoto, Vijana na Wazee.
10.Kundi au makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kama Sheria
inavyoelekeza, na
11. Kundi au makundi ya watu wenye mahitaji maalum katika jamii.

Sasa hizi kelele za kudai CCM inataka kutengeneza katiba ya nchi kama ya CCM zinatoka wapi kama siyo mwendelezo wa malalamiko yenu yasiyoisha wakati huo huo, mnajidai kama ninyi mko smart zaidi ya CCM. Kama mko smart zaidi ya CCM , kwa nini hamuishi kulalamika lalamika. It's high time to wake up to the reality and get real or get lost.
 
KITAELEWEKA TU KAKA,KWANI KIBAKI KATIBA YAKE SI ILIPINGWA NA ODM(KUMBUKA CHUNGWA) NA NDIZI so tusubiri madudu yao the itapingwa tu mimi nawakubali sana zanzibar hakuna cha cuf wala CCM wananchi wako pamoja so hata BARA INAWEZEKANA
 
Kama Mawio hawana certified copy au original ya walaka huo ....aisee wanamfuata Mwanahalisi muda si mrefu.
 
Hivi hao CCM tu ndiyo Wataipigia kura ya NDIYO au HAPANA hiyo katiba mpya, mbona wanajidanganya!

Au matumanini yao yapo kwenye NEC kwamba itachakachua KURA YA MAONI.

Kama rasmu ya katiba mpya haitakidhi maoni ya WATANZANIA tutapiga kura ya HAPANA. CCM msijidanganye, hurumieni kodi zetu mnazotumia sasa kutengeneza hiyo katiba ya ki-CCM, CCM

Mpaka hapo ushakosea njia, rudi barabarani. Kama hali halisi iliripotiwa na baadhi ya wadau lakini Warioba akasema hakuna kanuni zilizovunjwa nae anaendelea na mchakato kama kawaida, Hivi unadhani hizo kura za wananchi zitasomwa zile watakazopiga au zitatangazwa zile wanazotaka wakubwa!!!!!!! Jiulize mara kadhaa kama matokeo ya kidato cha nne yanayumbishwa hivi pamoja na watu kibao kupigia kelele je Hizo kura ambazo zitakuwa zinaonekana kwa NEC na ndio Kichwa cha CCM Unategemea chochote humo. Itakayoandikwa hata kama itakuwa mbovu kuliko zilizowahi kutungwa ndio itakayopita. Hata tusisumbue vichwa sana kwa ndoto za mchana.
 
Wkati watu wako busy na mchakato wa katiba, CHADEMA ilkuwa busy na maandamano! Mnategemea nini?

Well, katiba haizungumzii CCM bali mustakbali wa wananchi wote na sio kwamba wakishaamua hao wajumbe wa mabaraza ya katiba basi katiba inapitishwa kuwa sheria.

Katiba ni mchakato na mwisho wa siku itakuja tena kwetu kwa ajili ya kuipigia kura. Ni mapema mno kukata tamaa kwamba tuliyoyataka hayatakuwemo.

Hao wajumbe wa CCM walichofanikiwa kupata ni ajira ya muda tu si vinginevyo.

Mkuu Mimi nitofautiane na sababu ya chadema kuwa kwenye mchakato wa katiba.tukubali tu kuwa ccm wameamua kufubaisha katiba.
 
Back
Top Bottom