CCM yafumaniwa

CCM yafumaniwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Waraka wa Pongezi toka kwa Kamati Kuu ya CCM kuelekezwa kwa Watendaji wa chama hicho umenaswa. Waraka huo unapongeza kufikiwa malengo ya kumiliki Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Katika Mabaraza hayo Tanzania nzima CCM ina wajumbe asilimia 90. Waraka husika una jedwali linaloonesha mikoa,idadi ya wajumbe wa CCM,vyama vya upinzani na wale wasio na vyama. Alipoulizwa Mwigulu juu ya waraka huo,aliruka bila kutoa hoja ya msingi.

Waraka huu unathibitisha tuhuma zilizotolewa na CHADEMA kupitia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria,Tundu A. Lissu(Mb) pamoja na Jukwaa la Katiba linaloongozwa na Bwana Deus Kibamba kwamba CCM imeuingilia na kuuharibu mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya hasa katika uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba.

Chanzo: Gazeti la Mawio la Alhamisi tarehe 30/5/2013;Toleo Nambari 0045

Mimi: Waungwana wa Tanzania, hapa patapatikana Katiba ya nchi au ya chama tawala?

Cc Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Ritz Sumu MwanaDiwani et al

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
ccm bwana sasa kwa nini kupoteza mamilioni kwa kitu ambacho hakiisaidii nchi , kama hawakuwa tayari kwa mchakato wa katiba mpya si wangekaa kimya tu kama hapo awali mangapi wameyafumbia macho na wananchi wameyapigia kelele na wamekaa kimya.
 
Hivi hao CCM tu ndiyo Wataipigia kura ya NDIYO au HAPANA hiyo katiba mpya, mbona wanajidanganya!

Au matumanini yao yapo kwenye NEC kwamba itachakachua KURA YA MAONI.

Kama rasmu ya katiba mpya haitakidhi maoni ya WATANZANIA tutapiga kura ya HAPANA. CCM msijidanganye, hurumieni kodi zetu mnazotumia sasa kutengeneza hiyo katiba ya ki-CCM, CCM
 
Ni katiba ya CCM inasikitisha kuona tendo kubwa kama hilo linafanywa la kisiasa halafu Warioba anatunga uongo eti wananchi munaweza kuunda mabaraza yenu munavyotaka,huu ni uongo mkubwa tutajuaje watachukua mawazo ya hao wengine ndio maana hata rasimu wanaogopa kuitoa baada ya kelele za wananchi,chadema na jukwaa la katiba
 
sisi tunacho taka kwenye katiba hyo tume huru ya uchaguzi na kipengele cha kupinga matokeo ya uchaguzi ya uraisi mahakamani hivyo vingine tukiingia madarakani chadema wataitisha mchakato wa katiba mpya
 
Waraka wa Pongezi toka kwa Kamati Kuu ya CCM kuelekezwa kwa Watendaji wa chama hicho umenaswa. Waraka huo unapongeza kufikiwa malengo ya kumiliki Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Katika Mabaraza hayo Tanzania nzima CCM ina wajumbe asilimia 90. Waraka husika una jedwali linaloonesha mikoa,idadi ya wajumbe wa CCM,vyama vya upinzani na wale wasio na vyama. Alipoulizwa Mwigulu juu ya waraka huo,aliruka bila kutoa hoja ya msingi.

Waraka huu unathibitisha tuhuma zilizotolewa na CHADEMA kupitia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria,Tundu A. Lissu(Mb) pamoja na Jukwaa la Katiba linaloongozwa na Bwana Deus Kibamba kwamba CCM imeuingilia na kuuharibu mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya hasa katika uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba.

Chanzo: Gazeti la Mawio la Alhamisi tarehe 30/5/2013;Toleo Nambari 0045

Mimi: Waungwana wa Tanzania, hapa patapatikana Katiba ya nchi au ya chama tawala?

Cc Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Ritz Sumu MwanaDiwani et al

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Gazeti lenyewe mwanahalisi ambalo ni uchochezi na uzushi.
 
hivi kuwa ccm kunaendana vipi na kupoteza uwezo wa kufikiri kiusahihi!?
Kwani hiyo katiba wanadhani inaweza kusimamia maslahi ya mafisadi, wazembe kwa muda gani ...hapa tuifikirie Tanzania ya miaka 150+ ijayo ambapo kiukweli kinachoitwa adui huenda kisiwe adui, rafiki huenda asiwe rafiki, mali leo huenda kisiwe mali wakati huo nk lakini nchi (sio taifa) ya Tanzania litakuwepo!
 
Hivi hao CCM tu ndiyo Wataipigia kura ya NDIYO au HAPANA hiyo katiba mpya, mbona wanajidanganya!

Au matumanini yao yapo kwenye NEC kwamba itachakachua KURA YA MAONI.

Kama rasmu ya katiba mpya haitakidhi maoni ya WATANZANIA tutapiga kura ya HAPANA. CCM msijidanganye, hurumieni kodi zetu mnazotumia sasa kutengeneza hiyo katiba ya ki-CCM, CCM
Mkuu mbona unaongea ubwabwa mkuu hayo unayosema unauhakika nayo.
 
Mawio nalikubali sana yaani siku hizi linakata kiu yangu ya habari za uchunguzi
 
Lawama zangu nazipeleka kwa mwenyekiti wa kuandaa katiba mpya. Amekuwa ni mbishi na asiyeambilika. Sasa what next. Wanaosema ni uchochezi wanashabikia wasichokijua kwa hiyo nashauri wapuuzwe. Hapa siyo suala la chama bali taifa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Katiba siyo msahafu, wacha ipatikane, siku mwenye akili akiingia magogoni inapigwa chini fasta. Jambo la msingi ni kuweka jitihada za kumpata 'mwenye akili mmoja' aingie pale aanze kusafisha nyumba.
 
hoja za upinzani nyingi huwa zinafanyiwa utafiti wa kina kabla hazijaletwa hadharani,hili swali limeanza kupigiwa kelele mda sana,na hata cuf nao wamelisemea sana,lakini warioba kaziba pamba masikioni,ubinafsi na wa viongozi wetu hasa wa chama tawala ndiyo umetufikisha hapa tulipo,kwa kuamini wao wako perfect kwa kila kitu,kuna watu wanaweka utaifa mbele kimuonekano ila kimatendo ni tofauti kabisa.

katiba hii haikutakiwa kuingiliwa na chama chochote cha siasa,na wajumbe wa tume hii pia walitakiwa wawe huru na wengi watoka kwenye taasisi kama jukwaa la katiba,ama asasi za kiraia na sio vyama vya siasa,vyama vingetoa wawakilishi tu,lkn leo kumejaa waasisi wa Tanu na badae ccm unadhani tutakuw na katiba nzuri plus tume huru ya uchaguzi?<tutaitamani katiba ya kenya mpk kufa kwetu ila daima hatutafikia ubora wake labda kizazi cha watoto wetu not us>
Mwigulu,asha rose migiro,nape,kinana,mnakoipeleka nchi hii siko mnakodhani nyie,kizazi chenu kitawalaani sana kwani mawazo yenu hayawezi kuiwakilisha Tanziania nzima na wala hayataendana na kasi ya ukuwaji wa ubongo wa kazazi kijacho
 
Wkati watu wako busy na mchakato wa katiba, CHADEMA ilkuwa busy na maandamano! Mnategemea nini?

Well, katiba haizungumzii CCM bali mustakbali wa wananchi wote na sio kwamba wakishaamua hao wajumbe wa mabaraza ya katiba basi katiba inapitishwa kuwa sheria.

Katiba ni mchakato na mwisho wa siku itakuja tena kwetu kwa ajili ya kuipigia kura. Ni mapema mno kukata tamaa kwamba tuliyoyataka hayatakuwemo.

Hao wajumbe wa CCM walichofanikiwa kupata ni ajira ya muda tu si vinginevyo.
 
CCM ni janga la Taifa. Ee Mwenyezi Mungu tuepushe dhidi ya laana hii tuliyosababishiwa na ccm pasipo ridhaa yetu hata kutupelekea kuishi katika lindi la umasikini uliopindukia ndani ya Nchi yetu iliyojaa ASALI NA MAZIWA.
 
Waraka wa Pongezi toka kwa Kamati Kuu ya CCM kuelekezwa kwa Watendaji wa chama hicho umenaswa. Waraka huo unapongeza kufikiwa malengo ya kumiliki Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Katika Mabaraza hayo Tanzania nzima CCM ina wajumbe asilimia 90. Waraka husika una jedwali linaloonesha mikoa,idadi ya wajumbe wa CCM,vyama vya upinzani na wale wasio na vyama. Alipoulizwa Mwigulu juu ya waraka huo,aliruka bila kutoa hoja ya msingi.

Waraka huu unathibitisha tuhuma zilizotolewa na CHADEMA kupitia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria,Tundu A. Lissu(Mb) pamoja na Jukwaa la Katiba linaloongozwa na Bwana Deus Kibamba kwamba CCM imeuingilia na kuuharibu mchakato mzima wa uundwaji wa Katiba mpya hasa katika uchaguzi wa Wajumbe waMabaraza ya Katiba.

Chanzo: Gazeti la Mawio la Alhamisi tarehe 30/5/2013;Toleo Nambari 0045

Mimi: Waungwana wa Tanzania, hapa patapatikana Katiba ya nchi au ya chama tawala?

Cc Mwigulu Nchemba Nape Nnauye Ritz Sumu MwanaDiwani et al

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Huo waraka huko wapi? Umewekwa kwenye hilo gazeti, kama kuna mtu anao huo waraka aubandike hapa!!!!

Tiba
 
Hivi hao CCM tu ndiyo Wataipigia kura ya NDIYO au HAPANA hiyo katiba mpya, mbona wanajidanganya!

Au matumanini yao yapo kwenye NEC kwamba itachakachua KURA YA MAONI.

Kama rasmu ya katiba mpya haitakidhi maoni ya WATANZANIA tutapiga kura ya HAPANA. CCM msijidanganye, hurumieni kodi zetu mnazotumia sasa kutengeneza hiyo katiba ya ki-CCM, CCM
Kama wameweza kuchakachua mchakato wa katiba hadi hapa tulipofikia na wananchi tumetulia, usitegemee huko mbele ndo watashindwa kuchakachua. Lets see ila CCM watatuletea kizaazaa hapa Tanzania kwa uchu wao wa Madaraka.
 
Wkati watu wako busy na mchakato wa katiba, CHADEMA ilkuwa busy na maandamano! Mnategemea nini?

Well, katiba haizungumzii CCM bali mustakbali wa wananchi wote na sio kwamba wakishaamua hao wajumbe wa mabaraza ya katiba basi katiba inapitishwa kuwa sheria.

Katiba ni mchakato na mwisho wa siku itakuja tena kwetu kwa ajili ya kuipigia kura. Ni mapema mno kukata tamaa kwamba tuliyoyataka hayatakuwemo.

Hao wajumbe wa CCM walichofanikiwa kupata ni ajira ya muda tu si vinginevyo.

Nyumba huwa ni Msingi.Msingi ndio unaodefine nyumba.au mwenzetu kwenu mnaanza kujenga juu halafu ndio unamalizia msingi?
"Nyota njema huonekana asubuhi"
 
Sasa msingi wa katiba mpya ni nini, ili tujuwe kama ni hayo mabaraza? Sisi nyumba kwetu hatuanzi na msingi, tunaanza na Plan ya jengo lenyewe kwanza.

Utaanzaje kujenga nyumba kwa kuanza msingi ilhali hujuwi kama bajeti inatosha kwa aina ya jengo unalolitaka? GT vipi?
 
Back
Top Bottom