CCM yaendeleza ubabe dhidi ya serekali za wananchi

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,195
590
CCM Zanzibar kimewaonya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa chama hicho watakaounga mkono hoja ya kuundwa Serikali ya mseto, kinyume na azimio la Butiama la mwaka 2008, kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema hayo visiwani hapa jana alipokuwa akizungumzia maazimio ya kikao cha Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Zanzibar, kilichokutana juzi, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Amani Abeid Karume.

Majuzi nilitoa thread kuonesha suala la Richmond jinsi matakwa ya wabunge yalivyotupiliwa mbali, na watu kufanya wanavyotaka.

Hii itakuwa ni thread ya nyengine, jinsi chama cha CCM kinavyoendeleza ubabe dhidi ya matakwa ya wananchi.Hivi kelele zote zile za kuheshimu katiba ndio hizi za kujadili na kuingilia kati maamuzi ya vyombo vya kutunga sheria kwa kuwatisha wawakilishi au wabunge?

Hadi lini wananchi tutaendelea kuona wajumbe wetu wakipewa mikwala wasifanye maamuzi sahihi?
HTML:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom