Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Kilonzire kata ya Mabwepande Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam, kimezoa wanachama wapya 41.
kati ya wanchama hao wapya, saba wametoka katika Chama cha demokrasia na manedeleo (CHADEMA) wanachama hao wapya walipokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho kata ya kunduchi Michael Urio, aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kuwapokea wanachama hao.
akizungumza katika mkutano huo, Urio alisema CCM itaendelea kuwapokea wanachama wapya kwa vile ndicho chama baba na mama.
Alisema ni vema wale wote ambao waliopotea kwa bahati mbaya na kujiunga na vyama vya upinzani wakidhani ni vyama sahihi kwao kwa ajili ya maendeleo, wakatumia kipindi hiki kurejea CCM.
Pia aliwaaka wanachama na wapenzi wa CCM kuendeleza mshikamano wakati wakielekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani.
Katika habari nyingine;
Chama Cha mapinduzi kata ya Duga, halmashauri ya tanga kimejizolea wanachama wapya 165 na kupeleka salamu ka wapinzani kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 watahakikisha wanachukua maeneo yote katika halmashauri hiyo.