Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,490
- 96,054
Wana bodi ccm hali ni tete tena mjini lindi baada ya ccm kupigwa 7-0 na UKAWA ktk uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa kati ya mitaa 7 ilivyokuwa inagombaniwa UKAWA imechukua yote 7 na ccm kuambulia 0.
======
TUMEPATA USHINDI MKUBWA LINDI!
Ndugu zangu, leo Jumapili tarehe 12 Machi 2017 kumefanyika uchaguzi wa wenyeviti wa serikali za mitaa 7 katika manispaa ya Lindi, mkoani Lindi.
Hii ni baada ya kampeni za wiki mbili mfululizo. Katika mitaa yote 7 iliyofanya uchaguzi, CHAMA CHA WANANCHI CUF kimeiburuza CCM kwa kunyakua mitaa yote 7, CCM ikiambulia SIFURI.
Kwa niaba ya chama niishukuru timu ya kampeni ya chama chetu iliyokuwa chini ya viongozi wa Lindi mjini lakini mahsusi ikiratibiwa na Mhe. Khassim Hassan Fundi.
Kipekee kabisa nimshukuru Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Omary Kumbilamoto ambaye aliniwakilisha katika ufungaji wa kampeni. Nimshukuru sana mpiganaji asiyechoka Mohamed Mluya na madiwani wa CUF kutoka Dar Es Salaam ambao tuliwatuma kusimamia kampeni hizo.
LINDI ITUFUNDISHE MAMBO MATATU;
1. CUF itakuwa salama zaidi bila BWANA YULE, rejea uchaguzi wa madiwani ambao Bwana Yule aliingia na Milioni 400 za wizi akaambulia kata SIFURI na linganisha na uchaguzi huu tuliousimamia upande wa chama tukiwa hatuna pesa na kuchukua mitaa yote 7.
2. Ushirikiano wa vyama mbadala ni silaha tosha ya kuisambaratisha CCM. Katika uchaguzi huu wa marudio, vyama vya CHADEMA na NCCR vilijiweka pembeni na vikasimama majukwaani kuiunga mkono CUF, matokeo hayajaongopa.
3. Propaganda za Bwana Yule kwamba CUF inamezwa na CHADEMA na kwamba yeye anarudishwa na msajili kuja kuiokoa CUF ni upuuzi wa kiwango cha PHD.
Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front,
12 Machi 2017.