CCM yaanza kuaga Ikulu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaanza kuaga Ikulu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, May 29, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Na Alfred Lucas | Imechapwa 23 May 2012 | MwanaHalisi


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kufanya maandalizi ya kuaga ikulu na kuwa kiongozi mkuu wa upinzani bungeni, MwanaHALISI limeelezwa.

  Hatua ya chama hicho, chini ya mweyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, kupendekeza ushindi wa rais kuhojiwa mahakamani, tayari imechukuliwa kuwa ni kuona uwezekano wa kushindwa katika chaguzi zijazo.

  Miaka miwili na nusu kabla ya uchaguzi mkuu (2015), CCM imesema itapendekeza kwa Tume ya Kuratibu Maoni Juu ya Katiba Mpya, kwamba uwepo uwezekano wa kuhoji ushindi wa rais mahakamani.


  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ambayo imekuwa ikitumika nchini, inakataza ushindi wa rais kuhojiwa mahakamani. Nafasi nyingine – ubunge na udiwani – zimekuwa zikihojiwa.


  Tume ya kukusanya maoni iliyoanza kazi Mei Mosi mwaka huu, imepewa miezi 18 kukamilisha kazi hiyo; na Rais Jakaya Kikwete amewahi kusema kuwa katiba mpya ndiyo itatumika wakati wa uchaguzi mkuu 2015.


  Pamoja na kupendekeza suala la ushindi wa rais kuhojiwa na yeyote mahakamani, CCM imependekeza pia kuwepo kwa utaratibu wa mgombea binafsi.


  Mapendekezo ya CCM yanatokana na vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vilivyokutana mjini Dodoma wiki iliyopita.


  Kutohojiwa mahakamani kwa ushindi wa urais, ambako kumerithiwa kutoka mfumo wa chama kimoja, kumekuwa kukilinda mgombea, hata kama kulikuwa na hila au ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.


  Aidha, kuzuia mgombea binafsi kumekuwa kifungo maalum kwa wabunge wa CCM ambao pindi walipotofautiana na uongozi, ama walilazimika kujiuzulu au walifukuzwa uanachama.


  MwanaHALISI limezungumza na wachambuzi mbalimbali wa mambo ya siasa, wakiwamo viongozi wa sasa wa CCM na wastaafu kuhusu mapendekezo haya.


  John Mnyika, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA amesema, kwa CCM kukubali mambo hayo makuu, ni kujenga mazingira ya kupata fursa ya kupinga matokeo ya urais katika uchaguzi ujao.


  "Wamepima na kuona hawatashinda. Sasa lazima waanze mapema kutafuta fursa za kupinga matokeo ya urais," amesema Mnyika kwa njia ya simu.


  Aliyekuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM kwa muda mrefu, Pancras Ndejembe anasema, "Umefika wakati lazima tukubali mabadilko. Ukikataa mabadiliko, maana yake unaleta matatizo. Tutaonekana wabinafsi kuanzia kifuani hadi shingoni.


  "Kama tunataka kubaki na amani, umoja, mshikamano tulioachiwa na waasisi wa taifa hili, lazima tukubali mabadiliko…no other way out (hakuna njia mbadala," amesema Ndejembi.


  Gazeti hili lilikuwa likitaka kujua kutoka kwa wote waliohojiwa, maana ya CCM kukubali utaratibu wa mgombea binafsi na ule wa kuhoji matokeo ya urais mahakamani.


  Kwa upande wake, mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya CCM, Peter Kisumo anasema, "Mazingira ya sasa yanaruhusu chama au nchi kuendeshwa kwa mfumo wa kisasa.


  Amesema, lazima kuwe na mgombea binafsi, maana siasa za dunia zimebadilika. Wakati wa one party system (mfumo wa chama kimoja), umepita na sasa huwezi kuzuia hali na kasi hii ya mabadiliko.


  Kisumo anasema utaratibu wa sasa wa aliyepata kura nyingi kutangazwa mshindi ndio uendelee, badala ya ule wa kuchukua aliyevuka nusu ya kura zilizopigwa.


  Lakini, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye alipohojiwa juu ya mapendekezo ya CCM alisema, "Hivi ikitokea mtu akakuuliza kwanini tunaingia kwenye mjadala wa mchakato wa katiba mpya, utamjibu nini?"


  Kabla hata ya kujibiwa, aliongeza "…hilo jibu ambalo unataka kuniambia basi ujue kuwa ndio jibu la CCM."


  Alipohojiwa iwapo haoni kuwa sasa ndio CCM inaelekea kushindwa, Nape alijibu, "Hilo ndilo ulilotaka kujua? Nasema andika tu…"


  Lakini katibu mkuu mstaafu wa CCM, Luteni Yussuf Makamba alijibu kwa ufupi, "Hayo mambo yana wenyewe. Hilo wanaweza kuzungumza akina Mukama (Wilson). Lao hilo!"


  Naye katibu mkuu wa CCM, Wilson Mukama amesema, "…chama kimetoa maoni yake. Hata hili la mgombea binafsi likipitishwa, CCM itaendelea kushika dola mpaka mwaka 2015, na hata zaidi ya hapo."


  Mabere Marando, wakili wa Mahakama Kuu na mwasisi wa mageuzi nchini amesema, "Wamejua kwamba wakiendelea kupinga haya, watapata shida baadaye.


  "Hoja hiyo tuliibua sisi. Tuliipigania sisi; lakini sasa wanakubali kwa sababu hawana hoja tena ya kuzuia, amesema na kuongeza, "CCM inakwenda kushindwa ndiyo maana hata imekubali hoja ya matokeo ya urais kupingwa mahakamani."


  Marando ambaye chama chake kilimsimamisha Dk. Willibrod Slaa katika uchaguzi mkuu uliopita amesema, "CCM imeshakuwa chama cha upinzani. Dunia nzima, katika nchi yoyote ile, ukiona ndani ya chama tawala wanavurugana hadharani, wanagombana hadharani, ujue ni dalili za kushindwa."


  Ametoa mifano ya Kenya, Zambia na Malawi ambako amesema vyama tawala vilianguka na kuongeza, "…na hapa Tanzania unaona hata viongozi wa CCM wanakwenda upinzani. Muda umefika kwa CCM kukaa kando."


  Mbunge wa zamani wa Monduli, mkoani Arusha, Luteni mstaafu Lapilall ole Molloiemet anasema, "CCM sasa ijiandae kuwa chama cha upinzani baada ya kuwanyima watu utu wao na kuwadhulumu ardhi."


  Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro anasema, "Muda wa CCM kuongoza dola umefika ukiongoni. Wananchi wamepoteza matumaini. Sasa wanasubiri kuihukumu 2015. Basi!"


  Jaji mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani aliulizwa iwapo walikuwa wanatetea CCM, pale yeye na majaji wenzake sita walipotoa hukumu iliyoonekana kuzingatia matakwa ya chama hicho.


  Katika sauti ya utulivu, jaji ambaye sasa ni makamu mwenyekiti wa kamati ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya katiba mpya, alisema, walichofanya majaji si kupinga mgombea binafsi kwa mujibu wa kesi iliyofunguliwa.


  "Tulichofanya sisi ni kuona kwamba kuna vifungu viwili vinapingana katika katiba moja. Hivyo tukasema kwamba jaji mmoja, majaji watatu au sisi majaji saba hatuna uwezo wa kubadilisha sheria.


  "Wenye uwezo wa kufanya hilo ni bunge ambalo lilitunga sheria ambazo zinatumiwa na mahakama. Katiba hiyo hiyo inasema wagombea watokane na vyama vya siasa; wakati huohuo inasema kuna haki na mtu kugombea; haki ya kuchagua na kuchaguliwa," ameeleza.


  Jaji Ramadhani anasema waliamua kuwa suala hilo ni la kisiasa na kwamba linaweza kuamuliwa bungeni ambako kulitungwa vifungu vyote vya katiba.


  "Tuliona pia kwamba kwa uamuzi huo, hakuna kifungu kingine kilichokuwa kinavunjwa," amesema.

   
 2. m

  majebere JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Na nyie kwa kujipa imani za ajabu ajabu, jaribuni baada ya miaka hamsini mbele. Hii nchi ni ya CCM, ipigwe kura au isipigwe, rais wa Tanzania lazima atokee CCM. Au hamuoni hiyo viongozi wa CCM wanavyo gombania hiyo nafasi?
   
 3. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  ebu tueleze mlipata lini hati miliki gamba wewe.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  CCM na KANU lazima wawe ndugu
   
 5. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama kwali watanzania tuna taka maendeleo ni lazima tuiondoe ccm madarakani.maana sasa ccm imekuwa kama kiuganga bila hicho tunahisi tutakufa
   
 6. k

  karafuu Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walipata kwa nyerere
   
 7. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa akili za kutoweza kusoma alama za nyakati wala kuchambua mambo uko sahihi kabisa,lakini si kwa ualisia wa dunia ya leo!walikuwepo miungu watu wanaotawala kwa mikono ya chuma na kuogopwa vibaya mno leo wako na wafungwa magerezani na wengine wapo kuzimu!mabadiliko hayazuiliki kwa fikra nyepesi kama zako
   
 8. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nyerere mwenyewe alisha watabiria kifo cha mende,na ndicho hiki sasa
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,620
  Trophy Points: 280
  wameshanusa kitakachotokea
   
 10. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  hata hivyo si wanatawala kwa nguvu za maruhani, wazee wa dar es Salaam na Washili!
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  CCM watarajie kuwa kama KANU
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kikwete Amenunua furniture Mpya pale Ikulu sasa zile za zamani kapeleka wapi? Na hizo Mpya Atachukua Pia?

  Serikali ya Gas na Dhahabu ina pesa hiyo
   
 13. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  their end is very near
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hodi hodi ikulu, riz1 ajiandae kwenda kutumikia magereza yeye na babake.
   
 15. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Sasa Nape akibaki peke ake itakuwaje
   
 16. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Wamekwisha hao!!!!!
   
 17. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  naona kimenuka hapo kwa baba riz
   
 18. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  pamoja na kwamba tunapenda CDM ichukue dola. bado kazi ni pevu kuwahamasisha wapiga kura wengi ku support chama makini. Tanzania ni nchi kubwa sana na kuna sehemu nyingi tu bado wanaamini kuwa:-

  1. sisiem imeshika hatamu na Nyerere ni rais wao!
  2. Vyama vya upinzani vitaleta vita TZ kama vitapewa nafasi ya kuongoza nchi
   
 19. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mfa maji!
   
 20. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  very clever...ccm wakishindwa wakapeleka kesi mahakamani then kikwete bado anaendelea kua kwenye power...na mahakama zetu si mnazijua kesi mpaka isikilizwe ni miaka 5 so msishangae tukawa na kikwete for another 10yrs
   
Loading...