Anaeogopa Serikali Tatu anakusudia kuichakachua Rasimu ya Sasa ya Katiba, na hana lengo zuri na Taifa hili la Tanganyika ambalo kimsigi liko hewani hlina Rais, Halina Serikali, Halina Jeshi wala vyombo vya Dola kama sehemu mojawapo ya muungano, aana muungano lazima uwe wa serikali au mataifa mawili! maana vyote tulivyonavyo ni vya muungano, na ni Muungano wa Zanzibar ambayo ina serikali na misingi migni tu ya Dola ikiwemo bendera, rais, bunge n.k. ila upande mwingine?
Tusidanganyane, tuache ushabiki hebu tufikiri kidogo zaidi ya ushabiki. Maana haijalishi nani anaunga mkono hoja gani swala la katiba si la CCM wala CHADEMA wala CUF wala chama chochote ni swala la Kitaifa.
Hebu tizama, CCM Kamati Kuu ilikaa wakajadili hawakufikia muafaka, na mara nyingi huwa muafaka haufikiwi kwakuwa Mwenyekiti na wajumbe wanashindwa kukubaliana msimamo. Cha ajabu walikubaliana wapeleke Rasimu kwa wanachama, sasa sijui kikao gani hivho kilichokaa kikanyumbulisha maoni ya Wanachama na kuaj na msimamo huo unaoropokwa na baadhi ya viongozi wa CCM bila aibu kwa kutumia hisia zao na kulazimisha uwe msimamo wa chama??? Tena kwa Kiburi kuna walioandaa Waraka na kuusambaza kwa wananchi, Waraka huo haujakanwa na hatuna uhakika umeandaliwa na kubarikiwa na nani maana bado viongozi wanahaha na kujichanganya.
Cha msingi hapa bwana waliopo madarakani wanaogopa Mzimu wao na Kivuli chao kinavyowafuata hata chenyewe hawakiamini. Raimu ya Katiba kama ilivyo inatoa mwanga mpya wa matumaini na Uwajibikaji kwa Wananchi kwa wale wanaotaka kuchukua madaraka. Wengi wa hawa walioko madarakani sasa hawafurahishwi na jambo hilo na wangependa kutu-manipulate na kutuhadaa kwa hoja zao ambazo nyingi kwa sasa zina shida sana, hazina maslahi ya watu bali ya kwao binafsi. Viongozi Hawa hasa baadhi ya wale wa CCM wa ngazi ya juu wanaogopa kupteza madaraka mengi waliyojilimbikizia. Mfano wabunge wenye vyeo lukuki na mishahara na marupurupu kupitiliza ambayo hayalingani na uwajibikaji wao. Wewe ni Mbunge, wewe nni Waziri, wewe ni Mmiliki wa Kampuni fulani ya Biashara, wewe unahisa kwenye Kampuni ya Mwekezaji ambaye Mradi wake uko chini ya Wizara yako, achilia mbali kamati na tume, sielewi na haiingii akilini.
Ili kufanikisha hilo la kulinda maslahi yao, wanaficha hoja yao ndani ya Serikali Tatu! ili Rasimu isipite, isipopita watatumia kila hila kushinikiza matakwa yao.
Kwani mara ngapi tumewasikia baadhi yao wakiropoka kuhusu viti vyao walivyonavyo sasa ambavyo ni wazi Rasimu inavipiga chini? Wanahaha hawaoni mwanga mbele.