CCM ya Kikwete na Magufuli, Full 'Udikteta'!!

CCM ya Kikwete na Magufuli, Full 'Udikteta'!!

KILIVITE

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
1,302
Reaction score
556
Naomba nitumie haki yangu ya kutoa maoni. Ni dhahiri JPM endapo atapata fursa ya kuingia Ikulu atakuwa ni Kiongozi wa Ki Imla ambaye hajawahi kutokea duniani.

Mimi binafsi bila kushawishiwa na mtu yeyote naziona dalili zifuatazo ambazo tayari anazo kabla hata ya kupigiwa kura na kuapisha kuwa Rais;

1.Kuzuia taarifa muhimu ama kutoa taarifa zisizo sahihi kwa lengo kueneza propaganda ambazo ni hatari kwa Taifa.

2. Wizi wa kura kwa ajili ya kuzuia Mabadiliko ya Chama na Serikali.Tayari kuna mipango kabambe ambayo inalalamikiwa na Upinzani kwa lengo la kuzima demokrasia.

3. Kuingilia maamuzi ya Mahakama na vyombo vya dola. CCM ya Magufuli inatoa amri kabla hata ya kuingia madarakani.Hii ni hatari sana.

4. Mgawanyo finyu wa madaraka. JPM alinyang'anya Mamlaka ya TBA kugawa nyumba na kisha akaingilia kugawa nyumba zaidi ya 8200 kwa watu wake akiwamo kimada wake Sundi Malomo na mdogo wake Musa Magufuli.Hili limejionesha pia katika Majukwaa ya Kampeni.

5. Mamlaka ya kuzuia umiliki wa Vikundi vya Ulinzi na umiliki wa siraha kwa maelezo ya kuhatarisha usalama wa raia na Nchi lakini huwa sivyo.Tumeona wakizuia Red Brigade lakini wakitumia Majeshi kutoa vitisho na kukamata Wapinzani.

6. Kusingizia vita dhidi ya ugaidi ama Majambazi ama Wahalifu wa mtandaoni lakini wakilengwa wapinzani na wasiounga mkono CCM.

7. Kuwatumbukiza wafuasi wao wakiwa katika sura ya upinzani ili walete fujo na kisha kutangaza kuwa kuwakamata na kisha baadae hutangaza kuwavunja nguvu wapinzani mbele ya jamii ya wapiga kura.

8. Zoezi la kuwazima,kuwatishia wafichua maovu hii ikiwa ni ishara ya Chama ama Serikali kugubikwa na rushwa kubwa inayofanywa na tabaka la vigogo wakubwa.Kumbuka Escrow.

9. Matumizi ya vyombo vya sheria kuwazimisha wapinzani wa Chama ama Serikali yao kwa leno la kuwapendelea watu wa Serikali yao chama chao na wafuasi wao.

10.Kuondoa Uangalizi na Mizani (Check and balances) ya vyombo vya Serikali kwa kuwaondoa watu wanaohoji ama wanaoonekana kufuata taratibu na Sheria bila kupendelea upande wowote.Kumbuka Kuondolewa kwa Wakurugenzi wa NEC.

11. Kuundwa kwa tabaka ambalo lipo juu ya sheria.Kumbuka wezi wa Escrow na EPA ambao hawajafikishwa katika chombo chochote cha sheria ilhali wezi wa kuku wanasota jela.

12. Kuwafanya wananchi kuwa tegemezi kwa Serikali na chama.Hii ni kujenga utii kwa Viongozi wa Chama na Serikali kwa kufuata kile wanachokitaka.

13. Kuongezeka kwa watu kutokujua haki zao za kimsingi na kutokuzifuatilia na Serikali wakati mwingine kukataa kuwaelimisha wananchi.Kutokutoa elimu ya kutosha ni mbinu ya kuwafanya wananchi wasijue haki zao za Kimsingi na kutokuhoji.Watu wanapokosa kujua kuwa kupiga kura haki yao basi Viongozi wasiohitajika huingia madarakani kwa urahisi.

14. Matumizi ya Matukio yaliyopangiliwa vyema kwa lengo la kupata sapoti ya Wanachi wengi wasiojua ukweli. Mfano, Matukio ya kigaidi kumbuka Amboni Tanga na Morogoro, Viongozi kujivua uanachama wa Upinzani (Dr Slaa na Lipumba) hii huambatana na mikakati mathubuti ya kubana demokrasia kwa kisingizio cha hayo yaliyopangwa.Yapo yatakayokuja siku chache kbla ya uchaguzi.

15. Haki kugeuzwa kuwa upendeleo. Mfano kufanya Mikutano,kuandamana na kupata vibali vya kumiliki ama kufanya mambo mbalimbali katika jamii.

16.Kununuliwa kwa watu maarufu ili kujihusisha kukashifu watu ama upinzani kwa lengo la kutengeneza njia kwa tabaka tawala kushinda. Mfano Polepole, Slaa, Wasanii wa Maigizo na Muziki na Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kama Bulembo, Nape, Lusinde,n.k.

UJUMBE MUHIMU: Mwana "Mabadiliko" Amua sasa, ugandamizaji wa namna hii hauna tija kwao. Jitihada zote hizi zinafanywa kwa manufaa ya nani ilihali umeme hakuna, maji hakuna na Maisha ya leo ni bora ya jana?

Mimi nampigia KURA yangu ya thamani EDWARD NGOYAI LOWASSA. Wewe je?
 
lowassa anatosha, pombe atasubiri 2035 tutampa nchi akiwa ameshakomaa ki akili.

Kwa mazingra ambayo imefikia,tunahtaji mtu aina ya Magufuli na baada ya miaka 5 nidhamu itakuwa imerudi, tutampa mtu mpole mwingne.Watanzani mko nyoronyora sana,mnatakıwa kuwekwa sawa.
 
Huu udicteta wa Magufuli ni wakijinga, Magufuli anaonesha wazi kuwa yeye sio mjuvi wa mambo na pia haambiliki. Kwa sasa tunahitaji Raisi atakaye sikiliza ushauri wa wasomi na wataalam na kufanya maamuzi magumu na sio Raisi mpenda sifa na mkurupukaji.
 
Back
Top Bottom