CCM wote wameoza, hamkuamini, sasa tizameni.......! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wote wameoza, hamkuamini, sasa tizameni.......!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by jaxonwaziri, Jul 30, 2010.

 1. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Ndugu watanzania wenzangu, tumeona vielelezo kadha wa kadha kwamba wana CCM wameoza kwa rushwa na ufisadi! Hata wale ambao hatukuwategemea kabisa tunaona wanakutikana na matukio ya ajabu!
  Hebu angalia wabunge, wengine ni mawaziri wanakua na akili ya kuamini kuwa "rushwa" ndiyo inaweza kuwapatia kura za wapiga kura?
  Ina maana kuwa wagombea wa CCM wanaamini kabisa kuwa agenda zao, sera zao haziwezi kuwapatia kukubalika kwa wananchi na kwakuwa wanajuam kuwa watanzania wengi wana njaa, basi wanajua njia pekee ni kuwa mwema kwao kwa kuwapatia chochote kwa kipindi hiki ili watanzania wajisahau na kuwachagua tena! Aibu gani hii mtanzania!
  Nikawa nashangaa kwanini watu wengi sana kipindi cha miaka miwili iliyopita walikuwa wakosoaji wakubwa wa serikali ya CCM lakini tulipokaribia 2010 watu wameanza kulegea!
  Kumbe ni kwa sababu hawa wote wana njaa na ushabiki wao kwa CCM na viongozi wake ni kwa sababu ya njaa zao....!!!!
  Tutakuwa lini makini na hatima ya taifa letu?
  Wito wangu kwa watanzania wote ni huu: Chagua upinzani tuone mabadiliko ya kweli! Eti naambiwa hata yule DC wa kasulu nae tayari ameuopata ubunge wa viti maalum!
  Hivi mtu kama yule ( na wapo wengi sana wa aina hii katika CCM) atafanya nini kwa manufaa ya Tanzania?
  Wewe uliyekubali kupokea chochote kumpigia kura mtu mbovu wa aina hii, utakuwa na haki gani ya kumdai kiongozi huyu maendeleo ilhali mkataba wenu ni kuwa ; akupe pesa wewe umpe kura?
  Wakati mwingine hawa wagombea wa CCM wanatushangaza sana, ukitaka kujua ufinyu wa upeo wao wakufikiri hebu waulize: " Tungekuwa tuna barabara za kutosha, maji ya kutosha kila pahala, huduma za hospitali na shule vilivyoimarika, kiwango kizuri cha elimu, Je, wewe mgombea ungekuwa unaomba kura kwetu leo hii ili ukafanye mambo gani?"
  Utashangaa ataanza kubabaika, hana upeo mwingine, kwakuwa wanajua walichonacho cha kusema ni "matatizo yetu" tu, na ndio maana hawana mpango wa kuyamaliza maana uchaguzi ujao huu na nyingine zote zijazo watazungumzia nini majukwaani?
  Watanzania, hamjaamka na kufumbua macho tu ili kuona haya?
  Ndio maana nchi hii ikiwa chini ya CCM haitaendelea kamwe, kwakuwa woooote wanawaza matumbo yao na maslahi binafsi.
  Watanzania wanapumbazwa na Tsh. Laki moja unayopewa hivi leo halafu unayaweka rehani maisha yako na ya wanao! Watu wanaokupa rushwa ili kupata kura yako, watashindwa vipi kutia saini mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini, uranium, uendeshaji wa mashirika ya reli, ndege etc?
  Nawaasa, hawa viongozi wa CCM wanazungumza kuupinga ufisadi na rushwa wakati uchaguzi umepita ila ndani ya dhamira zao, hawana nia ya dhati kamwe ya kupambana nao.
  Huwa nashangaa sana kusikia nyimbo za "....ni chaguo la Mungu...."Mara oooh, '....Kiongozi wetu mpendwa na mchukia rushwa....' Waaapi, kumbe danganya toto!
  Wanajipendekeza tu hawa wooote maana wanaujua ukweli kuwa "uchaguzi CCM ni rushwa,mkwa hiyo ukipata uongozi, tafuta fedha kiasi cha kutosha hata kama ni kwa ufisadi ilimuradi uwe na fedha ya kuhonga kipindi cha uchaguzi...!
  Nimeanza kuamini kuwa Siasa kwa Tanzania ni "Uwekezaji.." na kiongozi wao alishasema Bungeni, ..."Ukitaka kula lazima uliwe.." yaani ukitaka kupata chochote lazima kwanza wewe utoe chochote! Aibu gani hii watanzania? Vivyo hivyo, kwa wabunge na madiwani, wakitaka ulaji wa uongozi lazima na wenyewe watoe chochote kitu kwanza...!

  Iko siku watanzania mtakuja kugundua uozo wa ubaya wa mnayoyafanya lakini kwa kipindi hicho mtakuwa mmechelewa sana, maana nchi nyingine zitakuwa zimetuacha mbali sana!
  Inatia aibu kuona baadhi ya nchi nyingi za kusini mwa afrika tulizozisaidia kupata uhuru na kujikomboa zimetuaacha mbali sana kimaendeleo!

  Mwisho, wito wangu kwa wapiga kura wote Tanzania, chagua MPINZANI pahala popote pale na katika ngazi yoyote ile ili tuone mabadiliko ya kweli!
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Umeongea ya kutosha. Kiukweli ccm wakishinda kipindi hiki
   
 3. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanashinda tena kwa kishindo,wewe ndiye unayeona uovu wa sisemi,watu wa hali ya chini hawasikii wanaona hawa jamaa wametumwa na mungu,pamoja na umasini wao
   
Loading...