Ccm wilayani iramba-singida yakanusha kumvaa nape nnauye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wilayani iramba-singida yakanusha kumvaa nape nnauye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iramba Willison Msengi (katikati) akitoa tamko juu ya taarifa ya kukipaka matope chama hicho. Wa kwanza kushoto ni katibu wa CCM wilaya hiyo Sikujua Samwenda.

  **********************************
  Na Nathaniel Limu

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Iramba mkoa wa Singida kimekanusha taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa ‘kimemvaa’ katibu mpya wa Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye juu ya utendaji wake.

  Mwenyekiti wa CCM wilayani humo Willison Msengi, ambapo amesema tamko hilo la kukanusha taarifa hiyo iliyotolewa na mtu ambaye sio msemaji wa chama hicho wilayani, limetolewa na kamati ya siasa ya wilaya.

  Msengi amesema taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti moja litolewalo kila siku hapa nchini, kwamba kauli za Nape zinalenga kukisabaratisha chama, sio za CCM wilaya ya Iramba, ni za huyo huyo aliyezitoa (jina tunalo) na kwamba amezitoa kwa lengo la kujinufaisha binafsi au na watu waliomtuma.

  “CCM wilaya ya Iramba, kimeshitushwa mno na kusikitishwa na taarifa hiyo iliyotolewa na mtu aliyedanganya kuwa ni katibu wa mipango na uchumi wa wilaya, wakati mtu huyo ni mwongo wa kupindukia, kwa sababu katibu wetu ni Charles Makala” alisema na kuongeza;”Chama kina wasemaji wake na hakina mpango wa kila mtu kujisemea ovyo”.

  Akifafanua zaidi, amesema taarifa hiyo imejaa majungu matupu, uzushi na inalenga kukipaka matope Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Iramba, akidai taarifa hiyo ni yake mwenyewe mtoa taarifa hiyo na kama katumwa, basi majungu hayo yatawapeleka kubaya.

  Akionyesha kuchukizwa msengi amesema “Natamka rasmi kuwa CCM wilaya ya Iramba haijamtuma mtu huyo kutoa taarifa hiyo, na kinalaani vikali tabia hiyo ya kutaka kukipaka matope chama hicho cha CCM, ambacho ni kimbilio la wananchi”
  Mwenyekiti huyo amesema CCM wilaya ya Iramba inaunga mkono juhudi zote zinazofanywa sasa na sekretarieti mpya ya chama akiwemo Nape, za kukiimarisha chama ili kiendelee kuongoza nchi.

  Msengi amesema CCM wilaya ya Iramba, kitashauriana na mwanasheria wa CCM ili kujua ni hatua zipi zitafaa kumchukulia hatua kali za kisheria, mtoa taarifa huyo bandia.


  [​IMG]
  Jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Iramba.
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Chupa na mfuniko
   
Loading...