Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
KATIKA hali isiyo ya
kawaida, Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoani
hapa kimesusa kushiriki
katika mapokezi ya mbio za Mwenge ulioanza
kukimbizwa mkoani
Tanga juzi.
Mwenge huo uliopokewa
Wilaya ya Pangani
ukitokea Mkoa wa Pwani,
viongozi wa CCM, ngazi ya
mkoa na wilaya
hawakuonekana katika shughuli hizo jambo lililozusha maswali mengi
kwa wananchi.
CCM kabla na hata baada ya kuingia kwa mfumo wa
vyama vingi vya siasa,
imekuwa mstari wa mbele katika shughuli zote za mbio za Mwenge wa
Uhuru, ikizitumia jumuiya
zake na hasa ile ya Umoja
wa Vijana kushiriki
kikamilifu tangu mwanzo
hadi mwisho wa mbio hizo.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Mussa Shekimweri, alipoulizwa
juu ya hatua hiyo, alikataa kuzungumza akidai kuwa
Katibu wake, Gustav Muba, ndiye atakayetoa taarifa
hizo.
Hata hivyo, Muba
alipoulizwa na kuambiwa kuwa mwenyekiti wake
ndiye aliyemtaka atoe
kauli, alisema kuwa chama hakina maelezo, badala
yake akadai kuwa
msemaji wa jambo hilo ni Mkuu wa Mkoa, Chiku Gallawa.
Chanzo: Tanzaniadaima