CCM wasitumie vyombo vya Habari, waende moja kwa moja kwa WANANCHI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wasitumie vyombo vya Habari, waende moja kwa moja kwa WANANCHI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaharakati m, Mar 6, 2011.

 1. mwanaharakati m

  mwanaharakati m Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya CHADEMA kumaliza ziara ya harakati za kuwaamsha wananchi kutoka kwenye lindi kali la usingizi juu ya masuala mbalimbali ikiwamo DOWANS,MABOMU YA GONGO LA MBOTO,UGUMU WA MAISHA na MFUMUKO WA BEI n.k
  CCM imeibuka na kuanza kutoa shutoma nzito,zikiwamo za kukihusisha CDM na uhaini na kuhatarisha amani. makada mbalimbali wakiwamo JEYKEY,WASIRA,CHILIGATI,TENDWA nk wameibika na kukishutumu na kutoa vitisho mbalimbali.

  hoja yangu kwa vile CHADEMA ilikwenda moja kwa moja kwa wananchi ikawaeleza,wakaisikiliza na wakaandamana maelfu kwa malaki. CCM badala ya kuita waandishi wa habari na kushutumu badala ya kujibu hoja, wangeenda kwa wananchi, wakawaeleza hayo katika mikutano ya hadhara.

  kwa nini waende? wananchi wa salama kati(Bunda) wanaopata mlo mmoja kwa taabu,hawawezi kununua gazeti, hawawezi kununua TV kwa vile hawana hata umeme wa DOWANS. Nivyema kuwafuata huko. naamini watawajaa kwenye mikutano na kuwasikiliza hasa ukizingatia ni takribani miezi minne tu tangu CCM ilipotangazwa mshindi kwa 61%, hivyo watu wengi wanaipenda.
  :hand:
   
 2. w

  watarime Senior Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  100% Agree! waende.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Hakuna atakayeshiriki maandamano ya ccm, labda wawaahidi watu kuwa siku ya maandamano kutakuwa na usafiri wa kwenda na kurudi, na kutakuwa na chakula na vinywaji, pamoja na vizawadi vidogo vidogo kama vile khanga, t-shirt na kofia
   
 4. m

  mgalisha Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanajua kuna kuzomewa na wananchi....!!
   
 5. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Fulana na kofia tulizopewa wakati wa kampeni zimeisha chakaa, malori yaliyokuwa yanatubeba wakati wa kampeni hatuyaoni na hakuna hata ahadi moja tuliyoanza kutekelezewa katika zile zaidi ya 100 walizoahidi. Sisi wakija hapa kwetu Nyankomogo Serengeti tutawapiga na mawe bure, heri wawadanganye nyie watu wa mjini kupitia maruninga yenu kwani mmenufaika sana na ccm huko mijini. Sisi huku vijijini sisiemu wakija ni kuwapiga mawe na mishare kwa udhalimu waliotufanyia tangu uhuru.
   
 6. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hawawezi kwenda kwa wanainchi hivi sasa kwani zile ahadi walizoahidi hawajatekeleza hata moja na HAZITEKELEZEKI KWA BAJETI TULIYONAYO zaidi ya hapo ni kwamba hali ndio kwanzaaaa inazidi kuwa mbaya...ninachokiona sasa hivi ni serikali kuanza kutumia ulaghai wa kuwa CDM wanataka kuchafua usalama wa Taifa ili kuwanyamazisha wakisahau kuwa shida kwa wanainchi bado ziko palepale, mafisadi ni walewale na hawachukuliwi hatua, rushwa ipo palepale kiaina aina wakifikiri kuwa watu hawawaoni au hawajui nini kinaondoka ktk chungu cha taifa, sasa hivi CCM ni kipofu, kiziwi, au mvuta bange au sawa na kichaa ambaye anaweza kuuwa saa yoyote tuweni waangalifu na kujaribu kusoma uelekeo wake kwani kuna kila dalili ya wao CCM kuanzisha songombingo hilo na wakiamini kuwa wakizidiwa basi watatumia dola waliyo nayo huku wakisahau kuwa kule Misri vifaru vilipopelekwa mtaani askari waliruhusu watu wavidandie kwa shangwe na vigelegele....CCM tokeni kwenye usingizi mliopewa na mafisadi, mnatakiwa mrudi kundini kabla jua halijazama
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Bila kusahau Original Komedi!
   
 8. Sabode

  Sabode Senior Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hv ile ahadi ya maisha bora imefutwa au??
   
 9. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Wanajua namna wanavyoingia gharama wakitaka kwenda kwa wananchi kwahiyo naamini hawawezi kufanya hivyo. Kwanza wameisharopoka pumba nyingi sana za dharau kwa wananchi kupitia vymbo vya habari, wanaogopa kuzomewa.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanaogopa watazomewa. Ndiyo maana wanatafuta individuals wasemaji wanukuliwe na vyombo vya habari. CCM Kwishney kabisa!!!!!!!
   
 11. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Treni linapita upepo unawawesesha,CCM waje na hoja gani?. Watasema nini,CDM IMETEKA MAWAZO YAO.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Thubutu!hawa hawa CCM nani aende? we watakulaani mpaka basi!
   
 13. f

  furahi JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Na TMK wanaume
   
 14. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Uwatakii mema CCM wanaogopa kipigo,walitega mabomu wakati wa uchaguzi kwa ahadi za uongo wanaogopa wakirudi kwa wananchi yatawalipukia.
   
Loading...