CCM washinda Uchaguzi wa Halmashauri ya Kilombero

Aug 20, 2015
24
30
CCM wameshinda nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya kilombero kwa tofauti ya kura moja, huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na CUF.

Hayo yametokea wakati mbunge wa jimbo hilo Lijualikali akishikiliwa na jeshi la polisi.

Ndg Ligazio -Diwani wa Kata ya Sanje amechaguliwa kuwa M/kiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 na mgombea wa CDM kura 18.

Utakumbuka CDM ndio ilikuwa na diwani mmoja zaidi ya Ccm,Pwahahahahaha...Demokrasia ya Africa
 
Ubakwaji wa demokrasia, mimi nipo maeneo ya halmashauri ya kilombero kinachotokea hapa ni ukiukwaji na ubakaji wa demokrasia kwa kutumia nguvu ya dola...
 
Ndg Ligazio -Diwani wa Kata ya Sanje amechaguliwa kuwa M/kiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 na mgombea wa CDM kura 18.
Utakumbuka CDM ndio ilikuwa na diwani mmoja zaidi ya Ccm,Pwahahahahaha...Demokrasia ya Africa
 
Lijuakali mlevi sana kila sehemu anadhani bangi itamsaidia kumbe siyo kweli.
 
naona Chama cha (ALCCM)wamechukua tena jiulize ni vyama gani majina yake yanaanza na AL
 
uchaguzi umejeuka kuwa vita badala ya tendo la kikatiba na kidemokrasia nukuu mbowe
 
CCM wameshinda nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya kilombero kwa tofauti ya kura moja, huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na CUF.

Hayo yametokea wakati mbunge wa jimbo hilo Lijualikali akishikiliwa na jeshi la polisi.
SAFI SANAAAAAAAAAAAA! LAZIMA UKAWA WAPATE UZOEFU KWANZA WASIJE KUTUHARIBIA HALMASHAURI ZETU
 
Wanaukawa wa Kilombero hasa madiwani hakikisheni mnamkwamisha shughuli Zake huyo Mwenye kiti wa kichina
 
Hebu tueleweshane kidogo.

Hivi huko kuna halmashauri ya wilaya ya Kilombero na ile ya mji mdogo wa Ifakara siyo?

Najua ktk mkoa wa Morogoro upinzani ulishinda majimbo matatu ya ubunge; Mikumi lililoko H/W ya Kilosa nadhani (Joseph Haule Profesa Jay) mbunge wake - CHADEMA; Mlimba lililoko H/W ya Kilombero (Susan Kiwanga mbunge wake - CHADEMA) na Kilombero yenyewe (Lijualikali mbunge wake - CHADEMA)

Sasa ni Halmashauri ipi waliyoshinda CCM na ipi UKAWA/CHADEMA wanaiongoza? Au ndo hivyo tena wameliwa kote kote kwa maana ile ya mji wa Ifakara na ya Kilombero?
 
CCM yakwapua Halmashauri Kilombero
MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kimekwapua Uenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Kilombero, anaandika Happyness Lidwino.

Uchaguzi huo umefanyika leo Morogoro wilayani humo ambapo David Ligazo wa CCM ametangazwa kushinda kwa kura 19 dhidi ya mpinzani wake G. Lwena wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 18.

Katika halmashauri hiyo, CCM ilikuwa na jumla ya wajumbe 19 ambapo vyama vinavyoundwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiwa 20.

Namna ilivyokuwa
Jeshi la Polisi lilitumika kukamata wajumbe wawili ambao ni wabunge, Peter Lijualikali na Devota Minja hivyo kufanya idadi ya wajumbe wa Ukawa kupungua kutoka 20 na kuwa 18.

Hata hivyo, kwenye uchaguzi huo idadi kubwa ya polisi waliingizwa ndani ya ukumbi ikiwa ni hatua za kuhakikisha CCM inapata ushindi.

Pia baadhi ya waandishi na wananchi walizuiwa kuingia ndani ya ukumbi huo ambapo waandishi walioruhusiwa kuingia ukumbini ni wa Star TV, TBC, Gazeti la Uhuru na Jambo Leo.

Pia, wasimamizi wa uchguzi huo hawakujali kitendo cha polisi kuwazuia wabunge hao kuingia kupiga kura zoezi liliendelea na hatimaye CCM walitangazwa kushinda.
 
CCM wameshinda nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya kilombero kwa tofauti ya kura moja, huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na CUF.

Hayo yametokea wakati mbunge wa jimbo hilo Lijualikali akishikiliwa na jeshi la polisi.
Ndicho wanachokitaka kukufanya kwa Dar! Lakini huko limeshagundulika na hata kwa Dawa CCM hawazi Kutoa Meya kwa uwiano wa 84:71 hata mvua inyeshe. Huo wa Kilombero ni wa kupinga mahakamani tena kwa facts.
 
Back
Top Bottom